Wanachopaswa kufanya CHADEMA baada ya Tamko la Polisi

sixgates

JF-Expert Member
Mar 19, 2011
3,979
1,662
Toka asubuhi nimeona taarifa za hamasa za kumpokea Tundu Lissu. Ni katika kuhamasisha mipango ya ndani ya CHADEMA kumtengenezea ukubwa Tundu Lissu, lakini nasikitika kusema CHADEMA wamefeli kwanzia planning, na execution ya Jambo la Lissu.

Nitaelezea siku nyingine hapo kwenye planning ila kwa haraka haraka, tayari walishajua kuna msiba wa kiongozi (former President) Mh Mkapa ni tukio zito katika level ya Taifa.

Alikuwa na nyadhifa mbalimbali, Rais, Mwenyekiti wa CCM na pia Amekuwa Amiri Jeshi mkuu. Attention ya taifa ni huko, Lissu anakuja kama mtu ambae anajinadi anataka kuongoza nchi, ile ni nafasi kubwa inabidi ajiweke (act as the one), kama mtu ambae atakuwa baba, mfariji na kiongozi wa wote.

Angekuja bila hyping au mbwembwe aelekee uwanja wa uhuru au nyumbani kwa Hayati Mkapa, ila kwa sababu CHADEMA hawana mipango na wao sio wanasiasa ni wanaharakati wanatafuta mob attention. Hakuna nchi inayoweza kuruhusu hilo. Msiba wa Rais (former), unatambulika kikatiba.

Ninachojua CHADEMA hawashauriki na wanapenda kushupaza shingo ila warudi wajiangalie upya.
 
Yaani mtu kanusurika risasi 17 halafu unasema akifika aende Taifa kwani akienda Taifa ndo Mkapa atafufuka?

Acha Mkapa apumzike Mungu alipomwandalia kutokana na matendo yake wakati yuko hai yeye kama binadamu lakini kwa dhamana akizokuwanazo jinsi alivyozitumikia na Lissu acha arudi akaione familia yake pamoja na wapendwa wake afanye tendo la kumshukuru Mungu kwa kumzawadia uhai kwa mara ya pili
 
Yaani mtu kanusulika risasi 17 alafu unasema akifika aende taifa kwani akienda taifa ndo Mkapa atafufuka?

Kugoma kwenda taifa kwa sababu hatafufuka hiyo ndiyo uanaharakati ndani ya Chadema. Ila pamoja na kwamba kanusurika kuuawa anarudi kama mtu ambae anataka kuwa Rais “siasa” ni kwenda kutoa pole.. unless uniambie Lissu hayupo serious na nafasi ya urais.
 
Kugoma kwenda taifa kwa sababu hatafufuka hiyo ndiyo uanaharakati ndani ya Chadema. Ila pamoja na kwamba kanusurika kuuawa anarudi kama mtu ambae anataka kuwa Rais “siasa” ni kwenda kutoa pole.. unless uniambie Lissu hayupo serious na nafasi ya urais.
Kwenda kutoa pole hakumfanyi kuwa rais akienda kutoa pole anapaswa kufanya kama binadamu sio kama njia ya kuutaka urais sasa lisu apaswa yeye ndo apewe pole na kumshukuru Mungu kwa kupona sio yeye aanze kutoa pole
 
Kugoma kwenda taifa kwa sababu hatafufuka hiyo ndiyo uanaharakati ndani ya Chadema. Ila pamoja na kwamba kanusurika kuuawa anarudi kama mtu ambae anataka kuwa Rais “siasa” ni kwenda kutoa pole.. unless uniambie Lissu hayupo serious na nafasi ya urais.
Sasa urais unahusianaje na kwenda kutoa pole? mbona unataka kumfundisha? kwani umeambiwa haendi!? mbona umeshupalia hio pole kwani akiwa hai alishawahi kulizungumzia suala la lissu kupigwa risasi mchana kweupe!?
 
Aisee..
Niko msibani napitia pitia juu juu tuu nitacoment baadae niko na mabosi zangu sijatulia kabisa gangu asubuhi
 
Lissu aliugua akalazwa Nairobi, LofaBoy hakwenda kumjulia Hali Wala kutoa pole hata tamko la kulaani kitendo alichofanyiwa Lissu!

Ningekuwa Mimi Ni Lissu siyo tu kutokwenda kuombeleza kufa kwa LofaBoy Yani ningetafuta hata wachawi wamuue Mara ya pili.
 
Ushauri mzuri na ni imani yangu chadema bado wapo wachache wenye busara na fujo zao watazifanyia mitandaoni ila airport Lissu atapokelewa kikawaida tu
 
Ujio wa Lissu umekurupua wanafiki wote kudadeki !
Wapumbavu na malofa kwao ni kiki ya kisiasa.

Nasisitiza kuwa kama Lissu angekuwa ni malikitu (asset) kisiasa, wapiga kura wake waliomwingiza bungeni na wanachama wa TLS (Rais wao wakati wa tukio la kushambuliwa) wangehamasishana kumpokea. Ila zumbukuku wa kisiasa wanadhani wamepata kumbe watapatikana.
 
👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👍🏽 Hata pole kwa Lissu sikumsikia atoe kwake binafsi, familia yake au Chadema.

Suala la Lissu kwenda kutoa pole ni suala lake binafsi.
Mbona Mkapa hakwenda kumuona Lissu hospitali wakati alikuwa na uwezo huo hata wa kwenda Ubelgiji?
Lissu ataamua aende uwanja wa taifa,nyumbani kwa Mkapa au Mtwara kwenda kuzika.
 
Back
Top Bottom