Hapana, ni uzushi huo wanaousambaza watu. Habari za uhakika kutoka kwa wanafunzi wenyewe zinaeleza kwamba Mpishi mkuu wa wanafunzi aliamua kubadilisha ratiba ya chakula ghafla na kubandika tangazo ukutani bila ya wanafunzi kushirikishwa siku ya Alhamisi, Ijumaa akafanya kweli kama alivyotangaza.
Viongozi wa wanachuo walipomwuuliza Mkurugenzi wa Taasisi aliwakutanisha mpishi mkuu huyo na wanafunzi, ikaelezwa kwamba alipaswa kuwashirikisha wanafunzi kabla ya maamuzi. Lakini Ijumaa jioni wanachuo wakajikuta wamepikiwa samaki wa Maghufuri na ugali badala ya wali kama walivyozoea, wakasusa.
Jumamosi wakati wanaulizana wanafunzi wale wasile siku hiyo, akaja Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi kuongea na wanafunzi, akaongea fyatu akiwaambia kama hawataki kula shauri yao. Kwa kujibu mapigo wanafunzi wakaungana tena kususia kabisa weekend yote chakula cha mpishi huyo. Hata wale waliokuwa afadhali walitaka kurudi wakale wakapata hasira na kususia. Walikwenda watu wa TBC1 na ITV kwa mwito kwenye story, lakini mpishi mkuu akakataa kuongea nao, pia walifungia masufuria ya chakula wapiga picha wasione, pamoja na kubembelezwa wakakataa kufungua yapigwe picha, wakaachia nyanya na vitunguu walivyokatakata tu.
Jumatatu asubuhi leo kwa msimamo mmoja wanachuo wakataka kumwona Mkurugenzi Mtendaji wa MNH ambaye ndiye mwenye dhamana na jiko lao. Bahati mbaya jamaa yupo kutibiwa India (kumbe hata madaktari hawaithamini hospitali yao wanaenda nje ila makabwela tu!). Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof Swai akasikilizana na timu ya uongozi wa wanafunzi kwamba ratiba ya zamani irejelewe kwa muda huu mpaka kitakapoeleweka baadaye, lakini akawaahidi kwamba atazungumza na serikali ya wanafunzi Jumatano, kisha na wanachuo wote Alhamisi kujua mwisho wa tatizo hilo. Wanafunzi wakaondoka zao.
Palikuwao polisi kibao wapelelezi katika nguo zao za kawaida, lakini walisikika wengine wakitoa taarifa kwa simu, kwamba wanachuo bado wako ka Swai lakini wametulia na hakuna dalili ya fujo yoyote. Madai ya wanachuo makubwa ni:
- Mpishi mkuu atimuliwe pale au apelekwe kokote lakini sio pale.
- Wapishi kadhaa wana lugha mbaya kwa wanachuo na hawatakiwi pale
- Ratiba ya zamani itulie japo hata hiyo sio nzuri sana
- Wapewe maelezo ya idadi ya wanachuo wanaopaswa kula pale na wanaochangia cost sharing - wanaojifadhili, wanaofadhiliwa na serikali na wanaotoka nje ya nchi na wamechangia kiasi gani.
- Wizara inaleta kiasi gani kwa wao kula chuoni
- Nini kinapungua katika mlolongo wa manunuzi iliwanachuo washauri kitu gani kifanyike
- Fidia itolewe kwa siku zile ambazo mpishi mkuu aliwalisha maharage mchana na usiku wanafunzi pasipo maelezo na je ya ratiba iliyokuwapo wakati wanafungua chuo, pia fidia itolewe kwa kile chakula ambacho ilikuwa wale tangia Ijumaa 9/1/10 hadi leo 11.1.10.
Kwa hiyo,sio kweli kwamba wanafunzi wanataka kula kuku kwa mrija kila siku, ila wasilishwe kama mifugoila washirikishwe kupanga nini wanatakiwa kula. Sio mtu anaamua tu leo mle ugali, kesho mnywe chai tu.
Hizo ndizo habari kamili kwa kiwango kilichokusanywa kutoka kwa wanaohusika. Waandishi wa habari walikuwapo kutoka ITV na TBC1 na wenginer, labda nao wataeleza ya kwao kwa kadiri ya ufahamu wao.
Leka