Wanajeshi wamenipiga mbele ya mke wangu

Wanajeshi wamenipiga mbele ya mke wangu

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,401
Reaction score
1,618
Ilikuwa juzi kwenye heka heka za kusheherekea pasaka mimi na demu wangu.

Maeneo ya barabara ya chuo kikuu (UDSM) inayoelekea changanyikeni nikawa nimepaki gari pembeni kidogo na barabara siku ipaki pembeni kabisa kiukweli kwa namna fulani nikamuacha demu wangu mi nikaingia sehem (hillpark) kununua vocha pamoja kumtumia mtu hela, nilipo maliza nikawa natoka nje nikakuta lile gari kubwa kabisa la jeshi limesimama nyuma ya gari yangu halafu kuna wanajeshi wawili wapo kwenye gari yangu wanaongea na wife wakimuuliza mwenye gari yupo wapi namimi nikawa natokea akasema huyo hapo... mamamamaaaaaaaa............... kabla hawajaniuliza kitu walinipokea kwa makofi na vibao, walinipiga sana kwa kweli, sikuweza kupigana nao hata kidogo kwasababu kuna wengine walikuwa wametulia tu kwenye gari lao. Mke wangu alishuka kuamulia waniache hawakumpiga lakn walimsukuma akadondokea mkono wa kushoka umeteguka.

Namshukuru sana Mungu, akashuka mwanajeshi mwingine sijui ni boss wao akawaambia waniache ndipo wakaondoka.

Mke wangu amewekewa muhogo mkononi huku mimi naugulia tu maumivu, nimeaibika sana mbele ya mke wangu japo naona aibu lakni najifanya uso mkavu kama ndimu.
 
Pole mkuu. Wrong parking ni makosa siku zote.
 
Sijui ni kwanini hawajamaa mara nyingi wameonekana kuwa juu ya sheria,,
Lakini mara nyingine huwa ni wa muhimu sana mfano,wewe una-park gari barabarani na wingi wa magari hapa mjini ni muhimu na lazima sana kukutana na mambo kama hayo.
Pole sana lakini.
 
Bosi ingawa ni maumivu lakini nimecheka. Samahani sana kwa hili! Kwa nini mnapaki gari barabarani? Pale hilpark kuna parking ya kutosha, kwa nini usingeiingiza ndani kule?
Pole usirudie tena!
 
Una utani na wajeda wewe. yeye mmoja, wajeda kadhaa awarushie ngumi? Licha ya hivyo kasema hakujiandaa, alishtukizwa.

Itabidi kujifunza karate maana hao wanasifa sana halafu hawana busara hata chembe
 
Sijui ni kwanini hawajamaa mara nyingi wameonekana kuwa juu ya sheria,,
Lakini mara nyingine huwa ni wa muhimu sana mfano,wewe una-park gari barabarani na wingi wa magari hapa mjini ni muhimu na lazima sana kukutana na mambo kama hayo.
Pole sana lakini.

ndio tatzo letu watz tunakuwa wa kwanza kuvunja sheria ila tukiadhibiwa hatuishi kulalama et tunaonewa, tunanyanyaswa....
 
parking ya bongo noma sana mtu anaona vibarabara vyetu vilivyo na anapaki tu barabarani .nani akusubiri sasa yaani ww ufanye makosa halafu useme umeonewa.
 
Mkuu POLE SANA!!! Wifw akikutania mwambie walikuwa wengi....
 
Hapo kama kauli ya mh pinda ilikuwa inafanyiwa kazi teh teh teh yaaani nimecheka sanaa pole lakini
 
Ilikuwa juzi kwenye heka heka za kusheherekea pasaka mimi na demu wangu.

Maeneo ya barabara ya chuo kikuu (UDSM) inayoelekea changanyikeni nikawa nimepaki gari pembeni kidogo na barabara siku ipaki pembeni kabisa kiukweli kwa namna fulani nikamuacha demu wangu mi nikaingia sehem (hillpark) kununua vocha pamoja kumtumia mtu hela, nilipo maliza nikawa natoka nje nikakuta lile gari kubwa kabisa la jeshi limesimama nyuma ya gari yangu halafu kuna wanajeshi wawili wapo kwenye gari yangu wanaongea na wife wakimuuliza mwenye gari yupo wapi namimi nikawa natokea akasema huyo hapo... mamamamaaaaaaaa............... kabla hawajaniuliza kitu walinipokea kwa makofi na vibao, walinipiga sana kwa kweli, sikuweza kupigana nao hata kidogo kwasababu kuna wengine walikuwa wametulia tu kwenye gari lao. Mke wangu alishuka kuamulia waniache hawakumpiga lakn walimsukuma akadondokea mkono wa kushoka umeteguka.

Namshukuru sana Mungu, akashuka mwanajeshi mwingine sijui ni boss wao akawaambia waniache ndipo wakaondoka.

Mke wangu amewekewa muhogo mkononi huku mimi naugulia tu maumivu, nimeaibika sana mbele ya mke wangu japo naona aibu lakni najifanya uso mkavu kama ndimu.

Pole sana ndugu. Hakuna kitu kibaya kama kudhalilishwa mbele ya mke na/au watoto. Ulifanya vyema kutokupigana kwani ungeishia kuumizwa tu na hao interahamwe. Mke wako anaelewa kuwa wewe siyo Mungu, wala Malaika na aliona mazingira yalivyokuwa. Ameumia akiwa kwenye harakati za kukusaidia usipate kipigo na ninaamini "intervention" yake ilisaidia bosi wa hao askari wasiokuwa na nidhamu aingilie kati. Mshukuru kwa ujasiri na upendo wake kwako na umuuguze apone haraka.
 
Back
Top Bottom