Wanamuziki acheni kulalamika hampewi sapoti. Mnataka sapoti ipi?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,891
WANAMUZIKI ACHENI KULIALIA HAMPATI SAPOTI; MNATAKA SAPOTI IPI?

Kwa Mkono wa Robert Heriel.

Imekuwa ni kawaida sasa watu hasa wa Tasnia ya muziki kulialia Mbuzi mee kila iitwapo leo.
Ooh! Hatusapotiwi!
Tunazimwa!
Tunafanyiwa figisu figisu!
Kuna Wasanii wanatukandamiza!
Yaani KELELE kelele Kama Mbuzi!

Taikon leo nawakemea na kuwaonya acheni tabia za kipuuzi, kulialia Kama Mbuzi!

Wanamuziki na watu wafani zingine lazima mjue, hakuna wa kukusapoti kwenye dunia hii zaidi ya wewe mwenyewe.

Jisapoti mwenyewe, jipromoti mwenyewe, pambana Kwa Hali zote. Sio uwapandikizie watu ubaya ambao sio wajibu wao.

Ni jukumu lako kujisapoti, labda na wazazi wako au Mkeo au Mumeo. Sisi huku ni mambo yako hayatuhusu, yatatuhusu Kama yatatuvutia.
Hata mafanikio yako utakayoyapata ni yako mwenyewe na familia yako.

Sasa mtu mafanikio utapata wewe na familia yako alafu unataka wengine wakusapoti hivi uliona wapi mambo ya hivyo.

Ukiona hausapotiwi ujue Huduma zako ni mbofu mbofu! Hazigusi watu.

Au unatoa Huduma nzuri lakini haipendwi na jamii husika.

Kwa mfano Mimi Taikon wa Fasihi, ninaandika vitabu vya kifasihi, Riwaya na tamthilia pamoja na scene za filamu.

Siwezi piga kelele watu wanisapoti wakati najua kabisa kazi zangu hata ziwe Bora vipi wakazi wengi WA TANZANIA hawapendi kusoma.

Ni wachache Sana wanaopenda kusoma vitabu hasa Riwaya.

Tena hao wachache wanapenda Riwaya laini laini za Mapenzi.

Wanamuziki acheni kulialia.

Mnataka sapoti ipi wakati maisha ni yenu wenyewe?

Ati Wakulima walie sapoti!

Waalimu walie sapoti!

Wanasheria walie sapoti

Mafundi cherehani walie sapoti!

Huko ni kutafutana lawama!

Alafu watu wanaopenda na kulialia kusapotiwa wakifanikiwa ndio wanakuwa wakwanza kuisumbua jamii. Wanaleta dharau, kejeli na vioja ndani ya jamii.

Mtu anayejiliza liza asaidiwe usimsaidie huyo achana naye.

Mtu anayehitaji kusaidiwa haombi msaada utamuona tuu jitihada zake.

Ogopa mtu anayelialia kwenye maisha yako.

Ogopa mtu anayesema ukimsaidia hatakuangusha, huyo usimsaidie hata Kama ulikuwa unampango wa kumsaidia.

Mtu anayelilia sapoti jua anajaribu kutoa lawama Kwa wengine wanaomzunguka. Mtu huyo ni Mbaya.

Siajabu watu wengi tunaowajua walipokuwa chini walikuwa wanaomba msaada au sapoti lakini walipopanda kimaisha ndio hawa hawa wanatusumbua ndani ya nchi.

Na hii haipo kwenye muziki, hii IPO hata kwenye maisha ya kawaida, kwenye Siasa, kwenye mambo ya Dini.

Unakuta jitu linaomba sapoti lipewe ubunge liwawakilishe, linaomba Kwa unyenyekevu wote alafu likishapata kinaanza kuwatukana na kuwatolea maneno ya kejeli.

Unaliambia Vijana wanahitaji muwafungulie njia aidha muwaajiri au wajiajiri. Linakujibu wajiajiri bila kuweka mazingira Rafiki.

Kuna mchungaji mmoja mkubwa wakati anaanza Enzi zile 2004/2005 alikuwa mpole Sana, mnyenyekevu, akiomba Sadaka mpaka analia machozi, Mungu akamfungulia njia watu wakamuelewa akaanza kupata pesa miaka ya 2013 baadaye limepata pesa linaanza kuongea shit za kipumbavu, ati kufa masikini ni ufala.

Wakati wanaomchangia hizo Sadaka ni masikini Mafukara.

Mtu anayejilizaliza ili umsaidie au umsapoti kaa naye chonjo, mtoe nduki au mchape kitasa akafie mbele.

Tena akiweka Sura ya Ngedere kujitia huruma usimsikilize. Fukuza huyo.

Wanamuziki nimewatumia hapa Kama chambo au kiwakilishi cha watu wanaopenda kulialia na kupiga mayowe ya kupewa sapoti. Ila ujumbe huu unahusu watu wote.

Hakuna wa kukusapoti.
Hakuna wa kukuonea huruma,
Pambana na Hali yako.

Mtu azione jitihada zako ndio akusapoti sio upeleke kelele zako.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Turiani, Morogoro.
 
Back
Top Bottom