Wanajeshi wanane wa kulinda amani wa UN wathibitishwa kupoteza maisha DRC

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,877
Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limesema waasi wameiangusha helikopta ya Umoja wa Mataifa mashariki mwa nchi hiyo.

Takriban watu wanane walikuwa kwenye ndege hiyo iliyodunguliwa wilayani Rutshuru katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Sita kati ya waliofariki walikuwa wanajeshi kutoka Pakistan. Jeshi la Congo limesema helikopta hiyo ilidunguliwa na wasi.

Ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa umesema helikopta yake moja ilitoweka katika eneo la Chanzu, ambalo lilishambuliwa na wapiganaji wa kundi la M23 Jumapili usiku.

Shirika la Msalaba Mwekundu linasema takriban watu elfu sita wamekimbilia nchi jirani ya Uganda ambapo wanapelekwa kwenye kambi ya wakimbizi.

Idara ya Operesheni za Amani ya Umoja wa Mataifa ilithibitisha kupoteza kwa askari wanane wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, kufuatia ajali ya helikopta yao Jumanne hii, katika Mkoa wa Kivu Kaskazini.

Miongoni mwa waliofariki waliokuwa ndani ya ndege hiyo, wafanyakazi sita kutoka Pakistani na wafanyakazi wawili wa kijeshi, mtawalia kutoka Urusi na Serbia.

Mapema leo, Vikosi vya Wanajeshi vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vilishutumu kundi la waasi kwa kuiangusha helikopta ya Umoja wa Mataifa.

Jenerali Sylvain Ekenge, Msemaji wa serikali ya Kivu Kaskazini aliviambia vyombo vya habari kwamba waasi wa M23 waliiangusha helikopta ya MONUSCO ilipokuwa ikiruka juu ya maeneo yanayodhibitiwa na M23, kwa misheni isiyo na hatia iliyolenga kuwasaidia waathiriwa wa mashambulio ya hivi majuzi.

Katika taarifa yake, leo, msemaji wa M23, Meja Willy Ngoma amelilaumu jeshi la DRC kwa kufanya mashambulizi dhidi ya nafasi zao, akisema walijibu ili kujilinda. Mapigano yalizuka kati ya jeshi la kawaida la DRC na M23 tangu mapema Jumatatu.

BBC Swahili
 
Back
Top Bottom