WanaJF wa MMU tumoderate jukwaa letu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

WanaJF wa MMU tumoderate jukwaa letu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by EMT, Sep 16, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kwa wapenzi wa Jukwaa la MMU,

  Wiki hii tumefahamishwa na moderators kuwa kuanzia sasa threads zote ambazo zitakuwa posted hapa MMU zitakuwa under moderation kabla hazijawa approved kama lilivyo Jukwaa la Siasa. Moderators wameamua kufanya hivi kwa sababu kumekuwa na mlolongo wa threads zisizokuwa na maana yoyote au thread ambazo kimsingi hazina mantiki yoyote ndani ya Jukwaa hili.

  Wengi wamekubaliana na hii hoja japokuwa mimi nilikuwa na reservation kama itafanya kazi ipasavyo. Hata hivyo bado inaonekana baadhi ya members wanaanzisha threads ambazo naweza kusema ni feki au za kutunga na kupoteza, pamoja na mambo mengine, muda na resources za members wengine.

  Mfano kuna member mmoja alinzisha thread mwezi uliopita titled: "Mwenzi wangu anatoa ukelele. majirani wanadai tunawasumbua hawalali eti tuhame". Kwenye hiyo thread aliandika: "kwa kweli kwenye shuhuli anatoa ukelele wa hali ya juu. sasa majirani wamecharuka wanadai tuhame tunawakaraisha. nimemsihi mwenzi wangu apunguze lakini anadai hafanyi makusudi anapokaribia mshindo tu ndo huwa balaa. Nifanyeje mwenzenu na kesi tayari ipo kwa mjumbe majirani wamecharuka."

  Jana member huyo huyo akaanzisha thread nyingine titled: "Anataka kunikimbia....kisa....eti simfikishi kilimani!" Kwenye thread aliandika: "Jamani nimetumia akili, nguvu, juhudi, jitihada, maarifa na kila kitu ili mradi tu afurahi; lakini sina hakika kama nimegonga mwamba au ni kwamba ameamua tu kuniumiza. Ndio kusema hanitaki? Au anayoyasema ni kweli! Sasa nyumbani kimenuka, na hataki tena nile. Hapa ameniambia nimtafutie nauli aende zake! Kumpenda nampenda, nifanyeje? Ndiye huyu huyu member alianzisha a thead titled: "Mwenzi wangu ana mbweche kubwa.

  Kwa kweli hii ni abuse ya hili Jukwaa na imetokea baada ya Moderators kusema kuwa watakuwa wana approve kila thread kabla ya kuwekwa hapa. Najua kabisa kuwa Mods hawawezi kupitia kila thread iliyoanzishwa. Kwa mantiki hiyo, kuna umuhimu wa sisi watumiaji wa Jukwaa la MMU ku moderate threads zinazowekwa hapa kwa ku report abuse kama hizi. Pia kwa faida ya hili jukwaa ni muhimu wale wanaoanzisha threads wajimoderate wenyewe kwa kuwa honest na wanachoandika badala ya ku spam hili jukwaa na stories za uongo. Kama hawawezi kutumia utashi wao kujimoderate then sisi watumiaji tufanye hivyo kwa kuwamoderate. Vingenevyo hili jukwaa litashuka hadhi yake ambayo imejengwa na members wake kwa muda mrefu.

  Nashauri tusiwe tuu tunasoma threads na kupost bali pia tuwe tunaangalia threads ambazo zina walakini na kuziripoti kwa Mods. Always remember kifute chekundu cha REPORT ABUSE. Kiko pale kwa sababu za msingi. Naomba kutoa hoja.
   
 2. BlackBerry

  BlackBerry JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 1,844
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli inaboa sana, kuna wakati ukiingia humu unasoma tu jina la mtoa mada na kufungua sababu unajua huyu hawezi toa za ajabuajabu,halafu na wale wanaojifanya sijui jirani anaomba ushauri , sijui nani nao tuwaweke kundi gani maana kwa kweli kuna wengine huwa ni waongo wakija kujibu posts huwa wanajichanhganya...mabadiliko yanaanza na sie wenyewe hakuna atakayeyaleta ....thanks EMT kwa kutukumbusha
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  very true
  ningeweza ningekuteua EMT uwe moderator
  nilikuwa sijagundua huyu ndo huyo huyo...
   
 4. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kweli tusipoangalia hapa patakuwa kama jukwaa la siasa ambapo unasoma threads na posts za watu fulani na nyingine una disregard kwa sababu ya ku assume kuwa hawaandiki cha maana.
   
 5. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Nafikiri watumiaji wote wawe moderators kwa maana ya ku report any abuse, spam etc kwa Mods. Mtu mmoja hawezi kumoderate hili jukwaa for 24 hours. Lakini sote kwa pamoja tunaweza. Kuna kipindi tulikuwa tunajadili hoja muhimu za mapenzi, mahusino na urafiki lakini naona kama either zimepungua hivi karibuni au zimezidiwa na threads kama nilizozitaja hapo juu.
   
 6. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Labda likifanikiwa hili na mimi labda ntakuwa naingia humu kushiriki jukwaani maana mimi hilo ndo lilikuwa kikwazo kikubwa kwangu..maana kila nikiingia huwa nakuta thread za ajabu mpaka nashangaa!!
   
 7. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #7
  Sep 16, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Nine ngwitika,......yaani naunga mkono hoja kwa 100%
   
 8. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Umesema maana aise siku hizi kubnaboa hata kuingia maana topic nyingine hazina hata mshiko ila zipo tuu zinatujazia humu
   
 9. Tulizo

  Tulizo JF-Expert Member

  #9
  Sep 16, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 849
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Good points EMT..

  Lakini binafsi nadhani kudhibiti tabia za watu itachukua muda na energy ya kutosha kwani watu wanaingia humu kwa malengo mbalimbali..kuna wanaotaka kujua na kujifunza..na kuna wale wanaotaka kumaliza frustrations zao hapa; na pia kuna wale (ashakhum si matusi) wanao balehe..Taabu kweli kweli!

  Kutokana na urahisi wa ku-create username..mtu anakurupuka na username just ku-post pumba ambazo yeye binafsi anaamini yuko sahihi na pia lile group lenye frustration kama yeye litaona yupo sahihi na wewe ndio hauko sahihi.

  Siku utakapoweza kudhibiti creation za unnecessary usernames ndipo utakuwa umepiga hatua moja mbele..
   
 10. Innovator

  Innovator Content Manager Staff Member

  #10
  Sep 16, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 387
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Every thread will be under moderation before it is approved
   
 11. Innovator

  Innovator Content Manager Staff Member

  #11
  Sep 16, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 387
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Every thread will be under moderation before it is approved
   
 12. M

  Magoo JF-Expert Member

  #12
  Sep 16, 2011
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 438
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Naunga mkono hoja.....95%
   
 13. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #13
  Sep 16, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Pamoja na mawazo mazuri ya EMT mimi na beg to differ.Binafsi kuna kipindi nilikuwa sikosi kwenye blog ya Issa Michuzi.Moderatation ndo ilinitoa nduki huko na nina miaka sijaenda huko.Moderation can make you feel stupid maana unajikunja unaona umefungua thread ya maana kisha mod in his considered opinion anakutolea nje,it hurts.
  ushauri: Mods acheni threads ziingie jukwaani na kisha sisi members ndo tuchambue kipi mpunga na kipi mchele.Pumba tunapotezea mchele tunapiga ma comments na ma likes.Afterall threads kibao mmu huwa zinaishia kupata ma views kibao with few comments.Sisi ni watu wazima bana tuacheni tujiamulie cha kusoma na cha kudharau.
   
 14. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #14
  Sep 16, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  kama kuna ka_ukweli vile,....
   
 15. BlackBerry

  BlackBerry JF-Expert Member

  #15
  Sep 16, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 1,844
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Naomba wazitoe thread zooote wanibakizie za bjbj, nachekaga sana , kwanza nikiona tu kabla sijafunga mie cheko
   
 16. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #16
  Sep 16, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mkuu na mimi hapo na omba kidogo kuudiffer na wewe
  Mkuu kuna thread kweli zinaanzishwa na mtu unaiona ya maana kabisa na watu wanachangia
  Nitoe mfano wa hizo mbili alizotoa jamaa hapo juu
  Kumjua kuwa ni yule yule ametoa topic ya ajabu nayo inakuw ani ngumu at least kwa mods inakuwa rahisi zaidi kujua kuwa huyu ni yule yule alikuja na story ya aina hii na kuiondoa
  Juzi hapa kulikuwa na story ya jamaa anasema yeye ni house boy na anapendwa na shemeji sijui mama wa jamaa aliyemleta na ndo anajifunza computer ila kashaijua JF
  Unaenda kwenye jukwaa la Technology unakutana na the same guy anaulizia vitu vya computer
  sasa unajiuliza huyu kule kwenye jukwa la MMU anasema ni house boy na ndo ana miezi miwili mjini na ndo anajifunza computer huku anaulizia masuala ya ndani kabisa ya computer yenyewe
  So naunga mkono hoja ya EMT kuwa Mods wafanye kazi yao aise kuondoa huu utitiri wa topic zisizo na mshiko
   
 17. k

  kiritimba JF-Expert Member

  #17
  Sep 16, 2011
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 603
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukiwa na mtazamo tofauti haimaanishi kuwa wewe uko sahihi.
  Ni kwa nini umenispot mimi. Kwako wewe hizo ndo thread mbaya kuliko zote humu jamvini? Kumbuka kuwa hizo thread zimepitia kwa mods tena baada ya huo utaratibu wa kumoderate ulipoanzishwa.

  Pamoja na madudu mengi mnayofanya nyie mnaojiita "wamiliki wa jukwaa/wavuti" nataka nikupe mfano mmoja tu:
  Kuna siku mtu mmoja alikuja humu eti aking'ang'ana kumuulizia member mmoja hivi eti amemmaind (Nina hakika alikuwa ni mtu huyo huyo katika ID tofauti-anajiulizia mwenyewe). "Wamiliki" wa hili jukwaa mliishabikia sana hiyo thread hata pale baadhi ya watu waliposema kuwa haikuwa na tija mliwageuzia kibao na kuwashambulia hao watu. Kwa kuona kuwa ule ulikuwa upuuzi mods waliiondoa tena bila kuambiwa na mtu. Kwa upuuzi wa hali ya juu ikarudishwa, mods wakaiondoa tena. Je hali hiyo nayo tuiiteje?
  Mnanikumbsha ile hadithi ya wanyama: "All animals are equal, but some are more equal". Mnachekesha sana.
   
 18. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #18
  Sep 16, 2011
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,217
  Trophy Points: 280
  Kwani hili jukwaa lina wamiliki?mimi sikujua.mimi husoma JF kwa style ya NEW POSTS.so najikuta navist majukwaa yote
   
 19. M

  Mr Daddy Member

  #19
  Sep 16, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa naona kuna unafiki tu. Ni vigezo gani vitatumika katika kuamua mada fulani ni ya kipuuzi na isiyostahili kuwekwa hapa jamvini na fulani ni yenye akili na hivyo kustahili kuwekwa jamvini ili maalwatan wa hapa MMU waichambue, waijadili, na wapige soga zao za nani anampenda nani na nani ni mjukuu wa nani na nani ni mpwa wa nani na nani ni shemeji wa nani na wapi mjumuiko ulipokuwa mwisho wa juma na nini kilichojiri kwenye huo mjumuiko?
   
 20. k

  kiritimba JF-Expert Member

  #20
  Sep 16, 2011
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 603
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Well researched and said!
  Umemaliza yote.
  Sina cha kuongeza.
  Nadhani "magwiji" wa hili jukwaa wamekusikia
  UJUMBE MZITO HUO HATA KAMA NGUMU KUMEZA.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...