Wanajeshi watoa kichapo mandela road

Wanajeshi watoa kichapo mandela road

Nyanya mbichi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2011
Posts
3,716
Reaction score
2,218
Leo kuna foleni kali hasa kwa magari yatokayo ubungo kwenda buguruni.

Tulivyo vuka daraja la matumbi tukasikia kin'gora kumbe ni Magari ya wana jeshi yamebeba zana za kivita wanatumia barara itokayo buguruni kwenda ubungo wao wamefanya kinyume .

Sasa kuna gari zikawa zinakuja MP wakateremka ili magari yakae kando heee kumbe dereva wa gari ndogo alikua amepaki gari pembeni si mjeshi mmoja akaanza kumtandika hadi basi. Tukio nimeliona vizuri sema picha nilishindwa kuchukua.
 
Ungepiga hata picha eneo la tukio habari ikamilike mkuu!!
 
Si sawa kupiga raia,wakumbuke raia ndio wanaowalipa wao mishahara kupitia kodi wanazokatwa,pia wao waliamua kuforce kupita njia ambayo siyo yao.Walipaswa wawe wapole na si kujichukulia sheria mkononi,na kwanin wasisafirishe zana zao mida ya usiku wakat hakuna purukushani nyingi.Kama walinzi wetu wanatupiga adui watafanyanyaje? Pia wakumbuke mafunzo yao ni ya hali ya juu na hawakufunzwa kuwapiga raia.NADHANI WAKATI UMEFIKA KWA BAADHI YA WANAJESH KUACHA KUHARIBU SIFA NZURI YA JESH LETU.
 
Kumbe maskini alikua amepaki pembeni ya barabara kwanini sasa apigwe ?
 
Leo kuna foleni kali hasa kwa magari yatokayo ubungo kwenda buguruni.

Tulivyo vuka daraja la matumbi tukasikia kin'gora kumbe ni Magari ya wana jeshi yamebeba zana za kivita wanatumia barara itokayo buguruni kwenda ubungo wao wamefanya kinyume .

Sasa kuna gari zikawa zinakuja MP wakateremka ili magari yakae kando heee kumbe dereva wa gari ndogo alikua amepaki gari pembeni si mjeshi mmoja akaanza kumtandika hadi basi. Tukio nimeliona vizuri sema picha nilishindwa kuchukua.

No discipline means doing anything arbitrarily!
 
Hawa ndio wale makuruta ambao ni plain kabisa ni rank au ana mbavu moja beganimyaani ni tabu tupu,,,hawa jamaa siku wakichukua nchi sijui itakuaje?
 
Ni uonevu huu, hawa wanatakiwa wakutana na trafic waliopinda kama yule wa mwaka 2011....

Leo nilitembelea maeneo ya Tabata kwa mwanangu, wakati narudi kwangu kule Kigamboni , ghafla kufilka pale wanapoita Tabata reli Trafiki Police alisimamisha magari ya upande mmoja ilikuokoa jahazi la magari yanayotoka Buguruni, sasa Gari la mwanajeshi likawa limekumbwa na kizaazaa cha kusimamishwa, mwanajeshi yule ana cheo cha staff sajenti alimvaa Police kwa kejeli na matusi. Trafic akamjibu tuheshimiane lakini mjeshi akaendelea kumtusi askari yule mwenye cheo cha Copro, kama mzaa mwanajeshi akamkwida Uniform , hahahahaaaah Police hakukubali dharau ile, akampiga Mtama mwanajeshi yule, alipoinuka akapigwa Gumi la kuushoto, baada kama ya Dakika 5, MWANAJESHI HOI, ashukuru Mungu jamaa wenye mabucha na askari Police wengine walikuja kuingilia ugomvi ule.
Hakuna dereva wala konda wa daladala alietamani Ugomvi ule uishe, ila jambo lililosisimua na aina ya Ngumi za yuleTrafic dhidi ya Mwanajeshi yule
.
 
Mchezo ndio kwanza unaanza, Raia siku hizi wanachonga sana, ngoja amri ya hatari itangazwe kutoka ndani saa mbili asubuhi kulala saa kumi jioni, tuone hizo wowowo zenu mtatingishia wapi?
 
Nampongeza kikwete pamoja na uanajesh wake wote watu wanamsema mengine ni ya kuuzi lakini mwanajeshi huyu ameonyesha ukomavu wake wa kujua namna ya kuwachukulia raia na mara zote anasmile.Kwanin nyie wanajesh mnaopga raia msiige tabia hii ya amir wenu mkuu?
 
Si sawa kupiga raia,wakumbuke raia ndio wanaowalipa wao mishahara kupitia kodi wanazokatwa,pia wao waliamua kuforce kupita njia ambayo siyo yao.Walipaswa wawe wapole na si kujichukulia sheria mkononi,na kwanin wasisafirishe zana zao mida ya usiku wakat hakuna purukushani nyingi.Kama walinzi wetu wanatupiga adui watafanyanyaje? Pia wakumbuke mafunzo yao ni ya hali ya juu na hawakufunzwa kuwapiga raia.NADHANI WAKATI UMEFIKA KWA BAADHI YA WANAJESH KUACHA KUHARIBU SIFA NZURI YA JESH LETU.

mkuu niliwaambia abiria wenzangu kuwa hivi kwa nini wasingesafirisha usiku kukiwa tulivu??.
 
Ungepiga hata picha eneo la tukio habari ikamilike mkuu!!

mkuu@chakii nilikua viti vya nyuma vya UDa halafu kile kioo kina ukungu fulani hakiko clear so nisingeweza kupata picha mzuri
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom