Wanafunzi vyuo wakosa mikopo, Serikali haina fedha

Mtaisoma namba.mmekataa elimu bure mpaka chuo kikuu

sunzu,usiwalaumu watanzania kwa kukataa elimu bure,walaumu NEC kwa kupindisha haki sisi 62%ya watanzania tulimchagua lowassa,hao walio bakia wacha waisome namba mbwa hao,sasa hivi hakuna kuwasaidia,kama walichagua chama tawalawa waanze kujiuza sasa, HAPA KAZI TU
 
Nafikiri njia rahisi ya demokrasia ya kweli ni kura ya wazi kwani haina utata wala matokeo hayachelewi kwani mtu wa mwisho anapohesabiwa tu na matokeo tayari na hakuna cha kulinda kura wala nini - sehemu ya kupangia mistari ni barabara za mitaa na kubwa.
 
Asimilia 82 ya Wanafunzi Wakosa Mikopo 2015/16

Zaidi-ya wanafundi 50,000 watashindwa kuendelea na masomo ya elimu ya juu kutokana na kushindwa kupata mikopo kutoka katika Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB).

Hayo yamebainika ikiwa ni siku tatu tangu HESLB kutoa majina ya wanafunzi waliofanikiwa kupata mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016, huku idadi kubwa ikiwa haimo katika majina hayo.Katika mwaka huu wa masomo bodi ya mikopo imeweza kuwapatia mikopo wanafunzi 12,000 pekee sawa na 17.1% ya waombaji zaidi ya 70,000, hivyo kufanya idadi ya wanafunzi waliokosa mikopo kufikia asilimia 82.9 ya waombaji wote.

Wanafunzi waliokosa mikopo ya kuwawezesha kujiunga na elimu ya juu na hivyo wazazi wao kutakiwa kugharamia elimu hiyo wameelezea kusikitishwa na hali hiyo huku wakiitaka serikali kuwaangalia kwa jicho la kipekee kwani hawana uwezo wa kuanza masomo pasipo kufadhiliwa na serikali.

Wanafunzi hao walionekana kukata tamaa ya kutimiza ndoto yao ya kujiunga na elimu ya chuo kikuu, wamefika makao makuu ya bodi hiyo huku wakiongozana na baadhi ya viongozi wa serikali ya wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kutaka kujua hatima yao.

Nimetokea Tabora, wazazi wangu walinipa Sh. 100,000 ya kutumia wakiamini tunapewa mikopo na serikali, lakini tumenyimwa na hatujui hatima yetu, nimebakiwa na Sh. 6,000, naomba serikali ituhurumie, isikie kilio chetu hatustahili kuteseka hivi,?-ameeleza Abdul Omary mwanafunzi mteule UDSM.Fatuma Bakari, mwanafunzi mwingine kutoka UDSM, amesema:-

Siwezi kujiunga na Chuo bila mkopo, tumefika hapa ili kuomba bodi ya mikopo itusaidie hatuna tumaini lolote zaidi ya kuomba Mungu atusaidie tuweze kupata mikopo na kuanza masomo.

Waziri wa Mikopo serikali ya wanafunzi (Daruso), Shitindi Venance ameeleza kutokukubaliana na majibu waliyopewa na uongozi wa juu wa bodi ya mikopo kwani yanakatisha tamaa na kuzima ndoto za wanafunzi wa masikini kusoma chuo kikuu.?Hapa UDSM ni wanafunzi 600 tu waliopata mikopo kati ya wanafunzi 7,000 waliopangiwa kuanza masomo, hili ni janga kubwa kwa watoto wa masikini kwani hawawezi kujisajili chuoni wala kupata makazi katika mabweni mpaka walipe ada na wengi wametoka mikoani.

Tunachukua hatua moja mbele na kuamua kulifuatilia suala hili kwa katibu mkuu wa wizara ya elimu na katibu mkuu wa wizara ya fedha kwa sababu bodi bado wanasisitiza tuwe na subira ilihali muda umeenda na wanafunzi wanateseka ameeleza Shitindi.

Mkurugenzi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HESLB, Omega Ngole amewaambia wanahabari waliofika ofisini kwake kuwa bodi haistahili kulaumiwa kwani serikali kupitia wizara ya fedha na wizara ya elimu ndio yenye uwezo wa kutenga kiasi cha fedha kulingana na mahitaji ya wakati husika.

Lengo la bodi ya mikopo ni kuwawezesha wanafunzi wa vyuo vikuu kusoma kwa ufadhili wa serikali na wala sio kuwakwamisha, tunaendelea kujadiliana na serikali kuona kama itatuongeza fedha ili tuweze kutoa awamu ya pili ya majina ya wanafunzi waliopata mikopo, tunawaomba wanafunzi wavute subira,?-anaeleza NgoleHata hivyo Ngole amesema hawezi kusema lini watatangaza majina ya awamu ya pili kwani hilo linategemea ni lini serikali itatoa fedha kwa ajili ya wanafunzi wa awam ya pili.

Katika mwaka uliopita wa masomo 2014/2015 serikali ilitoa mikopo kwa wanafunzi 30,000 sawa na 51.7% ya waombaji wote 58,000 na hivyo kufanya waliokosa mikopo kuwa wanafunzi 28,000 sawa na 49% pekee tofauti na mwaka huu ambapo waliokosa wamefikia asilimia 82.9

Chanzo: Mpekuzi blog
kwani mlipo kuwa mna ambiwa ccm ni ile ile mlikuwa mnafikri wanatania?
 
You made choices enl vs jpm! !!!!!!!! And yet more to come!
 
Walipewa tahadhari kwenye wimbo wa tumejipanga mwaka huu wataisoma
 
Nadhani serikali ikijipanga vizuri watapewa mikopo. Kwa sasa hela nyingi imetumika kwenye kampeni but ni jambo la kujiuliza "je hapakuwa na bajeti ya mikopo?" Na kama ilikuwepo kwa nini wasipewe kwa muda muafaka?
Serikali kupitia wizara ya Elimu ilijua mapema kuwa ni wanafunzi wangapi watadahiliwa mwaka huu. So kitendo cha kusema"subiri" ni mojawapo ya utendaji mbaya ambapo JPM anapaswa aanze nao hao hao.

Ataanzaje nao na angali zilitumika kumfikisha hapo alipo
 
Asimilia 82 ya Wanafunzi Wakosa Mikopo 2015/16

Zaidi-ya wanafundi 50,000 watashindwa kuendelea na masomo ya elimu ya juu kutokana na kushindwa kupata mikopo kutoka katika Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB).

Hayo yamebainika ikiwa ni siku tatu tangu HESLB kutoa majina ya wanafunzi waliofanikiwa kupata mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016, huku idadi kubwa ikiwa haimo katika majina hayo.Katika mwaka huu wa masomo bodi ya mikopo imeweza kuwapatia mikopo wanafunzi 12,000 pekee sawa na 17.1% ya waombaji zaidi ya 70,000, hivyo kufanya idadi ya wanafunzi waliokosa mikopo kufikia asilimia 82.9 ya waombaji wote.

Wanafunzi waliokosa mikopo ya kuwawezesha kujiunga na elimu ya juu na hivyo wazazi wao kutakiwa kugharamia elimu hiyo wameelezea kusikitishwa na hali hiyo huku wakiitaka serikali kuwaangalia kwa jicho la kipekee kwani hawana uwezo wa kuanza masomo pasipo kufadhiliwa na serikali.

Wanafunzi hao walionekana kukata tamaa ya kutimiza ndoto yao ya kujiunga na elimu ya chuo kikuu, wamefika makao makuu ya bodi hiyo huku wakiongozana na baadhi ya viongozi wa serikali ya wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kutaka kujua hatima yao.

Nimetokea Tabora, wazazi wangu walinipa Sh. 100,000 ya kutumia wakiamini tunapewa mikopo na serikali, lakini tumenyimwa na hatujui hatima yetu, nimebakiwa na Sh. 6,000, naomba serikali ituhurumie, isikie kilio chetu hatustahili kuteseka hivi,?-ameeleza Abdul Omary mwanafunzi mteule UDSM.Fatuma Bakari, mwanafunzi mwingine kutoka UDSM, amesema:-

Siwezi kujiunga na Chuo bila mkopo, tumefika hapa ili kuomba bodi ya mikopo itusaidie hatuna tumaini lolote zaidi ya kuomba Mungu atusaidie tuweze kupata mikopo na kuanza masomo.

Waziri wa Mikopo serikali ya wanafunzi (Daruso), Shitindi Venance ameeleza kutokukubaliana na majibu waliyopewa na uongozi wa juu wa bodi ya mikopo kwani yanakatisha tamaa na kuzima ndoto za wanafunzi wa masikini kusoma chuo kikuu.?Hapa UDSM ni wanafunzi 600 tu waliopata mikopo kati ya wanafunzi 7,000 waliopangiwa kuanza masomo, hili ni janga kubwa kwa watoto wa masikini kwani hawawezi kujisajili chuoni wala kupata makazi katika mabweni mpaka walipe ada na wengi wametoka mikoani.

Tunachukua hatua moja mbele na kuamua kulifuatilia suala hili kwa katibu mkuu wa wizara ya elimu na katibu mkuu wa wizara ya fedha kwa sababu bodi bado wanasisitiza tuwe na subira ilihali muda umeenda na wanafunzi wanateseka ameeleza Shitindi.

Mkurugenzi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HESLB, Omega Ngole amewaambia wanahabari waliofika ofisini kwake kuwa bodi haistahili kulaumiwa kwani serikali kupitia wizara ya fedha na wizara ya elimu ndio yenye uwezo wa kutenga kiasi cha fedha kulingana na mahitaji ya wakati husika.

Lengo la bodi ya mikopo ni kuwawezesha wanafunzi wa vyuo vikuu kusoma kwa ufadhili wa serikali na wala sio kuwakwamisha, tunaendelea kujadiliana na serikali kuona kama itatuongeza fedha ili tuweze kutoa awamu ya pili ya majina ya wanafunzi waliopata mikopo, tunawaomba wanafunzi wavute subira,?-anaeleza NgoleHata hivyo Ngole amesema hawezi kusema lini watatangaza majina ya awamu ya pili kwani hilo linategemea ni lini serikali itatoa fedha kwa ajili ya wanafunzi wa awam ya pili.

Katika mwaka uliopita wa masomo 2014/2015 serikali ilitoa mikopo kwa wanafunzi 30,000 sawa na 51.7% ya waombaji wote 58,000 na hivyo kufanya waliokosa mikopo kuwa wanafunzi 28,000 sawa na 49% pekee tofauti na mwaka huu ambapo waliokosa wamefikia asilimia 82.9

Chanzo: Mpekuzi blog

Fedha zooote za Mikoppo Waililipwa wasanii ktk kampeni.

Iombeni HESLB iazime fedha kwa wasanii kisha iwakopeshe wanafunzi.
 
Mlikichagua wenyewe acha muisome namba_ _ _ _mbele kwa mbeleeeee
 
Back
Top Bottom