Wanachama 12 chadema wafukuzwa!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanachama 12 chadema wafukuzwa!?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Endeleaaa, Mar 26, 2009.

 1. Endeleaaa

  Endeleaaa JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,227
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180
  TBC1 habari kwa ufupi saa kumi wamesema Chadema wamewatimua wanachama 12. Mwenye data za undani zaidi atushushie.
   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Zitto hayumo humo???
  Halisi yupo wapi atuletee ishu sisi tulio mbali
   
 3. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #3
  Mar 26, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Zitto yumo
   
 4. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Haya umeyetoa wapi?

  Kamati Kuu ya chama haikuwa na wala halijatokea wazo la kumjadili Mhe.Zitto kwani ni kiongozi wetu na tunamuhitaji kuliko wakati mwingine wowote .

  Waliofukuzwa ni wale waliokuwa wanajiita wanachama wa DSM , na kati yao wapo ambao wanafanya kazi kwa Guninita na wengine Usalama wa Taifa ambao hawa ni 2 na walifukuzwa baada ya kamati ndogo ya kamati kuu ya Bob Makani kuwatia hatiani kwa kosa la kukiuka maadili ya chama .

  Waliofukuzwa ni waliokuwa wanakihujumu chama na mjumbe mmoja wa kamati kuu yeye kasimamishwa ujumbe wa kamati kuu ila hajafukuzwa uanachama.

  Mjumbe wa kamati kuu aliyesimamishwa ni Mecky Mziray kutoka mkoa wa Pwani na yeye tangu 2005 alikuwa akigombea ubunge chalinze.

  Hawa watu walipewa haki ya kusikilizwa na kamati na waligoma kwenda kujieleza kwenye kamati hiyo.

  Kama chama lazima kiweze kuonyesha njia katika kuchukulia watu hatua za kinidhamu, kwani hata wakichukua serikali basi wataweza kuchukua hatua ipasavyo.
   
 5. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hizi ndio hatari za upinzani kufukuzana kwa haya mauzauza ya ufisadi yanavyokwenda nilitegemea CCM ndio watatimuana,kule CUF wanajiengua wenyewe ,ila sio mbaya ikiwa Chadema wamegundua kuwa ni jamii ya wasaliti ambao hutumiwa katika kupandikiza mtafaruku ndani ya Chama,hongera Chadema hakuna kulaziana damu ni lazima muanze kusafisha ndani ili Chama kiwe kisafi kila siku zikiongezeka,ila inaonyesha bado mpo nyuma katika safu ya usalama wa Chama,zidisheni utamaduni wa kwenda na watu wa aina hiyo mpaka wanajiengua wenyewe kutokana na wao wenyewe kujua kuwa wamejulikana kuwa ni mamluki ila hawajaambiwa rasmi.

  Ila hawa si ajabu ukasikia wanajiunga na Sultani CCM au wanaweza kujiunga na Mrema maana Mrema naona ana usongo na Chadema na ameshatangaza rasmi.
  Kila nikipima vyama vya upinzani naona bado havijatulia kama CUF chama ambacho hakina siasa za vishindo.
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Dogo Dogo usitake watu wasage chupa hapa .....
   
 7. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #7
  Mar 26, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Katika vyama vya upinzani chenye msimamo wa kuweza kushughulikia viongozi wajuu ni CUF ,ikiwa utaonekana kuvuka mipaka utaondolewa na hali ya kuwa unaridhika maana hata makelele yako yataonekana kama kweli ulitaka kukiharibu Chama ,mfano wa juzi tu japo si mtu kitu kwenye Chama kwa maana hajafikia stage ya juu lakini Pro Safari alipoondolewa alisikika akiimba musiki wa bongo fleva kuikanyaga CUf na kweli alizidi kuumbuka ,sasa naona simsikii tena sijui ataibukia wapi ,sidhani kama Chadema wana uwezo wa kuwatimua viongozi wasio kuwa na msimamo au wanaoonekana kukihujumu Chama ,ndio siku ya kugawika mapande.
   
 8. IronBroom

  IronBroom JF-Expert Member

  #8
  Mar 26, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 524
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Chadema yatimua wanachama 15 kwa madai ya utovu wa nidhamu

  Elias Msuya na Tausi Mbowe

  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimewafukuza wanachama 15 kwa tuhuma za kukihujumu chama hicho, lakini kikaeleza kuwa hakuna tofauti yoyote kati ya naibu katibu mkuu, Zitto Kabwe na viongozi wenzake.

  Akitangaza uamuzi wa kamati kuu ya chama hicho iliyokutana jana, katibu mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa alisema kuwa kwa muda mefu watu hao wamekuwa wakizusha tuhuma mbali kwa chama na viongozi wake.

  Dk Slaa, aliyekihusisha kikundi hicho na aliyekuwa makamu mwenyekiti wa Chadema na mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, alisema kilianzishwa mwaka 2005 na aliyekuwa kaimu mwenyekiti wa mkoa wa Dar es Salaam na kwamba kinaonekana kufadhiriwa na watu wa vyama vingine.

  Alisema tangu wakati huo kikundi hicho kilifanya hujuma na kuhamishia ofisi zake eneo la Ndugumbi Magomeni huku Wangwe akiwaunga mkono na kufanyakazi kazi nao huko, lakini uongozi wa Chadema uliamua kufuata taratibu.

  Alisema mwaka 2007 waliitisha mkutano mkuu, lakini siku ya uchaguzi watu hao walifanya vurugu kiasi cha uongozi wa taifa kuingilia kati ili kuepusha vurugu na kumaliza mgogoro. Lakini, Dk Slaa alisema juhudi hizo ilishindikana na kundi hilo likaendelea kumrushia tuhuma mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na kuandika barua iliyomtaka ajiuzulu. Barua hiyo ilisainiwa na watu 15.

  ‘‘Baada ya kupata tuhuma hizo makao makuu walitaka ushahidi, lakini kikundi hicho kilishindwa kutokea na ndipo Septemba 6 mwaka jana, kamati kuu ilikutana na kukubaliana iundwe kamati maalumu ya kuchunguza tuhuma zote walizozitoa,” alisema Dk Slaa.

  Alizitaja tuhuma hizo kuwa ni pamoja na kuwepo kwa ukabila kwenye chama na matumizi mabaya ya fedha kama kukodishwa helkopta wakati wa kampeni za uchaguzi. Pia alisema wamekuwa wakimtuhumu mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuhusika na mauaji ya aliyekuwa makamu mwenyekii wa chama hicho, Chacha Wangwe na kwamba alifanya sherehe nchini Afrika Kusuni.

  Dk Slaa alitaja tuhuma nyingine zilizokuwa zikirushwa na watu hao ni pamoja na madai kwua mwenyekiti hahudhuria vikao, anadharau wanachama na kwamba anaendesha chama kitoto.

  Dk. Slaa alisema kuwa kundi hilo pia lilifanya maandamano kuelekea makao makuu ya chama hicho yaliyo maeneo ya Kinondoni wakati Chadema ikishiriki uchaguzi mdogo wa Tarime.

  ‘Baada ya kamati kuu kupokea taarifa kutoka Kamati ya Bob Makani iliyoundwa kuchunguza tuhuma hizo, ilizijadili na kugundua kuwa tuhuma hizo ni kejeli kwa chama na mwenyekiti," alisema Dk. Slaa kabla ya kutangaza rasmi kuwafukuza wanachama hao.

  "Kitendo cha kuandamana kinaonyesha jinsi watu hawa walivyo wa hatari na kitendo cha kukataa kuhojiwa na kamati ya Bob Makani pia ni kudharau chama.”

  Aliwataja watu hao kuwa ni Martin Abdul Mateleka, Mkwanji Mauld, Bi mkubwa Uwesu, Peter Katuma, Nasr A. Chimko, Hamis B. Msasa, Andallah Kambi, Zubeir Hajj, Kimaro T, Shabu K Salum, Adam Yassin, Said K. Maleja, Mwanahamisi Sadiki na Martin Mung’ong’o, ambaye anatajwa kuwa mratibu mkuu wa hujuma hizo.

  Dk Slaa pia alisema Meck Mziray, ambaye ni mjumbe wa kamati kuu, anadaiwa kutoa siri za chama na hivyo kufuata mkumbo wa watu waliofukuzwa.

  Dk Slaa alisema kamati kuu ilibaini kuwa hoja zilizotolewa na kikundi hicho haziridhishi na hata walipoitwa kutoa ufafanuzi hawakutokea na badala yake walitoa maelezo yao kwa maandishi tu.

  ‘‘Kamati iligundua kuwa tuhuma za kuhusika katika kifo cha Wangwe ni hear say (maneno ya kusikia). Kwanini hawakupeleka polisi jambo hilo? Kwani hata kesi ya msingi iliyokuwa mahakamani haikumtaja Mbowe kuhusika na kifo hicho, hivyo kamati imetupilia mbali tuhuma hizo," alisema.

  ‘‘Kuhusu matumizi mabaya ya ruzuku, kamati ilijiridhisha kuwa matumizi ya bajeti ni lazima yapitishwe na kamati na baraza kuu (CC) na kwamba uamuzi wa kutumia helkopta ni uamuzi wa CC na baraza kuu na baadhi ya walalamikaji hao ni wajumbe wa vyombo hivyo vya juu vya chama hicho.”

  Alisema pia kuwa kamati ilibaini tuhuma za Mbowe kufanya sherehe nchini Afrika Kusini na Msasani jijini Dar es Salaam mara baada ya kupata taarifa ya kifo cha Wangwe zilizushwa na mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho kwa maslahi yake na kwamba tuhuma hizo nazo zilitupwa.

  Kuhusu tuma kuwa Mbowe anagombanisha na kuchochea migogoro ndani ya chama hicho, kuendesha chama kitoto na kwamba hana busara na uvumilivu pia vilitupiliwa mbali na kamati hiyo baada ya kugundua kuwa ni hisia tu, alisema.

  Alisema kamati pia ilishitushwa zaidi wakati Chadema ipo katika mapambano mjini Tarime katika uchaguzi mdogo wa ubunge, lakini kikundi hicho kiliandamana jijini Dar es Salaam kuupinga uongozi wa Mbowe.

  ‘‘Tuligundua kuwa watu saba kati yao walikuwa wa chama kingine," alisema. "Kamati iligundua kuwa watu hao wasingeweza kugharamia mkutano ule hivyo kuhisi kuwa kuna mtu yupo nyuma yao anayedhamani kwani hata uwezo wa kujenga hoja wakati walipoitwa katika kamati kujitetea hawakuwa nao.”

  Alisema katika adhabu hiyo wahusika wamegawanywa kwa makundi mawili ikiwa ni pamoja na viongozi waliojihusisha na mgogoro huo pamoja na walioandika utetezi na waliokataa kuandika wala kutoa maelezo yao ya kujitetea.

  Naye Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amekanusha vikali kuwepo kwa tofauti kati yake na naibu katibu mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe.

  Mbowe, ambaye kwa sasa yuko safarini nchini Uingereza na Hispani, aliyasema hayo alipokuwa akifungua kikao cha baraza kuu la Chadema linalofanyikia jijini Dar es Salaam.

  Alisema kwamba shutuma hizo zimekuwa zikitolewa na watu wasioitakia maendeleo Chadema na akaitaja CCM kuhusika na uzushi huo.

  ‘Taarifa kwamba tuna ugomvi na naibu katibu mkuu wangu, Zitto Kabwe si za kweli hata kidogo. Zitto ni mbunge wetu na ni kiongozi wa chama chetu. Tumemruhusu kwenda kuhudhuria mkutano wa kisiasa nchini Uingereza na Hispania. Huo ni uzushi wa CCM ambao siku zote hawatutakii mema na watabaki hivyo hivyo vichwa chini,” alisema Mbowe.

  Hata hivyo Mbowe alikiri kuwepo kwa tofauti ya misimamo kati yao kwenye suala la ununuzi wa mitambo ya Dowans.

  "Ni kweli kumekuwapo na tofauti za kimawazo, lakini sisi tunaruhusu mawazo mbadala. Kama wote kwenye chama tutakuwa na mawazo sawa, kitakufa. Chadema tunaruhusu mawazo mbadala na hivyo ndivyo chama chetu kinavyokua,” alisema.

  Katibu mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa akizungumzia suala hilo alipinga vikali kuwepo kwa mtafaruku kati yake na Zitto Kabwe.

  "Taarifa za kuwepo kwa tofauti kati yangu na Zitto nazisikia na kuzisoma kwenye vyombo vya habari. Nawashangaa wanaovumisha habari hizo kwanini huwa hawanipigii simu waniulize? Mara utasikia Zitto ameshushwa jukwaani mara Zitto amefukuzwa kwenye Operesheni Sangara, huo wote ni Uzushi mtupu," alisema Dk Slaa.

  Kabla ya kuanza kwa mikutano ya Operesheni Sangara, tulikuwa na Zitto Kabwe Moshi tukiandaa strategic plans (mikakati) kwa ajili ya mikutano hiyo na baadaye akaniaga kuwa anakwenda Uingereza na Hispania,” alisema Dk Slaa.

  Uvumi wa kuwepo mgogoro wa kiungozi katika chama hicho ulizidi kuenea hivi karibuni hasa baada ya Zitto, ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, kuunga mkono ununuzi wa mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura ya Dowans, tofauti na msimamo wa Bunge na viongozi wenzake kwenye chama.

  Source: Mwananchi Read News
   
 9. M

  Mkandara Verified User

  #9
  Mar 26, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Efuuuuh! sasa naweza kupumua maanake yule Kiranja alitaka niamini yasiyoaminika..Zitto of all people kuhamia CUF?...Ama kweli, wahenga walisema - Believe this U will believe anything!
   
Loading...