Uchaguzi 2020 Singida Magharibi wananchi wamlilia Hamisi Lissu Mahanju wa CCM kuhusu ubunge, wadai Kingu ni mwongo

Fundi Madirisha

Senior Member
Jun 30, 2020
184
987
Na Fundi Madirisha, Muhintiri-Ikungi-Sigida.

Katika harakati zangu za kupitapita katika kila kona ya jimbo la Singida Magharibi ili kujipatia taarifa muhimu juu ya mwenendo wa siasa za jimbo ambalo limekua chini ya CCM tangu Uhuru, inaonekana wananchi wa eneo hili wamechoka sana kulingana na hali zao duni za maisha na kutamani kuona maisha yanabadilika siku moja.

Jimbo hili lina taarafa 2, kata 15 na vijiji 51 ambapo kuna vituo viwili tu vya Afya ambao kimoja kilichopo tarafa ya Ihanja na kiingine tarafa ya Sepuka. Jimbo ambalo population yake imeongezeka kwa kiasi kikubwa sana bado linategemea vituo vya Afya viwili tu, hali za Mama zetu kujifungua kwenye huduma bora za afya si njema kabisa, Vipi kuhusu kauli mbiu yetu CCM kuhusu kituo cha Afya kila kata?. Elimu ndiyo kabisa kuna uhaba wa madawati, SINGIDA Magharibi hakuna shule ya kidato cha tank na sits hata moja. Miundombinu Umeme na barabara hali si nzuri sana.

WANANCHI WAMTAKA HAMISI MAHANJU KUA MBUNGE WAO, WADAI KUCHOSHWA NA KINGU KWAMBA NI MUONGO HATEKELEZI AHADI ZAKE.

Haya si maneno yangu na pia isichukuliwe kua ninampigia mtu kampeni,ni kauli kutoka kwenye vinywa vya wananchi wa Jimbo husika.

Jina HAMISI LISSU MAHANJU sio geni sana kwa wakazi Mkoa wa SINGIDA , MARA na DAR ES SALAAM. Huyu ni Afisa Elimu(REO) mikoa ya Mara na Dar es salaam, ni mzaliwa wa kijiji cha Msungua taarafa ya Sepuka Wilaya ya Ikungi. Bwana huyu ni mtu ambaye inasemekana ana akili nyingi sana kuhusu masuala ya kiungozi, ameinua kiwango cha Elimu kwa kiasi kikubwa sana katika mikoa ya Mara na Dar es salaam ambapo kila alipopangiwa aliikuta katika hali mbaya sana za kitaaluma. Mpaka anastaafu mwezi uliopita ameuacha mkoa wa Dar es salaam katika hali nzuri sana kielimu.

Ni mtu mwenye maono na mtatuzi mzuri sana hasa maeneo yenye kero nyingi au migogoro. Katika utendaji wake wa kazi ambao kimsingi unaacha alama kila anapopangiwa majukumu, imepelekea wananchi kumuomba kila wakati awe mwakilishi wao huenda matatizo yao yakapungua kwa kiasi kikubwa.Sasa huyu bwana amekwishatia nia katika Jimbo hilo kupitia CCM, akipewa nafasi huenda kiu ya muda mrefu ya maendeleo kwa wananchi wa Jimbo hilo ikatimia.

Wananchi kudai kuchoshwa na aliyekua Mbunge wa Jimbo hilo aliyemaliza muda wake ndugu ELIBARIKI KINGU ni baada ya mbunge huyo kushindwa kuendana na kasi ya Rais na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli, Kingu ameshindwa kabisa kutatua kero kubwa kabisa za Maji,Elimu, Afya na miundombinu ya barabara na Umeme katika Jimbo hilo.

Wananchi wanadai kwamba pamoja na siyo kazi yake kupeleka miradi hiyo Jimbo ni lakini ameshindwa hata kuisimamia na kuishauri serikali kuwakumbuka kwa jicho la kipekee kila mwaka wa bajeti unapofika. Amekua ni mtu wa kuzunguka kila wakati kwa safari za nje na ndani ya nchi zisizokua na manufaa kwa wananchi na kushindwa kutulia bungeni kama walivyo wabunge wengine. Jimbo halina she hata moja ya kidato cha tano na sita kulinganisha na idadi ya watu iliyopo ndani ya Jimbo,huwezi kuamini katika jimbo lenye kata 15 lakini kuna vituo 2 tu vya Afya.

Usanii mkubwa uliokua ukifanywa na aliyekua Mbunge wa jimbo hilo ni kutembea na fuso iliyojaa mifuko ya saruji ambayo huiazima kwa matajiri Singida mjini bila kuilipia na kuzunguka nayo kila kijiji ambapo huwaambia wananchi kila alipopita ameacha Mifuko kadhaa ya saruji wakati ukiangalia fuso tangu ametoka nalo mijini limejaaa vile vile hakuna mfuko hata moja uliotolewa. Kila Kijiji anakopita wimbo ni ule ule kua ameacha saruji kumbe hajaacha mfuko hata mmoja,akishamaliza usanii huo basi hurudisha saruji hizo zikiwa zimejaa vile vile kule alikozitoa.
Kwa hali hii ni Mwananchi gani atakupenda?

Kingu amelalamikiwa sana kwa kitendo chake cha kutoa amri kwa Viongozi wa kamati ya siasa ya Wilaya kuwakata majina watia nia wote wa udiwani wasiomuunga mkono yeye. Hichi kitendo kimewauma sana wananchi walio wengi. Haya yote achilia mbali matusi kwa wazee na viongozi wa dini katika jimbo hilo kwa kuwaita wanafki.

Wananchi wamechoka katika Jimbo hilo wanasubiri chama chao pendwa cha CCM kuwapa mtu mwadilifu afanane angalau na sifa za HAMISI MAHANJU kwa utendaji wake usiokua na shaka na siyo huyu bwana Kingu anayemaliza muda wake ambapo kuna tetesi kua amegawa rushwa sana kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya ili kujihakikishia ushindi wa kishindo kura za maoni.

MAONI YANGU BINAFSI
Ninakiomba chama chamapinduzi kufanya maamuzi sahihi wakati ili kujijengea heshima yake ya miaka mingi kisije kikapoteza Jimbo hili. Zipo kila dalili za wananchi kuja kupiga kura za hasira kwa sababu hawajafurhia maamuzi ambayo hawakuyatarajia. Nikisihi sana chama hichi kisikilize maoni ya wananchi.
 
Umejitahidi kujipigia debe.kwa umri wako no vema ukastaafu moja kwa moja.huu mi wakati wa vijana.
 
Hata kama hatumpendi mtu,lakini tuseme yale ya kweli, hivi Kingu amekuwa mbunge kwa miaka mingapi? Na hizo shida/changamoto katika jimbo zimeanza lini? Tumwogope Mungu
 
Ila kwa uwongo ni kweli Kingu ni mwongo haswa. Nakumbuka alivyowahi kutengeneza tukio moja baya sana Igunga wakati huo akiwa Mkuu wa Wilaya.
 
Hata kama hatumpendi mtu,lakini tuseme yale ya kweli, hivi Kingu amekuwa mbunge kwa miaka mingapi? Na hizo shida/changamoto katika jimbo zimeanza lini? Tumwogope Mungu

Mkuu, umepiga nyundo juu ya msumari! Maana halisi ya mleta mada ni kuwa toka uhuru miaka 50 na ushehe mambo anayoyataja hayakuwahi kufanyika na anamdai mtu mmoja tu - Kingu!! Ni bahati mbaya wananchi wengi hawana uelewa mpana. Wakiambiwa “mlikosea mkachagua upinzani” wanaamini hivo. Wakiambia upinzani ni pingapinga wanaamini. Wakiambia maendeleo hayana vyama, wanaamini. Wakiambiwa Bungeni wapinga bajeti maendeleo hayatapelekwa majimboni mwao, wanaamini.

Ukweli ni kuwa eneo lao sio kipaumbele au ni salama kwa CCM. CCM wanashighulika na maeneo yaliyo na wapinzani ili kuonesha CCM inapenda maendeleo na ichaguliwe.

Hapa mjini walikuja kufanya kampeni baada ya madiwani kujiuzulu Chadema na kwenda CCM. Wakaahidi maji, hospitali, barabara nk. Walipoondoka baada ya ushindi - hakuna hata kitu kimoja kimefanyika!!
 
Kwani Kingu walimchagua?! Kingu aliteuliwa akapita bila kupingwa, hakuwa akitekeleza yao, bali ya aliyemteua.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom