Wanafunzi Muhimbili Waandamana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi Muhimbili Waandamana

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lekanjobe Kubinika, Jan 11, 2010.

 1. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sasa hivi ninapoandika mambo haya wanafunzi wa vyuo vya Taasisi za Afya Shiriki Muhimbili, ambao ndio uti wa mgongo wa shughuli za maabara, uuguzi na baadhi ya tiba katika hospitali ya Taifa Muhimbili wameandamana na wanasemekana wako ofin kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo.

  Wanafunzi hao wanafadhiliwa na Wizara ya Afya, analipwa mkurugenzi 50 Million kila semesta kwa kuwalisha wanafunzi ambao ni wengi wanaochukukuwa program za MUHAS. Hasikii kitu akiulizwa anawalisha nini watu hawa.

  Wote wanafunzi wamegoma kuingia madarasani. Atakayeingia ati ni mkong'oto. Habari zaidi baadaye.

  Leka
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,269
  Likes Received: 22,029
  Trophy Points: 280
  Ndio elimu ya juu kwa vyuo vyetu bongoland ilivyo.
   
 3. al1983

  al1983 JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 230
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 60
  Migogoro katika vyuo vikuu hapa nchini imekuwa ni kama msimu wa jua au mvua, kwa maana ya kwamba kila mwaka huwa mvua zinanyesha na jua huwaka pia kwa kipindi fulani. Sasa ni jambo linalostaajabisha kuona taifa letu kupitia vyombo husika linashindwa kutatua migogoro hii. Nadhani ifikie mahala haya mambo yawe historia tu. Watanzania tunapaswa kubadilika na kuwa misingi imara pamoja na dira ya Taifa letu ili huko mbeleni tusijikute tena kwenye matatizo kama haya. NI LAZIMA TUWAJIBIKE KWA MAMBO YETU SISI WENYEWE NA SI KUSUBIRI WAHISANI NA WAFADHILI TU KILA WAKATI.
   
 4. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2010
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Unafikiri suluhu itapatikana? wanajitafutia kufukuzwa shule hao, bora wavumilie miaka hiyo 3 sio mingi, watakula vizuri makwao.
   
 5. O

  Omumura JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nasikia wanataka kula chips, wali, kuku,kitimoto, samaki wa kuokwa na prawns.Hawataki makande, maharage na ugali, duh,!!
   
 6. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hapana, ni uzushi huo wanaousambaza watu. Habari za uhakika kutoka kwa wanafunzi wenyewe zinaeleza kwamba Mpishi mkuu wa wanafunzi aliamua kubadilisha ratiba ya chakula ghafla na kubandika tangazo ukutani bila ya wanafunzi kushirikishwa siku ya Alhamisi, Ijumaa akafanya kweli kama alivyotangaza.

  Viongozi wa wanachuo walipomwuuliza Mkurugenzi wa Taasisi aliwakutanisha mpishi mkuu huyo na wanafunzi, ikaelezwa kwamba alipaswa kuwashirikisha wanafunzi kabla ya maamuzi. Lakini Ijumaa jioni wanachuo wakajikuta wamepikiwa samaki wa Maghufuri na ugali badala ya wali kama walivyozoea, wakasusa.

  Jumamosi wakati wanaulizana wanafunzi wale wasile siku hiyo, akaja Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi kuongea na wanafunzi, akaongea fyatu akiwaambia kama hawataki kula shauri yao. Kwa kujibu mapigo wanafunzi wakaungana tena kususia kabisa weekend yote chakula cha mpishi huyo. Hata wale waliokuwa afadhali walitaka kurudi wakale wakapata hasira na kususia. Walikwenda watu wa TBC1 na ITV kwa mwito kwenye story, lakini mpishi mkuu akakataa kuongea nao, pia walifungia masufuria ya chakula wapiga picha wasione, pamoja na kubembelezwa wakakataa kufungua yapigwe picha, wakaachia nyanya na vitunguu walivyokatakata tu.

  Jumatatu asubuhi leo kwa msimamo mmoja wanachuo wakataka kumwona Mkurugenzi Mtendaji wa MNH ambaye ndiye mwenye dhamana na jiko lao. Bahati mbaya jamaa yupo kutibiwa India (kumbe hata madaktari hawaithamini hospitali yao wanaenda nje ila makabwela tu!). Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof Swai akasikilizana na timu ya uongozi wa wanafunzi kwamba ratiba ya zamani irejelewe kwa muda huu mpaka kitakapoeleweka baadaye, lakini akawaahidi kwamba atazungumza na serikali ya wanafunzi Jumatano, kisha na wanachuo wote Alhamisi kujua mwisho wa tatizo hilo. Wanafunzi wakaondoka zao.

  Palikuwao polisi kibao wapelelezi katika nguo zao za kawaida, lakini walisikika wengine wakitoa taarifa kwa simu, kwamba wanachuo bado wako ka Swai lakini wametulia na hakuna dalili ya fujo yoyote. Madai ya wanachuo makubwa ni:
  1. Mpishi mkuu atimuliwe pale au apelekwe kokote lakini sio pale.
  2. Wapishi kadhaa wana lugha mbaya kwa wanachuo na hawatakiwi pale
  3. Ratiba ya zamani itulie japo hata hiyo sio nzuri sana
  4. Wapewe maelezo ya idadi ya wanachuo wanaopaswa kula pale na wanaochangia cost sharing - wanaojifadhili, wanaofadhiliwa na serikali na wanaotoka nje ya nchi na wamechangia kiasi gani.
  5. Wizara inaleta kiasi gani kwa wao kula chuoni
  6. Nini kinapungua katika mlolongo wa manunuzi iliwanachuo washauri kitu gani kifanyike
  7. Fidia itolewe kwa siku zile ambazo mpishi mkuu aliwalisha maharage mchana na usiku wanafunzi pasipo maelezo na je ya ratiba iliyokuwapo wakati wanafungua chuo, pia fidia itolewe kwa kile chakula ambacho ilikuwa wale tangia Ijumaa 9/1/10 hadi leo 11.1.10.
  Kwa hiyo,sio kweli kwamba wanafunzi wanataka kula kuku kwa mrija kila siku, ila wasilishwe kama mifugoila washirikishwe kupanga nini wanatakiwa kula. Sio mtu anaamua tu leo mle ugali, kesho mnywe chai tu.

  Hizo ndizo habari kamili kwa kiwango kilichokusanywa kutoka kwa wanaohusika. Waandishi wa habari walikuwapo kutoka ITV na TBC1 na wenginer, labda nao wataeleza ya kwao kwa kadiri ya ufahamu wao.

  Leka
   
 7. O

  Omumura JF-Expert Member

  #7
  Jan 11, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  Ok, umesomeka mkuu!
   
 8. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #8
  Jan 11, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hili la kwamba Ijumaa jioni wanafunzi hao waligoma kwa sababu ilikuwa siku ya Wali lakini wakakuta wamepikiwa Ugali na Samaki wa Magufuli Halijakaa vyema. Labda kama kuna lingine ambalo hatujaambiwa lakini kama ni hili tu ama lingine linalofanana nalo, kuna mtu ameishasema vizuri hapo juu, Wasome kama kula vizuri watakwenda kula kwao.
   
 9. M

  Mong'oo Member

  #9
  Jan 11, 2010
  Joined: Oct 13, 2008
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Hivi kuna vyuo bado wanapikiwa Tanzania? Si wanafunzi wanapewa hela wanajinunuliwa chakula anachotaka? Nadhani ili kuboresha hao wanafunzi wapewa hela halafu wajinunulie wanachotaka. Sio utaratibu nzuri maana lazima lawama zitakuwepo.

  Poleni sana
   
 10. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #10
  Jan 11, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,276
  Likes Received: 19,427
  Trophy Points: 280
  Leh! hawa jamb wanachezea shilingi ******.kwani huko kwao wanakula hizo kuku kila siku?
   
Loading...