Hebu njooni tujadili hili kutoka Simba SC

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
HAJI MANARA ACHA KUVUKA MIPAKA, UMEWAKOSEA SANA WACHEZAJI WA SIMBA.

Na Kulingwe Msafiri
Mwanachama Simba
Matalawe Njombe

Moja kati ya mambo ambayo hunipa furaha sana katika maisha ya ulimwengu huu pamoja na changamoto zote za dunia ni Ushindi wa Simba na Arsenal.Nazipenda timu zote ila Simba naipenda zaidi.

Ni ukweli usiopingika kwamba Timu yetu ya Simba ni kati ya vilabu bora sana katika Afrika ,kwa miaka ya hivi karibuni baada ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na Mohamed Dewji klabu ya Simba imekuwa katika ubora wa kuanzia nje ya uwanja mpaka ndani ya Uwanja.

Kwa aina ya wachezaji waliopo Klabu ya Simba,ni dhahiri shahiri kwamba kila mpenzi na mshabiki wa Simba anategemea matokeo mazuri kwa kila mechi.Ila Simba hii inatupa kitu cha ziada ambacho ni Burudani ya Soka ambalo ni kama la Playstation,hii hasa inatokana na kikosi kukaa muda mrefu na kuelewana.

Wasiwasi wangu ni kuanza kujiaminisha kwamba Timu yetu hii itabaki katika kiwango kile kile kwa mechi zote na kwamba hatustahili droo wala kufungwa.

Wasiwasi zaidi unaongezeka nikiona mtu kama Haji Manara ambaye kimsingi yeye ni Msemaji tu wa Timu anakwenda mbali zaidi kutoa lawama katika mambo ambayo muda mwingine ni ya kiufundi,na hata kama alitaka kutuma huo ujumbe zipo njia sahihi za kufanya hivyo kwasababu na yeye ni sehemu ya Menejimenti badala ya kuandika ujumbe ule kwa umma hali ambayo inaweza kuwaathiri sana kisaikolojia wachezaji wetu ambao tumeshawajengea confidence kubwa kupitia mashabiki.

Manara anapaswa kutambua majukumu yake,haya mengine awaachie wahusika.Kazi ya Msemaji ni kusema baada ya jambo kuchakatwa ili lije kwa matumizi ya Umma.

Manara anajisahau kana kwamba hii ni Timu binafsi na yeye ndio mwenye kuamua cha kusema bila kuangalia athari ya maneno yake katika umoja na mshikamano wa Timu kwa muda huu.Kusema kuna wachezaji hawana sifa kuichezea Simba ni kuikosea pia Kamati nzima iliyofanya scouting ya wachezaji.

Kwa mechi kama ya jana hakuna mchezaji wa kulaumiwa,tumepata matokeo kama sehemu ya mchezo.Tuliwatawala Yanga kipindi cha kwanza,wakarudi na mbinu mpya ambayo ni kuzidiana kwa mbinu za kimchezo.

Goli la Mapinduzi Balama hata ungemleta De Gea na kipa yoyote unayemjua angefungwa tu.Ni goli la kiufundi ambalo hata sisi mashabiki wa Simba tulibaki mdomo wazi.

Aishi huyu huyu ametuokoa sana Ligi ya Mabingwa kwenye kuepuka vipigo vya aibu,leo hatuoni thamani yake na kumlaumu kwa mechi moja?

Ifike wakatai sasa CEO wa Simba achore mstari wa majukumu kila mtu asimame upande wake vinginevyo tutavurugana wenyewe kwa wenyewe wakati bado tuna safari ndefu.

Manara Simba niyetu sote punguza Mdomo kws kutafuta HURUMA na Kujihami kwa Porojo zako za Kibinafsi. Simba ni yetu sote uwe na shukurani.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tukiwambia Manara anawaaribia timu yenu kwa shombo zake mnatuonaga eti tuna wivu, haya sasa mmejionea.
Manara anaingiza mapato na ni lazima ahamasishe.
Hivi jinsi nyinyi mlivyoingia kwa uchache vile bila Manara Pesa ingepatikanaje hapo.
Manara anaujaza uwanja kalibu kila mechi.
Hii ndio kazi yake, kama kushinda gemu shindeni nyie basi.
Watu uwanjani mnaingia chini ya sehemu ya ⅛ ya uwanja halafu mnambeza Manara.
Hivi ile nyomi ya Simba mnaichukulia vipi, inatoka hewani au.
Hongereni na Sare yenu.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Manara njaa kali, ana post ujumbe wa kuwakandia wachezaji wa mikia ikiwa imeambatana na picha ya sauti ya ng'ombe (moo). Huku ni kujikomba

Mikia mlipigwa 2-1, lile lingine ni la refa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Manara ni spika ya Mohamed Dewji, MO pamoja na kujitahidi kuhonga marefa, kumpa Kagere hirizi, bado timu mbovu, hapo MO ana wasiwasi washabiki hawatanunua kadi za simba na kwenda uwanjan hivyo atakosa mapato
Team mbovu inayoongoza ligi na bingwa mtatajiwa kwa miaka 10 ,kumbuka mwaka wa tatu huu ndio safari inakaribia katikati
 
Tukiwambia Manara anawaaribia timu yenu kwa shombo zake mnatuonaga eti tuna wivu, haya sasa mmejionea.
.
kuna mtu mwenge shobo kama yule mpaka mkorogo nugas!?yule jamaa sijui choko yule..anachokiongea hakieleweki,hajui mpira kapania kumcrash manara kwa kila jambo
 
Namshangaa Manara kwa sababu nyingi tu:
1. Hivi baina yake na mchezaji anayetoa damu na jasho lake uwanjani, nani anahitaji zaidi ushindi? Nani anasikitishwa zaidi na hali ile?

2. Anasahu kwamba kabla ya mechi alisema kwamba angepokea matokeo yoyote?

3. Kama ni Kutoka sare, mbona hakuwalaumu wachezaji wakati wa sare dhidi ya Prisons?

4. Kama wao wametoka Sare na Prisons ambayo baadaye ikafungwa na Yanga, hiyo jeuri ya kuamini kwamba wangewafunga Yanga mengi ni kwa mantiki ipi mpaka atahayari walipoambulia sare?

5. Kipi kinauma zaidi baina ya kutoka sare na kufungwa? Mbona hakuwatolea shombo wachezaji haohao walipofungwa na Mwadui ambayo uwekezaji wake ni mdogo zaidi kuliko hata wa Yanga? Au anaamini ni bora kufungwa na Mwadui kuliko kutoka sare na Yanga?

6. Ushabiki wake wa Simba ndio unaomtoa uwezo wa kubaini kauli kadhaa ambazo hata mbumbumbu wa mpira anazijua : football is a cruel game, it is not over until it is over, it is not football if it is predictable n.k.? Hata kama Yanga ingekuwa dhaifu kama hivyo anavoitathmini yeye, udhaifu wake kwa Simba ni zaidi ya ule wa Senegal kwa Mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia Ufaransa ambao walifungwa goli moja? Hakumbuki iliyokuwa Ujerumani Magharibi kufungwa na iliyokuwa Ujerumani Mashariki kwenye Kombe la Dunia? Hakumbuki Simba iliyofika Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika kutolewa na U D Songo? Anakuwaje kiongozi wa mpira asiyakumbuke hayo? Basi umahiri wake uko wapi?

7. Anapowalaumu wachezaji kwa kumwangusha tajiri, ametumwa na huyo tajiri? Ina maana viongozi, washabiki, wanachama na wadau wote wa Simba hawakuumizwa na sare ile isipokuwa tajiri tu? Tajiri ana hisa za asilimia ngapi na wanachama wana ngapi hata wa kusikitikiwa kwanza awe tajiri? Hizi fikra za kitumwa kazitoa wapi?

8. Timu gani duniani isiyofungwa na mtani wake au isiyotoka sare nayo? La ajabu lipi mpaka iwe nongwa kutoka sare hadi atafutwe wa kutolewa kafara?

Ninachokihisi ni kuwa anatafuta pa kutokea baada ya kauli na viapo vyake kwamba ‘ombaomba’, ‘gongowazi’ na majina yote ya ajabu ‘watakula bao za kutosha’ zimemgeuka. Matokeo yake? ‘Gongowazi’ wamamgeuza yeye kuwa ‘Bumbuwazi’!
 
Manara ni mbumbumbu kiongozi , alichokifanya manara ni kuwaweka wachezaji katika presha kubwa, Maana yake Simba haistaili kufungwa wala kutoa Sare kitu ambacho hakipo. Manara ana tafuta pa kutokea baada ya kuwzkejeli wapinzani wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom