Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,325
- 11,193
Buriani kwa sisi waswahili ni maneno ya mwisho ya mtu ambaye amejiona yuko hatua za mwisho kufa na kuiacha dunia.
Salamu kama hizo leo zimetolewa kwa wingi kwenye mitandao ya kijamii kama tiktok na miningene amabayo JF huenda haijawezesha kutumika matoleo yao.
Mmoja kati ya wanaharakati hao ambaye huenda alitumia kijino cha mwisho cha chaji ya simu yake na mtandao wa kasi ya 2G amesema mengi.Machache nimeona nimnukuu hapa.
Neno terror halina maana isipokuwa kila mmoja na anavyokusudia
Haki za watoto na wanawake inategemea ni watoto na wanawake wa eneo gani.
Maazimio ya kivita na haki za wafungwa inahusiana na wafungwa wa nchi gani.
Wako wapi waislamu milioni 315 wanaoizunguka Palestina wakati wenzao wanachinjwa.
Watu wa Gaza hatuna wa kutunusuru isipokuwa ni Allah na yeye ndiye atakayehukumu siku ya kiama
Tunashahadia na tunakufa.Tutaonana siku ya kufufuliwa.
Baada ya kumsikiliza mpalestina huyo akiagana na dunia nikakumbuka ile jumuiya ya umoja wa nchi za kiislamu ambao miaka ya nyuma ulikuwa maarufu sana masikioni mwa watu na hata Tanzania ilitaka kujiunga nao.
Jumuiya za nchi za Kiarabu zinazoizunguka Palestina na Israel zimekutana katika hali ya kificho na kuondoka bila kutoa matamko ya maana.Upande wa OIC katika mzozo huu tangu tarehe 7 Oktoba sijawahi kuusikia kusema au kukutana popote.