Wanafunzi Wasomea Chini Ya Miti Dar... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi Wasomea Chini Ya Miti Dar...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by RRONDO, Jul 31, 2010.

 1. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #1
  Jul 31, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,879
  Likes Received: 20,925
  Trophy Points: 280
  *WANAFUNZI WA DARASA LA SABA WASOMEA CHINI YA MITI DAR


  [​IMG] Wanafunzi wa Darasa la saba wa Shule ya Msingi Mtoni Jijini Dar es Salaam, wakiwa katika masomo yao ya kila siku nje ya madarasani chini miti wakati wakifundishwa na mwalimu wao leo mchana. Walimu wa shule hiyo baada ya kuona kamera ya Sufianimafoto ikiwa kazini walijitetea kuwa wameamua kuwakusanya wanafunzi hao wa mikondo minne na kuwafundisha kwa pamoja, ili waweze kuelewa kwa pamoja kuelekea kujiandaa na mitihani ya darasa la saba ya mwaka huu. Lakini cha kushangaza ni kwamba kama hivyo ndivyo imekuwaje wanafunzi hao wote wafundishwe na mwalimu mmoja je wataweza kuelewa na lengo lao litatimia kweli?

  MATATIZO YA OFISI ZA WALIMU BADO NI CHANAGAMOTO...
  [​IMG] Walimu wa Shule ya Msingi Twiga ya Jijini Dar es Salaam, wakisahihisha madaftari ya wanafunzi wao wakiwa chini ya miti nje ya madarasa jambo linaloonyesha kuwa shuleni hapo kunaupungufu wa madarsa na ofisi za walimu.

  *MADARASA KAMA HAYA KWELI WANAFUNZI WATASOMA KWA BIDII?
  [​IMG] Hili pia ni moja kati ya madarasa ya Shule ya Msingi Twiga, kwakweli yanakatisha tamaa kwa wanafunzi kujisomea kwa bidii na hata kwa mzazi anayefika shuleni hapo na kuona mazingira hayo. Hapa mvua ikinyesha ni balaa na naamini ndani ya darasa hili patakuwa hapakaliki, Wadau hebu liangalieni hili kwa macha manne ili tukomboe Elimu ya Tanzania kwani hapa ni ndani ya Jiji kubwa na lenye maendeleo mengi na kila kitu kizuri na zaidi Jiji hili ndilo hasa lenye ofisi za wakuu wote wa nchi hii Je wakuu mnaridhika kweli kuwa na madarasa kama haya katika jiji kama hili? Kama Dar tu ni hivi je Vijijini ni vipi????

  [​IMG] Wanafunzi hao wakiendelea kufundishwa na hapa wamepigwa kwa nyuma ili kuonyesha uhalisia wa mahala penyewe na uwingi wao ambao bado wamekatwa kulingana na kamera kwa kweli ni wengi mno.....

  [​IMG]Wanafunzi wakiwa katika darasa bovu wakifurahia kupigwa picha....
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Jul 31, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Wow!
   
 3. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #3
  Jul 31, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  sasa hiyo ni dar ipo hivyo je huko mikoani vijjn kabisa hali ikoje? inackitisha kwa kweli.
   
 4. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #4
  Jul 31, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 2,004
  Likes Received: 1,054
  Trophy Points: 280
  Dar hali iko hivyo vp huko Choma cha Nkola, Tabora itakuwaje?
   
 5. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #5
  Jul 31, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  picha ya pili kutoka juu, walimu hawana viatu au ni mimacho yangu tu? ,halaf wanacheka na madaftari tu baada ya kuona flash ya picha. dah!
   
 6. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #6
  Jul 31, 2010
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Hayo mabati jamani yalivyo na kutu yakiporomoka na kuumiza wanafunzi mana yameshachoka mpaka kukatika katika..eeeh kweli kuna watu wanaishi duniani na wengine ulimwenguni!!
   
 7. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #7
  Jul 31, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,879
  Likes Received: 20,925
  Trophy Points: 280
  kwanini wapinzani wasitumie image kama hizi,hospitali kama temeke kuwaonyesha wananchi CCM ilipotufikisha??
   
 8. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #8
  Jul 31, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,879
  Likes Received: 20,925
  Trophy Points: 280
  hapo upepo mkali tu bati linachinja mwanafunzi.....lakini hawaoni hio hatari.....
   
 9. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #9
  Jul 31, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  hiyo bati ikikugusa ,tetanus yake ni bora ukumbwe na UKIMWI. dah! kidumu chama cha mapinduzi!
   
 10. bht

  bht JF-Expert Member

  #10
  Jul 31, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  Prondo wa kina nani hawaoni hatari?
  waalimu na wanafunzi?
  au watawala?
   
 11. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #11
  Jul 31, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,879
  Likes Received: 20,925
  Trophy Points: 280
  wote......ila nasamehe wanafunzi coz ni watoto hawajui hatari hata wakijua hawana cha kufanya
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Jul 31, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Mimi nadhani hata hao wapinzani ni sawa tu na CCM. Kwanza wengi wao ni wanachama wa zamani wa CCM.

  Pili, kwa ujumla na sisi wanachi tunachangia kwa kiasi kikubwa hali kama hizi kwa kuwa tegemezi sana kwa serikali. Hivi unataka kuniambia hapo kwenye hiyo shule wazazi wa watoto wasomao hapo wakijikusanya na kufanya harambee ya kuchangisha fedha za kuboresha mazingira ya shule hiyo watashindwa kweli kupata hela za kutosha? Maana usikute wazazi wengi wa hao watoto wanatumia hela nyingi sana ktk starehe zao.

  Tuna matatizo mengi sana lakini moja ya nililoliona ni ukosefu wa hamasa na mwamko wa kuupiga vita umaskini kwa vitendo. Tunapenda sana kuupiga vita umaskini kwa maneno. Laiti tungepunguza kuongea na kuongeza kutenda tungekuwa mbali sana kimaendeleo.
   
 13. bht

  bht JF-Expert Member

  #13
  Jul 31, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  wakiambiwa mambo ya 'hovyo hovyo' wanachangia kwa sifa na kujionesha.
   
 14. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #14
  Jul 31, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,879
  Likes Received: 20,925
  Trophy Points: 280
  tukiwa na moyo wa kujitolea kama kwenye maharusi na mambo kama hayo tungeweza kusaidia ku-improve vitu fulani.....lakini serikali inabidi iwe mfano.....ni ngumu mimi kuchangia wakati nalipa kodi na naona kodi hio inanunua LAND CRUISER V8 nyingi na najua bei ya gari hio moja ingetosha kununua madawati mengi sana au kuongeza madarasa......
   
 15. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #15
  Jul 31, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hili la kusomea chini mbona ni la kawaida kwa nchi hii.
  Wakati huo huo inaletwa timu ya nchi fulani inagharamiwa mabilioni kwa mabilioni.
   
 16. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #16
  Jul 31, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,879
  Likes Received: 20,925
  Trophy Points: 280
  kwanini iwe kawaida??hii hali haikubaliki lazima tuiondoe....mimi ningekuwa mwalimu mkuu shule yangu wanafunzi wasingekaa chini.
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Jul 31, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Sawa, kodi ndio tunalipa. Lakini mchango wa jumuia kwenda kwenye mali za jumuia kama mashule ni mchango ambao ni wa moja kwa moja na ni ninyi wenyewe ndio mtakaosimamia hayo matumizi ya fedha mlizozichanga. Hapo serikali mnaipiga bao na kuionyesha jinsi mambo yanavyopaswa kuwa.

  Hivi unadhani huko ughaibuni serikali huwafanyia watu kila kitu? Ikija kwenye mambo ya shule/elimu, bustani za kupumzikia, na sehemu za kuchezea watoto, ni jumuia za wanajamii waishio humo ambazo hukaa chini na kupanga mikakati na mbinu za kutatua matatizo yanayozikabili. Wenzetu huwaga hawasubiri serikali kuwafanyia kila kitu licha ya wao kulipa kodi pia.

  Tunaweza kabisa kuwa proactive sema basi tu tuko magoigoi na tusiopenda kujishughulisha kwa kubuni mbinu mpya za kufanya mambo yatakayoleta mabadiliko na ndio maana unaona kila kukicha serikali yetu inapokea misaada kutoka kwa wahisani. Kwa hiyo serikali yetu bila wahisani haitafanya kazi vizuri na sisi wananchi bila msaada wa serikali hakuna tunalolifanya. Shameful
   
 18. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #18
  Jul 31, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,879
  Likes Received: 20,925
  Trophy Points: 280
  mkuu....ughaibuni ni kubwa,ila sehemu ndogo ninayoijua mimi serikali inafanya hayo tunayolalamikia hapo[kwa shule za serikali]....habari ya madawati/madarasa ni jukumu la serikali....lakini ni kweli na sisi tunaweza kusaidia kutatua matatizo kama haya...ila serikali ionyeshe mfano na kututia moyo......serikali yetu inakatisha tamaa...kuna watu washaleta misaada wakajuta kwanini walijitolea kwa jinsi kulivyo na urasimu kila idara ya serikali
   
 19. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #19
  Jul 31, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,010
  Trophy Points: 280
  .
  Slaa rais mtarajiwa aliwaeleza wananchi wa Msoma jana jinsi ambavyo serikali inavyoendesha nchi kwa takwimu. Mkuu wa kaya na wasaidizi wake wanatembea na lukuki ya makabrasha mengine yakiandikwa na watu ambao hata hawaijui Tanzania. Hivi unavyomwonyesha mtu wa kawida graff ya maendeleo inavyopanda huku uhalisia ukidhihirisha huu mfano wa wanafunzi wakifundishiwa chini ya mti. Mie hapa sipati jibu ni nani chizi, kati ya mlisha takwimu na mlishwaji.
   
 20. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #20
  Jul 31, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,010
  Trophy Points: 280
  .
  Yakishachinja ndio unawaona watendaji wakihudhuria kwenye nyumba za misiba na L/cruiser V8 la mil180 kodi za wananchi, wakiwa na elfu hamsini ya udi. Aibu gani hii TZ?
   
Loading...