WanaCCM tusikae kimya, chama kinapoteza sura yake

WanaCCM tusikae kimya, chama kinapoteza sura yake

Nilikuwepo Dodoma kwa mfano wakati mwenyekiti wetu alipojizolea 100% ya kura zote. Wengi walikuwa wakinong'ona pale kwamba mbona hawakumpigia lkn kapata 100%?. Lkn pia kuwekwa ndani kwa Msukuma na Bashe kipindi kile alipojaribu kubadili kanuni za chama kwamba 2020 apite bila kupingwa.

Mkuu mm ni mhenga ndani ya chama. Nadhani tusiwape faida wapinzani. Amini ninayokuambia
Nakubaliana na wewe kuwa wanachama wana haki, na ni wajibu wao, kutoa maoni yao ili kukiboresha chama.

Lakini kusimama jukwaani, bungeni au mitandaoni na kukikashifu chama chako wewe ndie unaewafaidisha wapinzani badala ya kukisaidia chama chako.

Tuuchulie mfano wako wa uchaguzi wa mwenyekiti wa CCM. Waasisi waliuweka huu utaratibu kuwa, atakaechaguliwa na waTZ wengi kuiongoza nchi basi yeye ndie atakaefaa kukiongoza chama wakati akiwa Rais.

Lakini kwa kuwa haya yalikuwa makubaliano ya waasisi na hayakuwa ndani ya katiba ya CCM, chama kilikubaliana kisiibadilishe katiba bali ifahamike kuwa uchaguzi mwenyekiti wa chama utakuwa RUBBER-STAMP tu kwa sababu uchaguzi wenyewe ulifanyika wakati wa kumchagua Rais.

Sasa kama wanachama hawautaki mfumo huu hili hufanyika kabla ya mwenyekiti aliepo madarakani hajamaliza muda wake. Mfano, hivi sasa ingekuwa muda muafaka wa kujadili CCM itampataje mwenyekiti wake mpya baada ya Magufuli kustaafu.

Huwezi kusubiri mpaka siku ya kumchagua mwenyekiti mpya ndipo useme tubadilishe kanuni za chama.

Hii itakuwa ni sawa na siku ya mechi ya world cup nchi moja shiriki iseme jamani tubadilisheni sheria za mchezo. Sasa wachezaji wanaruhusiwa kutumia mikono yao. This will be chaos.
 
Ccm inawanachama wengi siyo wewe tu na wote wananafasi sawa, au kunanafasi ipo wazi? mlizoea ninyi zamu yenu kutembelea meno

Kweli mkuu, ina wanachama zwazwa mengi sana tena sana, na hawa ni wanachama ama mashabiki kwa hiari yao. Ila sema wakipata kujitambua tu basi ndiyo kwa heri. Pia wako wanaojitambua lakini chama kinawaomba na kuwalipa waendele kujifanya mazwazwa kwa manufaa ya chama, hawa wanajitambua lakini wanaweka tumbo mbele kwa kulipwa vijisent, mfano ni kijanamzee, bidhaa mpya kafu..., Kilio cha taifa mleta majina kumi, Lizabuni na wengineo. Hawa hufanya haya kwa maslai ya matumbo yao.
 
Nilikuwepo Dodoma kwa mfano wakati mwenyekiti wetu alipojizolea 100% ya kura zote. Wengi walikuwa wakinong'ona pale kwamba mbona hawakumpigia lkn kapata 100%?. Lkn pia kuwekwa ndani kwa Msukuma na Bashe kipindi kile alipojaribu kubadili kanuni za chama kwamba 2020 apite bila kupingwa.

Mkuu mm ni mhenga ndani ya chama. Nadhani tusiwape faida wapinzani. Amini ninayokuambia

Jamaa yenu apiga ile inaitwa flying kick (Iba kura za wapinzani mpaka wana ccm wenzake, ila huyu si mwenzenu kama hamjui)
 
Udugu, umoja na mshikamano havipo tena ndani ya chama. Chama kimejaa fitina giliba na na uzandiki. Tumekiuka miiko ya chama "Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko". Hivi sasa kinacho hubiriwa tofauti na kile kinachotendeka. Nitawapa mifano mitatu ktk jambo hili.

1. Hivi kwann Mwandosya na Membe watengwe na ccm hadi kufikia wakalalamika? Walifanya kosa gani?

2. Hivi wake wa wabunge wetu maarufu ambao sasa ni narehemu: John Komba na Deo Filikunjombe kwann wanatelekezwa hadi kufikia wanalalamika?

3. Iweje mzee Yusufu Makamba, ingali bado you hai amesahauliwa na chama ktk kipindi hiki...

Kumbukeni nyoka akiingia ndani dawa siyo kuikimbia nyumba bali kumuua nyoka. Kama ANC na ZANU- PF wameweza kwann ccm tusiweze?

Kidumu Chama Cha Mapinduzi
Ua Nyoka, alhamisi 26 April 2018
 
CCM yenye furaha imebaki kanda ya Ziwa tu!
Nimesikia ndotoni...
 
Pia Abdul Rahman Kinana...Hayuko Ofisini tena. Mbadala wake Rodrick Mpogolo, naye si kama Katibu vile!
 
Back
Top Bottom