Ukweli kuhusu ziara za mafunzo na masomo ya vitendo Israel

Mzee Abaya

JF-Expert Member
Nov 20, 2023
700
1,826
Kumekuwa na upotoshaji kuhusu ziara za mafunzo na vitendo (Internship programs) zinazofanywa na wanafunzi wa fani za Kilimo na ufugaji toka pale SUA na hii ni baada ya vifo vya vijana wetu wawili waliouliwa na HAMAS.

Na declare interest kuwa mimi ni mmoja wapo wa member waanzilishi wa SUGECO nikiwa kama graduate wa SUA mwaka 2011 na mnufaika wa "grant" tulizopata pitia SUGECO 2012.

SUGECO ni ushirika wa wanafunzi wa SUA ulioanzishwa mwaka 2011 kwa lengo la kubadilisha "mind set" ya wanafunzi ili wawe na wafanye ujasiliamali pitia Kilimo. Ushirika huu ulisajiliwa na kuanzishwa rasmi mwaka huo na mwaka 2012 ulianza kutoa grants kwa graduates wa SUA ili waweze kujiajiri kupitia Kilimo nami ni mmoja wa wanufaika na nilipewa 20M kwa ajili ya shughuli za kilimo.

Katika kuendeleza "entrepreneurship mind" kwa vijana, SUGECO toka mwaka 2015 imekuwa ikitafuta fursa za vijana kwenda kujiendeleza kwa kufanya mafunzo ya vitendo kwa kuwapeleka vijana sehemu mbalimbali duniani kama Israel, Marekani na sasa Denmark.

Jumla ya wanafunzi 900 wamepelekwa sehemu mbalimbali duniani ambapo 400 wamepelekwa Israel, 420 wamepelekwa USA na 80 wamepelekwa Denmark kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.

Utaratibu huu na ushirikiano kupeleka wanafunzi kufanya mazoezi kwa vitendo sio Israel ni sio kwa SUA tu bali vyuo vingi vinafanya hivyo kwa sababu ni kweli Israel ina teknolojia ya hali ya juu kwenye Kilimo kulinganisha na nchi nyingine duniani.

Kuna chuo nakifahamu kipo kule Kilolo Iringa nacho kina program hiyo ya kupeleka wanafunzi Israel kwenda kujifunza kuhusu kilimo na mwaka 2022 kilipeleka vijana 8 kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo na walikaa kule mwaka mzima akiwemo mdogo wangu na sasa amejiajiri na anaendeleza maisha yake pitia Kilimo.

Wanapofika kule, vijana hawa huwa wanapelekwa kwenye mashamba maeneo mbalimbali ikiwemo Kibbutz eneo maarufu kwa shughuli za Kilimo hivyo sio kweli kwamba wanapelekwa jeshini au kufanywa manamba ila wamekuwa wakienda kufanya mafunzo ya vitendo kwa ajili ya kuboresha sekta ya kilimo Tanzania

FB_IMG_1704082937726.jpg

Picha inajieleza

FB_IMG_1704083065509.jpg

Kijana wa Kitanzania aliyepelekwa Israel kwa ajili ya mafunzo kwa Vitendo. Nenda pale Kondoa Mision uone anavyopiga kazi. Jamaa ni very smart.

FB_IMG_1704083174706.jpg

Nembo ya SUGECO japo we Mkurugenzi wa Kwanza uliyekuwa mwanafunzi mwenzetu pale SUA ulininyanganya Demu wangu Flora na kumuoa wewe. Sawa tu we si ulikuwa Mkurugenzi mi nilikuwa home hahe ila ilikuwa Pisi Kali sana ile. Dah, yalikuwa maisha tu ila sasa nimetoboa.😀😃😄😁😆
 
Back
Top Bottom