Wanaijeria kuitwa Wapopo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaijeria kuitwa Wapopo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Balantanda, Feb 4, 2009.

 1. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #1
  Feb 4, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Heshi mbele wakuu...Mara nyingi nimekuwa nikisikia hawa jamaa wa Nigeria(hasa waliopo nje ya bara la Afrika) wakiitwa wapopo..Hivi hili neno lina maanisha nini???,ni nini asili yake???,naomba mnijuze hilo wakuu maana linanichanganya...Be blessed
   
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  Feb 4, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Sababu ya TAMAA, UTAPELI na Undumila kuwili wao, ndio maana wamefananishwa na Popo.

  Kama wewe ni msomaji wa hekaya na ngano utakumbuka simulizi moja iliyokuwa inahusu ndege na wanyama. Wanyama wakataka msaada kwa Popo, Popo akawatolea nje kwa kudai kuwa yeye ni ndege kwa sababu ana mbawa na ana ruka hewani kama wafanyavyo ndege wengi.

  Ndege nao waliposikia hiyo habari wakamuomba ajiunge nao kwa kuwa na yeye ni mmoja wao kwani ana ruka kama wao, Popo kama kawaida yake akawatolea nje kwa kuwaambia kuwa yeye ni mnyama na si ndege kwa sababu ana zaa. Akawauliza "...Mmeona wapi ndege akazaa...!?

  Lakini ajabu ilipofika kipindi cha kugawana mapato akataka kupata huku na huku tena bila haya. Upande wa wanyama akajitia yeye ni mnyama, na upande wa ndege akajifanya yeye ndege.

  Jamii ya wanyama na ndege wakamshtukia wakamtoa mbio na kumtangazia hukumu ya kifo popote pale atakapo onekana. Na ndio maana mpaka leo anatoka wakati wa usiku tu, kwa kuogopa kushushiwa kipigo kati ya wanyama na ndege.

  Wa'nigeria nao wana sifa kama hizo zinazoendana na simulizi niliyo kutolea hapo juu.

  Pia bila kusahau wanaitwa 110 (One-Ten) au 1/10 (One over Ten). Na hii ni jinsi walivyo wengi Ulaya na Marekani. Yaani kila alipo Mwafrika mmoja wao wapo 10. (!?)

  Habari ndio hiyo mkuu...!


  NB:
  Tusubiri taarifa na maelezo
  toka kwa wachangiaji wengine.
   
 3. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Nashukuru sana ndugu yangu X-P kwa mwanga huu ulionipa angalau nimeanza kupata ufahamu juu ya asili ya jina hili..Asante sana ndugu
   
 4. Geeque

  Geeque JF-Expert Member

  #4
  Feb 4, 2009
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 848
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  hahahahaha hii stori imenifurahisha sana hahahaha.
   
 5. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #5
  Feb 4, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Any time Brother kaka...! you are welcome!
   
 6. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #6
  Feb 4, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Vile vile kuna Wayuropa wanaoitwa VISHOKA. Hii ni Made in Poland (Polish)
   
 7. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2009
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,556
  Likes Received: 1,322
  Trophy Points: 280


  Pia wanaitwa wabrash viatu(wapolish)
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Feb 5, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,801
  Likes Received: 83,173
  Trophy Points: 280
  X-PASTER, unaonekana wewe ni mpiga hadithi mzuri sana. Ahsante kwa kutufumbua macho hata mimi hili la Wanigeria kuitwa wapopo nilikuwa sijui limeanzia wapi. Sijui na sisi Watanzania watu wa mataifa mengine wanatuitaje.
   
 9. M

  Mahmoud Qaasim JF-Expert Member

  #9
  Feb 5, 2009
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 922
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 60
  Wa-Kenya wanatuitwa Wa-Bongolala japo tunawaliza kila mara pamoja na "Ubongolala" wetu. iko siku watatujua kuwa sisi sio Bongolala kama wanavyofikiria.
   
 10. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #10
  Feb 5, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Naona dharau ya Wakenya kwetu ni kubwa sana. Afadhali Waganda wanakuwa na heshima (mutual respect). Labda ungenambia tunawaliza nini ili na mimi nifurahi!

  Mara nyingi ninapokutana nao huwa wengine wanajifanya wajuaji sana, ila wakigundua wewe ni mkali wao wanaingia mitini! Hata hivyo ni ukweli usiopingika kuwa ipo kazi kubwa kukabiliana na Wakenya katia EAC. Nafurahi sana kwamba angalau tumeanza na msimamo mzuri kuhusu ardhi na pia kuikataa tamaa ya madaraka ya M7. Mara nyingi watu wengine wanajaribu tumia udhaifu wakutojua kimombo kama fimbo ya kutupigia! Lakini kwa mwanzo huu naamini tutakula nao meza moja.
   
 11. Elusive

  Elusive JF-Expert Member

  #11
  Feb 5, 2009
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Waulizeni mabaharia wa zamani waliokuwa wanafuata meli ugirigi, wao ndo walileta haya majina kama ifuatavyo.

  Wagirigi - Wamanga
  Waturuki - Mabata
  Watanzania - Wabongo
  Wamarekani - Wanyamwezi
  Wanigeria - Mapopo
   
 12. K

  Kakulwa Senior Member

  #12
  Feb 6, 2009
  Joined: Oct 10, 2008
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  jina lao lingine unyamwezini ni mapolak
  sema mademu zao watamu kishenzi!!
   
 13. K

  Kakulwa Senior Member

  #13
  Feb 6, 2009
  Joined: Oct 10, 2008
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hivi hawa wakenya kwa nini wanadharau wabongo wakati wenyewe ni washamba kishenzi yani...yale mademu yao ndiyo duu
  kiingereza chao chenyewe mbona cha kawaida tu na class ukikutana nao unawakimbiza vilevile
  mimi huwa wananikalia mbali kabisa manake wanajua wakilianzisha basi watakimbia wenyewe.
   
Loading...