Wanajamvi nimeng'atwa na nyoka

Wanajamvi nimeng'atwa na nyoka

Pole sana,nakumbuka mwezi uliopita nilitoka safari,wakati nataka sasa kulala nazima taa,nyoka chumbani,aliingiaje sijui,baada ya muda simuoni,nikalala nikiassume yupo kabati la nguo,kesho yake mafuta ya taa yalimtoa,kumbe alipanda kwenye nguo kabatini,tukamuua,kwakweli mpaka leo sina hamu,na naogopa kila nikiingia ndani.
 
Nakumbuka za mani kulikuwa na Yale mawe meusi unachanja then unabandika linanasa mpaka sumu ikiisha linadondoka, asubuhi unalidumbukiza kwenye maziwa fresh kutoa sumu then linakuwa ready kwa Matumizi mengine. Hebu tuelezane first aid jamani seriously wengi tumehamia makazi mapya. Mkojo ni tiba? Sometimes distance to the hospital plus traffic can be very challenging
 
Nipo hospitali nimehudumiwa na kupatiwa kitanda nimetundikiwa maji baada ya sindano mbili. Nilikua nmevaa sandals usiku huu natoka kupaki gari jirani tu na napokaa. Naendelea vyema
Pole sana mkuu,hata hivyo wataalam wanasema nyoka wengi huwa hawana sumu.
unapogongwa na nyoka cha kwanza kuangalia ni kama
kuna alama mbili au mashimo mawili yanayotoa damu,yaani nyoka wenye sumu
wana meno mawili ambayo hutumika kuinject sumu.
kama hakuna alama,huyo ni nyoka wa kawaida .lakini inashauriwa kwenda hospitali kuonana na daktari.
Na kama utakuta hayo mashimo mawili yanatoa damu
usiogope na kusababisha damu kwenda mbio kitu ambacho husababisha sumu kutembea haraka mwilini
na wala usifunge juu ya eneo lililoumia kwani hii husababisha,sehemu iliyoumia kukosa damu,na endapo itachukua muda mrefu
inaweza kukusababishia kupoteza kiungo hicho
Cha kufanya ukiishagundua aliyekugonga ni mwenye sumu,fanya taratibu za kwenda hospitali haraka
na ikiwezekana usitembee kwa mguu tumia usafiri.
 
Nakumbuka za mani
kulikuwa na Yale mawe meusi unachanja then unabandika linanasa mpaka
sumu ikiisha linadondoka, asubuhi unalidumbukiza kwenye maziwa fresh
kutoa sumu then linakuwa ready kwa Matumizi mengine. Hebu tuelezane
first aid jamani seriously wengi tumehamia makazi mapya. Mkojo ni tiba?
Sometimes distance to the hospital plus traffic can be very
challenging

well said
 
Kuna jamaa yetu mmoja aliwahi kugongwa na nyoka mitaa ya ubungo, kila zahanati tuliyompeleka walikuwa wanashangaa kwa nini kagongwa na nyoka mjini. Na tiba walikuwa hawana zaidi ya kutoa tu huduma ya kwanza.
 
Pole sn mkuu.

Na sasa waendeleaje?
Naendelea vyema na sasa naweza kukanyaga chini ila mguu bado umevimba... I hope j3 ntakua vizuri kuweza kwenda kazini kulijenga taifa as usual
 
Pole sana mkuu,hata hivyo wataalam wanasema nyoka wengi huwa hawana sumu.
unapogongwa na nyoka cha kwanza kuangalia ni kama
kuna alama mbili au mashimo mawili yanayotoa damu
,yaani nyoka wenye sumu
wana meno mawili ambayo hutumika kuinject sumu.
kama hakuna alama,huyo ni nyoka wa kawaida .lakini inashauriwa kwenda hospitali kuonana na daktari.
Na kama utakuta hayo mashimo mawili yanatoa damu
usiogope na kusababisha damu kwenda mbio kitu ambacho husababisha sumu kutembea haraka mwilini
na wala usifunge juu ya eneo lililoumia kwani hii husababisha,sehemu iliyoumia kukosa damu,na endapo itachukua muda mrefu

inaweza kukusababishia kupoteza kiungo hicho
Cha kufanya ukiishagundua aliyekugonga ni mwenye sumu,fanya taratibu za kwenda hospitali haraka
na ikiwezekana usitembee kwa mguu tumia usafiri.
Yaani mkuu ulichoandika ndicho kilichotokea maana nilipohisi kung'atwa nikacheki kwa kutumia simu ndo nikaona vidam kama vimeruka matundu mawili...na hapo ndipo nikaanza kukimbia tena kurudi kuchkua gari ili niwahi hospital,ajabu nimefika kwenye gari ndo nikaanza kuskia maumivu taratibu na ganzi...nikahisi sitoweza kufika hospital alone nikarudi hm kwanza nipate firts aid, ndio nikafungwa mguu juu kidogo...baada ya hapo mguu wote ulikufa ganzi na maumivu niliyokua naskia hapo sijawahiyapata maana hata gari niliona kama hawakimbizi...na hospital pia walinambia kufunga kamba pia ni hatari nikabaki nashangaa maana mimi siku zote nilikua najua ndio njia sahihi ya kuzuia sumu kusambaa
 
Pole sana mkuu,naamini sasa utakuwa unaendelea vizuri.
Viumbe hawa yaani nyoka wapo,na inasemekana mara nyingi hugonga pale tunapowaumiza kama vile kumkanyaga
maana wanatambaa chini,lakini kama hawakuumizwa mara nyingi hawaumi kwani wana kipochi kinaitwa "jacob son'' huwasaidia kujua kwa mbali adui au kisababishi cha madhara kwao kwa njia ya ulimi wao ambao mara nyingi wanautoa nje na kuingiza ndani/puani tendo hilo hupeleka signal kwenye kipochi hicho ambacho hutafsiri,kama kilichopo mbele yake ni adui au ni kitu cha kawaida.
Inashauriwa unapokutana na nyoka mkubwa ambaye huna uwezo wa kummdu,usiwaze kumdhuru.cha kufanya tulia
wala usiangaike kana kwamba unatafuta silaha ya kumdhuru,ndani ya muda mfupi utaona anajiondokea,lakini ukionekana unataka kumdhuru ndo hapo anaanza kushindana nawe.
 
Kuna jamaa yetu mmoja aliwahi kugongwa na nyoka mitaa ya ubungo, kila zahanati tuliyompeleka walikuwa wanashangaa kwa nini kagongwa na nyoka mjini. Na tiba walikuwa hawana zaidi ya kutoa tu huduma ya kwanza.
Mkuu mlifanya vema kumpeleka hospitali,madaktari wanajua kuangalia kama nyoka aliyegonga ana sumu au la,
mara nyingi wakigundua hana sumu,wanakufanyia kukutuliza kisaikolojia
maana hata wakikupa dawa ya sumu ya nyoka ni kukuumiza bure.
Ni muhimu kwenda hospitali ili madaktari wamuone mgonjwa na kufanya maamuzi.
 
nakumbuka mi niliumwa mguuni, wakanifunga kamba damu isitembee then nikaenda kuwekewa jiwe. baada ya muda nikpelekwa hosp
 
Hata kama umeumwa na Cobra, kunywa mkojo wako ndio dawa ya awali, ila utatapika kinoma noma, kama ni cobra au swila. Kuna futher step.
 
Nakumbuka za mani kulikuwa na Yale mawe meusi unachanja then unabandika linanasa mpaka sumu ikiisha linadondoka, asubuhi unalidumbukiza kwenye maziwa fresh kutoa sumu then linakuwa ready kwa Matumizi mengine. Hebu tuelezane first aid jamani seriously wengi tumehamia makazi mapya. Mkojo ni tiba? Sometimes distance to the hospital plus traffic can be very challenging
Mkuu hilo la mkojo sijawahi kulisikia kwenye huduma ya kwanza kwa mtu aliyengatwa na nyoka.
katika ulimwengu wa sasa uliojaa magonjwa,unaweza kusababisha tatizo kubwa wakati unajaribu kutatua tatizo dogo.
Asilimia kubwa ya nyoka hawana sumu,ila nao wanagonga.wenye sumu wakigonga huacha alama za meno mawili yaliyotoboa,ie utakuta panatoa damu.
na hao wenye sumu,wako makundi matatu(sumu inayoingia kwenye nyama,sumu inayoingia au kusafiri kwenye damu na sumu inayosafiri kwenye nerve system(akina na black/green mamba))
wale wa kundi la kwanza sumu yao huwa inatend kuozesha sehemu iliyoathiriwa(nyama/misuri);kundi la pili ndo hao sumu inatembea kwenye damu na kundi la tatu hawa sumu yao inaua haraka sana yaani ndani ya madakika lakini hawa mara nyingi wapo maporini siyo mjini.
Huduma ya kwanza ni kumfanya mgonjwa asipanic(assurance) hii inazuia kama ni sumu inayotembea kwenye damu,basi moyo wa mtu aliyepanic huenda mbio na hivyo damu hukimbia haraka na hivyo kusambaza damu/sumu haraka. Usifunge kiungo kilichoathiriwa na endapo utafunga,basi uwe unafungua kila baada ya dakika walau 30. ili kufanya damu ifike na kupeleka oksijeni kwenye kiungo hicho.kama kiungo kilichogongwa ni mkono uninginize ili damu inayorudi kwenye moyo iwe na resistance ya kupanda badala ya kuuinua juu.kama ni mguu kaa endelea kuuninginiza.
Lakini hizi ni huduma ya kwanza tu,lazima utaratibu wa haraka wa kumpeleka mgonjwa hospitalini unafanywa au fanya hayo huku mgonjwa akiwa kwenye chombo cha usafiri kumpeleka hospitalini.Jitahidi kupata usafiri badala ya kwenda hospitali kwa mguu au mgonjwa abebwe.Kama ulivyotaja kijiwe unaweza kitumia lakini nacho kama huduma ya kwanza huku unampeleka mgonjwa hospitalini.
haya ndio ninayoyajua tuendelee kuchangia.
 
Nipo hospitali nimehudumiwa na kupatiwa kitanda nimetundikiwa maji baada ya sindano mbili. Nilikua nmevaa sandals usiku huu natoka kupaki gari jirani tu na napokaa. Naendelea vyema

Pole kiongozi, nyoka wanaua
 
Naona watu wengi wanazungumzia kijiwe ambacho husaidia kunyonya sumu mara unapo umwa na nyoka.
Actually kile sio kijiwe bali ni mfupa wa mnyama.
 
Mungu akujalie upone harak, urudi katika pilikapilika za mtu mweusi.
 
Back
Top Bottom