Wanafunzi Law School mnayo nafasi ya kujipigania

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,879
35,881
Yamekuwa yakisikika matokeo yasiyo na tija Law School.

Kwamba wanafaulu wanafunzi chini ya 3%? Kwamba wanafunzi bado mpo tu kama makondoo mmetulia kumsubiri nani kuwapigania?

Shule zinaposhindana ubora kwa kufaulisha, kwa nini Law School wao wanajinasibu ubora kwa kufelisha? Kwamba hawa wa kozi ya miezi kadhaa tu ndiyo wenye ubora mno kuliko vyuoni walikotoka wanafunzi hawa?

Ni muhimu kutambua Tanzania ni jamii ya watu waliojaa wivu, choyo, husuda, fitna, ujinga, upumbavu na ujuaji uliopitiliza.

Siyo serikali, wananchi wala Mwakyembe atakayekuja kuwasemea ninyi la maana.

Ripoti ya Tume ya Mwakyembe ni another Professorial Rubbish

Waungwana kama kina Prof. Mahalu hao ni exceptions na ni wachache mno.

Kadhia ya Law School "Wasomi Nguli" wasikilizwe

Ukiritimba wa Law School ni lazima umalizwe. Mwenye jukumu la kuumaliza ukiritimba huo ni nyie wenyewe. Vinginevyo mtaendelea kuwa mbuzi wa kafara milele.

Mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe.

Isimamisheni shule hii hadi kieleweke, na inawezekana.

Wanafunzi Law School kulikoni kushindwa kujisimamia

Kwa nini kwenda kusomea kufeli? Kama mnadhani wanaofeli kila mwaka ni wao siyo nyie, yatakapowakuta msituletee huku kelele zenu.

Biashara asubuhi na kupanga ni kuchagua.
 
Mkuu, suala la Wanafunzi kupinga lingekuwa lina mashiko iwapo katika Watahiniwa wote kama ni 800 basi asiwepo hata mmoja aliyefauru.

Lakini watahiniwa 800 alafu unakuta kuna wenzio kadhaa 23 wamefauru, hii iwe kama ni alert ⚠️ kwa Watahiniwa kuongeza bidii ya kujifunza wawapo Law School.

Changamoto ninayo iona, kuna uwezekano Wanafunzi wanakuwa busy na utafutaji/ kazi na kukosa muda wa kujisomea.

Nina uhakika zaidi ya 57% hadi 70% ya Wanafunzi wa law school ni in service
 
Kuna muda mwanafunzi anapofeli na mwalimu naye anapaswa ajitathimini kiukweli kwenye ufundishaji wake kama kweli anaeleweka

Si muda tu. Mass failure haiwezi ku m exempt mwalimu.

Kwa nini shule bora zimekuwa zile zenye kufaulisha wanafunzi wengi? Kwa nini shule zinazoshika namba za juu ni zenye ufaulishaji zaidi na siyo zenye kufelisha?

Hapa walimu wote walikuwa wa kufurushwa tu. Ajabu na kweli wanafunzi waliopo pale leo, kana mbuzi wa kafara wapo wapo tu nao wanasubiri kufeli.

Nani awapiganie ninyi sasa? Ni hawa watanzania wajuaji wasioyatakia mema mafanikio yenu?
 
Mkuu, suala la Wanafunzi kupinga lingekuwa lina mashiko iwapo katika Watahiniwa wote kama ni 800 basi asipo hata mmoja aliyefauru.

Lakini watahiniwa 800 alafu unakuta kuna wenzio kadhaa 23 wamefauru, hii iwe kama ni alert ⚠️ kwa Watahiniwa kuongeza bidii ya kujifunza wawapo Law School.

Changamoto ninayo iona, kuna uwezekano Wanafunzi wanakuwa busy na utafutaji/ kazi na kukosa muda wa kujisomea.

Nina uhakika zaidi ya 57 hadi 70 ya Wanafunzi wa law school ni in service

Suala la kupinga liko pale pale hata kama ni mmoja tu angefeli isivyo haki.

Una maana hao 23 kumbe ni wa danganya toto siyo?

Kwa nini shule bora ni zenye kufaulisha na walimu Kwa wanafunzi huzawadiwa?

Tuacheni wivu, choyo, husuda, fitna, ujinga, upumbavu na ujuaji uliopitiliza dhidi ya wengine.

Kwamba mkuki kwa nguruwe siyo?
 
Law school ilipaswa ifundishwe na majaji na mahakimu na wanasheria wastaafu sio walimu wa vyuo vikuu.

Mwalimu ambae hana practical experience hasa walimu wetu wa kitanzania ni mwalimu tu. Akili ya walimu wengi kama sio wote inajulikana, ni kutunga mitihani migumu na kuona wanafunzi wanashindwa kufaulu ndio raha na faraja yao.

Walimu wetu wana mentality ya kwamba ukifaulu mitihani migumu basi wewe ni genius ama una akili sana.

Mitihani ya elimu za ulaya ni rahisi sana, sana na bado wana akili na uwezo kuzidi wataalamu wetu. Kama mitihani migumu ingekua ndio ugeniou basi Tanzania ingekua imejaa magenious tupu.

Walimu wa level ya post graduate wanapaswa kua ni wale wenye practical experience na sio hawa wakariri makaratasi wasiojua ulimwengu halisi unaendaje.

Nilisoma postgraduate degree hivi karibuni, yaani walimu wetu ni weupe vichwani balaa, wao wamekariri mi theory ya kizamani isiyo na uhalisia wowote kwenye ulimwengu wa kibiashara ama corporate world lakini wamekomaa wanafunzi wakariri hivyo hivyo. Ukijaribu kuwachallenge wanawaka balaa.

Tunahitaji kufanya reforms kwenye mfumo wetu wa elimu hasa postgraduate level. Haiwezekani kwenye level ya postgraduate watu wafundishwe kwa kukaririshwa ama wakaririshwe, haiwezekani.
 
Elimu na siasa haviendani hata ukiangalia shule tulizosoma wale waliokuwa wanajifanya wana misimamo ya kisiasa mara sijui kutka haki wengi sio wasomi ni janja janja tu na uwizi wa mitihani.

Hamna exception zaidi ya kusoma hili jambo likipelekwa kisiasa sijui walimu wana makosa mara kukata rufaa ni hatari.

kama jamaa hapo juu kasema wengi wapo kweny mifumo hata kazi wanazo ...Aisee hili ni tatizo kubwa sana hawapo active na masomo wao mara kazini mara huku kwa Degree wanatoboa maana kula ubabaishaji wa kiwango cha juu mara kucopy na kupaste assignment ,kufanyiwa research hata kuiba mitihani ya mwisho
 
Hiyo Law School ndio chuo pekee hapa duniani ambacho kinafelisha wanafunzi wengi kisha walimu wake kupongezwa.

Huku wajinga wakiwatetea hao walimu kwamba wanafunzi wa siku hizi ni wavivu, hawapendi kujihangaisha, wanafunzi wale ambao wametokea undergraduate kwa walimu walioridhishwa na ufaulu wao.

Au ndio mnataka kusema walimu wa undergraduate nao ni wajinga kama hao wanafunzi waliofaulu kwao? kwamba walimu wa undergraduate wa sheria nao wakipewa mitihani ya Law School nao watafeli?

Wengine wanasema tatizo ni kule wanafunzi walikotoka, kama kule walikotoka ni tatizo, hao walimu wa Law School kazi yao ni ipi? mbona bado wanafunzi wanafeli wengi hata wakifundishwa nao? kama muda ni mdogo basi uongezwe, lakini sio huu wizi wanaowafanyia wanafunzi.

Pia tuambiwe, kwani hao walimu wa Law School ni malaika walioteremka duniani kutokea sayari ipi? maana inaonekana wanakijua wao pekee kile wanachokifundisha, au ndio walifundishwa mbinguni?!
 
Suala la kupinga like pale pale hata kama ni mmoja tu angefeli isivyo haki.

Una maana hao 23 kumbe ni wa danganya toto siyo?

Kwa nini shule bora ni zenye kufaulisha na walimu Kwa wanafunzi huzawadiwa?

Tuacheni wivu, choyo, husuda, fitna, ujinga, upumbavu na ujuaji uliopitiliza dhidi ya wengine.

Kwamba mkuki kwa nguruwe siyo?
Ninachotaka kusema ni kuwa kwa wale services Man ambao wanakwenda kusoma law school wakiwa kazini ni vyema wakaomba hata likizo kwa waajiri wao ili wapate muda mrefu wa kusoma na kujiandaa.

Sio rahisi kusoma ukitokea kazini (evening program) na ukafauru masomo magumu kama hayo ya shule ya sheria.

Kuna chuo niliwahi kupata nje ya Nchi kwa fani ya Masters Degree in Structural engineering two years Online, nilikataa kusoma.

Siwezi kusoma fani kama hiyo Online, lazima nitafeli. Hivyo kujiepusha kufeli nikaomba ni cancel mpango wa kusoma Mwaka huo.

Point yangu ni kuwa huenda Wanafunzi wanakosa muda wa kujiandaa kutokana na kuwa busy na mambo ya kazi n.k hivyo muda pamoja na Utulivu wanakosa.
 
Elimu na siasa haviendani hata ukiangalia shule tulizosoma wale waliokuwa wanajifanya wana misimamo ya kisiasa mara sijui kutka haki wengi sio wasomi ni janja janja tu na uwizi wa mitihani.

Hamna exception zaidi ya kusoma hili jambo likipelekwa kisiasa sijui walimu wana makosa mara kukata rufaa ni hatari.

kama jamaa hapo juu kasema wengi wapo kweny mifumo hata kazi wanazo ...Aisee hili ni tatizo kubwa sana hawapo active na masomo wao mara kazini mara huku kwa Degree wanatoboa maana kula ubabaishaji wa kiwango cha juu mara kucopy na kupaste assignment ,kufanyiwa research hata kuiba mitihani ya mwisho

Wengi wako kwenye mfumo gani ndugu? Mnazipata wapi takwimu hizi Ili kumpotosha nani?

Zaidi ya 90% ya wanafunzi wote Law School ni fresh from universities.

Tuacheni wivu, choyo, husuda, fitna, ujinga, upumbavu na ujuaji uliopitiliza dhidi ya wengine.
 
Back
Top Bottom