vibertz
JF-Expert Member
- Mar 15, 2022
- 1,452
- 2,647
Kwanza kabla ya kuanza kutaka point za mezani naomba unieleweshe hapa.Mnakumbuka tulisajiri kipa kutoka America kusini ligi daraja la nne, uto na viongozi wao waliongea sana hatimaye akaenguliwa.
Wenzetu wapo vizuri kwenye kutumia udhaifu wa mpinzani, ila kwetu hatupo hivyo utakuta tunajipa lawama wenyewe kuwa ni uzembe wetu, na sipingi hilo.
Nini namaanisha, ni hili jambo la Yanga kumchezesha mchezaji asiyethibitishwa, mbona TFF hawamtaji na kanuni hazifuatwi.
Tupo baridi na msemaji wetu kujifanya msema ukweli, kuwa timu yetu mbovu, ubovu tulio nao umesababishwa na Simba wenyewe.
Ila hili jambo la Yanga kama hawalioni, ila ingekuwa ndio Simba imefanya hivyo basi hakika tungekoma sana.
Juzi hapa Yanga waliishurutisha Azam media kufuta taarifa za Mayele alizosema Yanga. Unaona kabisa wenzetu hawapo tayari kuchafuliwa hata kidogo ila sisi tupo baridi.
Najua mtakuja kusema mpira ni dakika 90 na ndio zinaongea lakini tukumbuke hiyo nayo ni kanuni, na bila kanuni kila mtu atafanya anachotaka.
Ni mawazo yangu tu.
#Sina Imani na viongozi wa Simba akiwemo Ahmed ally
Ni kwamba kwenye barua ya TFF wamesema kuwa Yanga wamekiuka katika FIFA’s Regulations on the Status and Transfer of Players (“RSTP”)
Na kosa lao ni kutoingiza uthibitisho wa malipo wa mchezaji husika kwenye system (TMS)
Je RSTP ni nini? Sheria yake ipoje?
Je mchezaji asiyekamilishiwa kuingiziwa taarifa ya malipo kwenye RSTP anakuwa ni mchezaji halali au sio mchezaji halali?