dudus
JF-Expert Member
- Feb 28, 2011
- 22,126
- 49,385
Wakuu heshima;
Pamoja na kasi iliyopo nchini ya kumtafuta sana elimu popote alipo hata kama ni Uchina, kuna "wajinga" fulani hapo wilayani Rufiji badala kuzingatia masomo wao wanatishia kuwabaka walimu wa kike hapo shuleni kwao.
Taarifa hizi nimezipata asubuhi ya leo kwenye kipindi cha Radio One Nipashe ambapo mwandishi alifanya mahojiano na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji (sorry, nimemsahau jina). Mkuu wa Wilaya amethibitisha ukweli wa habari hizo na ameiagiza mamlaka husika kuifunga shule hiyo kutokana na utovu wa nidhamu uliokithiri kiasi kwamba imefikia hatua walimu wote kuomba uhamisho au kuacha kazi baada ya kukerwa na tabia chafu za wanafunzi wa kiume shuleni hapo.
Haya wakuu, hiyo ni "sample" tu kati ya shule zetu kadhaa zenye mienendo isiyoridhisha kitaaluma na kimaadili. Nawasilisha mezani kwenu Great Thinkers.
My Take:
(i) Hivi huu utovu wa maadili uliopitiliza unaoelekea kusambaa kwa kasi nchini hadi kwa "watoto wadogo" chanzo na athari zake kwa mustakabali wa taifa letu ni nini? Na ni hatua gani zichukuliwe?
(ii) Hivi hawa "maamuma" wanajua kinachoendelea duniani kweli hawa? wanajua nafasi ya elimu katika maisha ya mwanadamu wa leo? Si ndio hawa hawa leo wanachezea nafasi waliyoipata na ndio wa kwanza kesho kulalamika "tunaonewa"?
(iii) Rufiji ni kati ya maeneo yaliyo nyuma kielimu nchini. Ilitegemewa wangechangamkia sana fursa hii ili kujikomboa lakini inaonekana kuwa kinyume. Jamii za huko zina mchango gani katika kadhia hii? Wazazi na hata taasisi za kidini nini mchango wao hapa; malezi ya watoto na maadili kwa ujumla?
(vi) Endapo shule hiyo itafungwa kwa mujibu wa agizo la DC, nini kitegemewe? Maandamano ya wanafunzi na wanajamii kupinga "uonevu" huu kama ambavyo imekuwa ikishuhudiwa siku za hivi karibuni? Mihadhara mikali mikali kwenye nyumba za ibada na shutuma kwenye media za kidini kupinga uonevu huu "uliokithiri" kama ambavyo imetokea kule Tunduru, Bagamoyo, n.k?