Wanafunzi Wasomea Chini Ya Miti Dar...

Wanafunzi Wasomea Chini Ya Miti Dar...

JK ana mpango wa kuwapa laptop hao walimu wote kufikia mwaka 2015. Pia ana mpango wa kuhakikisha kila shule ina kompyuta ifikapo 2015. Nafikiri atakuwa anaziweka humo chini ya miti. Haya yatakuwa ni maendeleo makubwa sana nchini.
 
Shule utafikiri NAZI concentration camp.There ought to be laws against these abuses. Hivi unategemea hawa wanaafunzi watakuwa watu wa kawaida kweli ? No wonder tunapataa marais Vikwete
 
Hivi wazazi wa watoto hawa wako wapi? How do you let your child go to a school looking like that? Unawezaje kuwa na amani kuwa mwanao is safe wakati hali halisi ndio kama hiyo. Kama wanaisubiri serikali kukarabati hiyo shule watasubiri sana, kwani ata wapinzani wakiingia madarakani hawatakarabati shule. Kama jamii inabidi tuwajibike na kubadilisha mazingira yetu, serikali haiwezi kutufanyia kila kitu. Tukiwa pro active itakuwa rahisi kuiwajibisha serikali kwani tutakuwa na mifano.
 
Hivi wazazi wa watoto hawa wako wapi? How do you let your child go to a school looking like that? Unawezaje kuwa na amani kuwa mwanao is safe wakati hali halisi ndio kama hiyo. Kama wanaisubiri serikali kukarabati hiyo shule watasubiri sana, kwani ata wapinzani wakiingia madarakani hawatakarabati shule. Kama jamii inabidi tuwajibike na kubadilisha mazingira yetu, serikali haiwezi kutufanyia kila kitu. Tukiwa pro active itakuwa rahisi kuiwajibisha serikali kwani tutakuwa na mifano.

labda ungejiuliza uwezo wa hao wazazi......i guess wangekuwa na uwezo wangewapeleka "st.academy school".....
 
Kama Mkuu wa kaya akifuta ziara za kitalii kwa mwaka mmoja nchi nzima inakuwa na madarasa na madawati ya kutosha

Lakini bahati mbaya hayo hayako katika priorities zetu
 
Hayo ndiyo MAISHA BORA yanayohubiriwa majukwaani kila kukicha. Hali kama hiyo iko DSM ambapo viongozi wote wa Taifa wamejilundika, ukisogea mikoa ya pembezoni kidogo utakayoyaona kama una roho ya huruma utaanza kulia kabla hujaelezwa chochote. Najaribu kufikiria pale Rais aliposema kwenye hotuba yake kuwa anashangaa jinsi mambo yalivyobadilika na kuwa ktk ziara zake mikoani kila anapopita wananchi wamejaa furaha tele kutokana na maendeleo yaliyopatikana hususan ktk kipindi cha awamu ya nne ya uongozi wake.

Wananchi wanatakiwa kufikiria kwa kina na kuangalia uhalisia wa mambo yanayotendeka ktk jamii na kuwa makini zaidi na maneno yanayotolewa na viongozi waliopewa jukumu la kuongoza taifa letu.
 
*wanafunzi wa darasa la saba wasomea chini ya miti dar


wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi mtoni jijini dar es salaam, wakiwa katika masomo yao ya kila siku nje ya madarasani chini miti wakati wakifundishwa na mwalimu wao leo mchana. Walimu wa shule hiyo baada ya kuona kamera ya sufianimafoto ikiwa kazini walijitetea kuwa wameamua kuwakusanya wanafunzi hao wa mikondo minne na kuwafundisha kwa pamoja, ili waweze kuelewa kwa pamoja kuelekea kujiandaa na mitihani ya darasa la saba ya mwaka huu. Lakini cha kushangaza ni kwamba kama hivyo ndivyo imekuwaje wanafunzi hao wote wafundishwe na mwalimu mmoja je wataweza kuelewa na lengo lao litatimia kweli?

matatizo ya ofisi za walimu bado ni chanagamoto...​
walimu wa shule ya msingi twiga ya jijini dar es salaam, wakisahihisha madaftari ya wanafunzi wao wakiwa chini ya miti nje ya madarasa jambo linaloonyesha kuwa shuleni hapo kunaupungufu wa madarsa na ofisi za walimu.

*madarasa kama haya kweli wanafunzi watasoma kwa bidii?
hili pia ni moja kati ya madarasa ya shule ya msingi twiga, kwakweli yanakatisha tamaa kwa wanafunzi kujisomea kwa bidii na hata kwa mzazi anayefika shuleni hapo na kuona mazingira hayo. Hapa mvua ikinyesha ni balaa na naamini ndani ya darasa hili patakuwa hapakaliki, wadau hebu liangalieni hili kwa macha manne ili tukomboe elimu ya tanzania kwani hapa ni ndani ya jiji kubwa na lenye maendeleo mengi na kila kitu kizuri na zaidi jiji hili ndilo hasa lenye ofisi za wakuu wote wa nchi hii je wakuu mnaridhika kweli kuwa na madarasa kama haya katika jiji kama hili? Kama dar tu ni hivi je vijijini ni vipi????

wanafunzi hao wakiendelea kufundishwa na hapa wamepigwa kwa nyuma ili kuonyesha uhalisia wa mahala penyewe na uwingi wao ambao bado wamekatwa kulingana na kamera kwa kweli ni wengi mno.....

9.jpg
wanafunzi wakiwa katika darasa bovu wakifurahia kupigwa picha....

inaonesha jinsi ilani ya ccm ilivyotekelezwa. Hatudanganyiki 2010
 
Kwa tulivyo wachoyo na wabinafsi akija kutokea mmoja wa hao watoto akawa mkubwa serikalini hatakumbuka (atasahau jumla), sioni kama ni KKT tu wa kumlaumu hapa, hao hao kina Dr Sl tutawapigia na incase wakishinda (hatutegemei anyway) mambo yatakuwa yaleyale tu.
 
Mimi nadhani hata hao wapinzani ni sawa tu na CCM. Kwanza wengi wao ni wanachama wa zamani wa CCM.

Pili, kwa ujumla na sisi wanachi tunachangia kwa kiasi kikubwa hali kama hizi kwa kuwa tegemezi sana kwa serikali. Hivi unataka kuniambia hapo kwenye hiyo shule wazazi wa watoto wasomao hapo wakijikusanya na kufanya harambee ya kuchangisha fedha za kuboresha mazingira ya shule hiyo watashindwa kweli kupata hela za kutosha? Maana usikute wazazi wengi wa hao watoto wanatumia hela nyingi sana ktk starehe zao.

Tuna matatizo mengi sana lakini moja ya nililoliona ni ukosefu wa hamasa na mwamko wa kuupiga vita umaskini kwa vitendo. Tunapenda sana kuupiga vita umaskini kwa maneno. Laiti tungepunguza kuongea na kuongeza kutenda tungekuwa mbali sana kimaendeleo.
NN hivi tutachangia mangapi na sisi tuna ukata kibao? Hapa naomba nipishane na wewe mawazo!
Hizo kodi zetu wanazotanulia hawa wezi kweli nitapat wapi courage ya kuchanga wakati mtu anachota 300 b na kuondoka na anatanua kwa matusi tu mengi huko mtaani?
Mimi ni mmoja kati ya watu wanaochangia sana shughuli za maendeleo hasa kwenye eneo langu. Lakini kwa pesa ya nchi hii inavyochezewa nasita kuendelea kuchangia.
Angalia wenzetu wazungu wametuchangia kiasi gani na kimetutoa tulipokuwa kiasi gani? yaani mpaka sasa wao nao wanajiuliza kuwa pamoja na misaada yote tunayopata mbona hatusogei? No, nadhani kuna shida mahali fulani! Tukianza kufikili kila kitu wananchi watachangia kwa kuwa serikali ime-prove kushindwa tutashindwa kwenda mbele.
 
Back
Top Bottom