Wanajeshi wengine watatu wa Tanzania wafariki dunia huko Sudani

Wanajeshi wengine watatu wa Tanzania wafariki dunia huko Sudani

Nimefurahi sana kusikia hii mijibwa koko imeuliwa... Damu ya wanaMtwara haiwezi kupotea hivi hivi.... Yaendelee kufa tu...
Sitaki kabisa kuamini kuwa unalichukia jeshi letu kwa kiwango hiki, pia sitaki kuamini kuwa hekima imehusika katika kuandika haya uliyoandika: naichukia sana CCM, lakini si kwa kiwango cha kufurahia mabaya kwa jeshi letu.
 
R.I.P wapiganaji wetu, tatizo serikali yetu ya kipumbavu, wanaingia mikataba ambayo haina tija irimladi kutimiza wajibu.

Hapa usiingize siasa, mikataba ya kijeshi huwezi kukwepa.
 
Duuuu wabongo kwa tume tu hatujambo sasa tume vitani inaenda kufanya nini?
acha tume iende nayo wadungunyue huko ili iundwe kamati teule, nayo ipotelee huko...bingo kila kitu ulaji tuuu kama vile pesa zimekosa matumizi
 
Sitaki kabisa kuamini kuwa unalichukia jeshi letu kwa kiwango hiki, pia sitaki kuamini kuwa hekima imehusika katika kuandika haya uliyoandika: naichukia sana CCM, lakini si kwa kiwango cha kufurahia mabaya kwa jeshi letu.

Huyo MD25 bila shaka ni SUGU mkuu wala usishangae
 
acha tume iende nayo wadungunyue huko ili iundwe kamati teule, nayo ipotelee huko...bingo kila kitu ulaji tuuu kama vile pesa zimekosa matumizi

Mbona mnazidisha pumba humu JF, ina maana mnafurahia watanzania wenzenu kuuliwa?
 
mbona unajishauwa? kongo ni lazima iwe huru kawa gharama yoyote ile!

Mbona haueleweki?wanaotafuta uhuru wa DRC ni hao waasi dhidi ya utawala dharimu wa Kabila kama wanavyosema wao pia kumbuka Watanzania pia tunahitaji kuwa huru dhidi ya utawala wa kibeberu wa CCM.
 
Mbona mnazidisha pumba humu JF, ina maana mnafurahia watanzania wenzenu kuuliwa?



NOOO big no. hakuna watu ninaowaheshimu kama wale ambao wako tayari kutoa uhai wao kwa kusimama mstari wa mbele ili wengine wawe salama, i sincerely respect soldiers , kinachouma ni kwamba kuna majitu mengine yenyewe kila likitokea tukio unapenyezwa fursa ya ulaji kwa kisingizio cha tume, sababu za vifo vya wanajeshi wetu ziko wazi kwamba walishambuliwa na alshabaab na kwa kuwa role yao ni peace keeping sio mara nyingi kutumia silaha za moto 'articlce 9' ya UN peace keeping chatre (kama sijasahau) so kwa tanzania tume ni za kupiga marufuku kabisa kwa kuwa uzoefu unaonyesha huwa ni mianya tu ya ulaji...na pale serikali au taasisis zake zinapoguswa ukweli unafichwa, i hope u got me so damn cleear
 
Mbona mnazidisha pumba humu JF, ina maana mnafurahia watanzania wenzenu kuuliwa?

Hakuna anaefurahia hapa ni watu wanaonyesha hisia zao kwa serikali yetu kuwatoa sadaka wanajeshi wetu ikumbukwe tumeishapoteza askari wetu wengi kule Msumbiji,Angola na maeneo mengine lakini serikali haijajifunza tu vita vya Uganda tulipigana pekeyetu je tungepigwa hawa wanaotutumia leo wangekuja kutusaidia?pia tukumbuke Idd Amin alitoroka kupitia hukohuko Sudani ambako wanajeshi wetu wameuliwa.
 
Nashauri serikali iendelee kuwatoa wanajeshi wetu wakapate mazoezi huko kwenye viwanja vya mapambano.

Mleta mada naona ameamua kupotosha kwa makusudi.
 
Tuko pamoja na askari wetu popote walipo; tunawapa pole sana wafiwa kupoteza askari vitani sio mwisho wa Tanzania kujitolea kwenye majeshi ya kimataifa; askari endeleeni kutekelezqa majukumu yenu hadi kieleweke!
 
R.I.P wapiganaji wetu, tatizo serikali yetu ya kipumbavu, wanaingia mikataba ambayo haina tija irimladi kutimiza wajibu.
'Irimladi' mbona hiyo propaganga mkuu. Kusaidia ulinzi kama kule congo wasishambuliwe na wapumbavu sio upumbavu.
 
2.png


WINGU zito limetanda kwa askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), katika nchi za Sudani Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).


Wakati Watanzania wakiendelea kuomboleza vifo vya wanajeshi saba wa jeshi hilo waliopoteza maisha katika Jimbo la Darfur, Sudani kwa kushambuliwa na waasi, nchini DRC yamezuka mapigano makali baina ya waasi na majeshi ya Serikali.

Mapigano hayo yameripotiwa kuibuka kati ya Wanajeshi wa Serikali na waasi karibu na mji wa Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Msemaji wa wapiganaji wa waasi wa M23, ameliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kuwa ndege za kivita za Serikali zimefanya mashambulio ya anga katika maeneo yao usiku wa kuamkia jana.

Umoja wa mataifa kwa upande wake umesema uko tayari kutumia nguvu, kuwalinda raia ikiwa wapiganaji hao wa M23 wataingia katika mji wa Goma.

Raia wakimbia mapigano

Wakati huo huo, mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu, yamesema kuwa zaidi ya wakimbizi elfu sabini raia wa Congo wamekimbilia nchi jirani ya Uganda, kukwepa mapigano hayo.

Wapiganaji wa waasi wa Uganda nchini Congo, Allied Democratic Forces walishambulia mji wa Kamango na kusababisha mapigano makali kati yao na jeshi la serikali.


JWTZ: Askari wetu DRC wapo salama
Kwa upande wake, Msemaji wa Jeshi la Tanzania (JWTZ), Kanali Mgawe, alipoulizwa kuhusu mapigano hayo aliwataka wananchi kutokuwa na wasi wasi kuhusu usalama wa wanajeshi wa Tanzania.

“Wanajeshi wa Tanzania wapo salama hakijatokea kitu chochote tofauti na kama kuna tatizo lolote tutatoa taarifa, wanajeshi wetu nchini Kongo DRC wapo salama,” alisema.


Wanajeshi wengine wadaiwa kufa Darfur
WAKATI Watanzania wakiendelea kuomboleza vifo vya wanajeshi saba wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), waliokufa katika Jimbo la Darfur nchini Sudani, askari wengine watatu wa jeshi hilo wamedaiwa kupoteza maisha.

Idadi hiyo imedaiwa kuongezeka, baada ya wanajeshi hao watatu ambao ni kati ya 14 waliokuwa wamejeruhiwa vibaya, nao kupoteza maisha katika shambulizi la kushtukiza.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya JWTZ, kimesema kuwa askari hao wamefariki dunia baada ya jitihada za madaktari kuokoa maisha yao kushindikana.

Askari hao walifariki baada ya kushambuliwa na kikundi cha waasi wa Sudani, walipokuwa katika msafara wa kusindikiza waangalizi wa amani kutoka Khor Abeche kwenda Nyara, katika Jimbo la Darfur.

MTANZANIA ilipomtafuta msemaji wa jeshi hilo, Kanali Kapambala Mgawe kuzungumzia taarifa hizo, alisema hakuna taarifa zozote zinazoonesha kuwapo na ongezeko la idadi ya vifo vya Darfur, Sudani.

Kuhusu usafirishwaji wa miili ya askari hao kuja nchini, Kanali Mgawe alisema suala hilo la usafirishwaji wa miili ya askari hao, linaratibiwa na Umoja wa Mataifa (UN), ingawa JWTZ inafuatilia kwa karibu.

“Ninapenda kukuambia kuwa hadi sasa hakuna mwanajeshi aliyeongezeka, ila hizo ni taarifa ambazo si sahihi na zimekuwa zikienezwa katika mitandao ya kijamii. Sisi kama jeshi hatuna taarifa kama hizo,” alisema Kanali Mgawe.

Alipoulizwa kuhusu kutajwa kwa majina ya marehemu waliokufa katika tukio hilo la kushtukiza, Kanali Mgawe alisema jeshi haliwezi kutaja majina hayo kwa sasa, ila kinachofanyika ni kuwasiliana na ndugu wa marehemu hao.

“Safari hii asilimia kubwa ya askari wetu waliokwenda Sudan, wametoka katika mikoa ya mipakani, kwa hiyo tunachokifanya sasa tumeshawasiliana na makamanda wa kambi zote za jeshi ambazo wametoka marehemu hawa, ili waweze kuwasiliana na ndugu wa marehemu.

“Hivi ndugu utajisikiaje unasoma gazeti au unaangalia TV na kusikiliza redio halafu ukasikia kuwa ndugu yako amefariki utajisikiaje, ni lazima katika hili tuweze kufuata taratibu nzuri zinazokubalika kwa kuwasiliana nao moja kwa moja.

“Ninachotaka kuwahakikishia Watanzania kuwa JWTZ lipo imara na kama kuna taarifa yoyote tutaitoa mbele ya umma,” alisema.

Hata hivyo Kanali Mgawe alisema jeshi hilo limetuma ujumbe maalumu kwenda Darfur kuchunguza kiini cha tukio hilo, ingawa hakuweza kueleza kikosi hicho kinaundwa na wataalamu wa fani gani.


Source: Mtanzania
​
Tz imekosa mwelekeo...!!!???
 
Sitaki kabisa kuamini kuwa unalichukia jeshi letu kwa kiwango hiki, pia sitaki kuamini kuwa hekima imehusika katika kuandika haya uliyoandika: naichukia sana CCM, lakini si kwa kiwango cha kufurahia mabaya kwa jeshi letu.

Kwa hiyo yale mazuri ya kupiga na kuwabaka wanaMtwara ndio unayoyafurahia?...
 
Tume hadi vitani?? Kweli Tanzania inashida ya kufikiri!

Tunawaombea wapiganaji wetu Mungu apumzishe roho zao kwa amani peponi amen. Binafsi nahunga mkono kuhundwa kwa tume ya uchunguzi - tusiaze kulahumu Al Bashir, Janjaweed au Al Shabaab mimi sioni kama vikundi hivyo vilikuwa na a burning desire ya kuwapa fundisho wanajeshi walio kuwa wanalinda Amani kutoka Tanzania - narudia kutoka TANZANIA!! Swali ni: Why pick on Tanzanians wakati walinda amani huko Darfur wanatoka mataifa mbali mbali!

Tume ianzie kwa kupeleleza kikundi kilicho pora/hiba magari ya UN yaliyo kuwa yanatumiwa na Majeshi ya Tanzania a day or two kabla ya tukio hili la kinyama na baadae magari hayo yakatumika kama chambo cha kuwa-ambush wapiganaji WETU!! Swali ni je - wahusika wa tukio ili ovu ni wenyeji kweli wa Sudan au ni a well trained commandoes kutoka a foreign country ambao walipenyezwa nchini Sudan kwa lengo la kuwadhulu wanajeshi WETU ili Taifa letu likate tamaa ya kupeleka wanajeshi wetu nchini DRC, nilisha sema mbinu za kuvamia wanajeshi wetu halina tofauti na kuvamiwa kwa wanajeshi wa South Africa huko Central Africa, kumbuka Nchi zetu hizi mbili ndizo zitapeleka majeshi yao DRC.

Narudia kuwakumbusheni kwamba operation ile haiwezi kuwa imetekelezwa na a rag tag army; namshukuru Mh.Kikwete kwa kuomba ushirikiano wa Al Bashir katika upelelezi wake, Bashir akiahamua kutuhangusha nina hakika Taifa letu lina mbinu nyingi za kuweza kupata taarifa za kuaminika; swala hili tuwashilikishe Africa Kusini vile vile.
 
tufikie mahala tuwe na mshikamano na utaifa mbele itikadi za kisiasa tuziweke pembeni!hivi kazi za jeshi nini?hivi nyie mnataka wanajeshi wetu wawe wamekaa tu nchini bila kazi yoyote?mimi nafikiri kwenda kulinda aman kwenye nchi zingine ni njia mojawapo ya kuliimarisha jeshi letu!

huko ndiyo kuimarisha???? Acheni hizo tumeumia sana ndugu zetu kufa ugaibuni ni bora wangekufa wakati wakifanya mazoezi na wenzao humu ndani. Tunajua pesa za mazoezi mnazichakachua hawaendi mazoezi.mbona wakati wa nkapa walifanya mazoezi misitu ya korogwe na kilindi tanga na walikuwa wanarusha moja kwa moja leo mnawaminyia.acha wafe mjifunze
 
Wengi hawakumwelewa Paul Kagame aliposema ''I will hit him''

Huyu Jamaa ni Mtaalamu wa Medani za Kivita.Ni Generali wa Msituni Kivitendo si Mezani.Anaelewa Mikakati ya Ushindi.Amefanikiwa kuwashawishi Marais wa Afrika Mashariki kutususa.Anatenda anachodhamiria na ni Mjanja sana Kimbinu.Si ajabu akafadhili Waasi kushambulia Majeshi ya Tanzania popote pale Duniani.
 
Huyu Jamaa ni Mtaalamu wa Medani za Kivita.Ni Generali wa Msituni Kivitendo si Mezani.Anaelewa Mikakati ya Ushindi.Amefanikiwa kuwashawishi Marais wa Afrika Mashariki kutususa.Anatenda anachodhamiria na ni Mjanja sana Kimbinu.Si ajabu akafadhili Waasi kushambulia Majeshi ya Tanzania popote pale Duniani.
Ndo kaishaanza hivi kutupeleka kuzimu mmoja mmoja..! He has full support from Kenya, Uganda, Malawi na Burundi..! Chezea pua ndefu weye..! Kwa upande mwingine at least he will keep JK busy na ataisahau Chadema japo kidogo..!
 
Ndo kaishaanza hivi kutupeleka kuzimu mmoja mmoja..! He has full support from Kenya, Uganda, Malawi na Burundi..! Chezea pua ndefu weye..! Kwa upande mwingine at least he will keep JK busy na ataisahau Chadema japo kidogo..!

Wenzao wako busy kutafuta maslahi ya nchi wao kiguu na njia kukabili chadema, kumbe hawajui kuwa adui mkubwa yuko nje ya mipaka.I will hit him at the rght place in Darful
 
Mbona haueleweki?wanaotafuta uhuru wa DRC ni hao waasi dhidi ya utawala dharimu wa Kabila kama wanavyosema wao pia kumbuka Watanzania pia tunahitaji kuwa huru dhidi ya utawala wa kibeberu wa CCM.

slim boy kazini.
 
Back
Top Bottom