Wanafunzi wajawazito kuendelea na shule je, wale walioko jela nao waendelee na masomo?

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Waraka wa Mhe. Waziri wa Elimu unaotoa ruhusa kwa wanafunzi wajawazito kurudi shule kuendelea na masomo baada ya kujifungua haujatoa majibu kuhusu haki ya elimu kwa wanafunzi/watoto wadogo walioko jela za watoto nao waendelee na masomo wanapotumikia vifungo vyao au hatima za maisha yao ndiyo zimeishia jela?

Kiufupi, waraka huu umeharakishwa kisiasa kuliko kisayansi na kuacha nje mambo muhimu kama haki ya elimu ya wanafunzi waliko jela na pia wanafunzi wanaotia mimba walimu wao.

Taswira kwa hisani ya google.

1643199637742.png


Wafungwa-watoto wa umri wa shule/chuo je, wanaweza kusoma wakiwa gerezani sawa na wale wanaorudishwa shuleni baada ya kujifungua?
 
Back
Top Bottom