DOKEZO Wana Rorya tunamuomba, Rais Samia aturudishie Utegi Farm

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

WrestlerRSF254

JF-Expert Member
Jan 30, 2023
1,199
2,003
Habari wazalendo wenzangu! Hope mu wazima wa afya!

Katika halmashauri ya Wilaya ya Rorya, kuna eneo lilokuwa likitumika na Utegi Dairy kipindi cha wakoloni sijui.

Nimezaliwa miaka ya 80, kiwanda kile kilikuwa hakitumiki mifugo ila walikwepo wachache, walikamuwa maziwa na kwenda kuuza Tarime na Sirari sijui na Migori Kenya huko.

Awamu ya mwisho ya Kikwete, lile eneo la Utegi Farm ilirudishwa kwenye mikono ya raia, kwamba wale raia waliopisha Utegi Farm warudi kwenye mashamba yao since hawakulipwa chochote enzi hizo.

Baadaye uongozi wa Kikwete mwishoni, uliamua kubadilisha matumizi ya eneo lile ya Utegi Farm, na lengo sasa iwe kiwanda cha sukari, eneo lile lilimwe miwa kushirikiana na wawekezeja kutoka China

Mara baada ya kuingia Magufuli mtu wa visasi, akapeleka jeshi eneo lile la Utegi Farm, kwamba kulikuwa na upigaji pale, mifugo iliyobaki yakawekwa chini ya Jeshi JWTZ, na matrekta yalioletwa yote yakawa chini ya jeshi.

Raia tukaamini kweli mafisadi waliofisadi, Utegi dtairy hadi ikafa, matrekta na mifugo basi ndio mwisho wao na watulipe mali zetu walizofuja but up to leo nothing!

Cha ajabu, wananchi waishio vijiji vya Nyanduga, Ingri Chini, Nyasoro, Ingri Juu, Mika, Kowaki, nk, hawana ardhi ya kufanyia shughuli zao za kilimo. Serikali iliwaruhusu warudi kwenye maeneo ndani ya Utegi Farm but alipofika Magufuli alipeleka jeshi kuwafurusha tena.

Leo hii jeshi limekuwa kero kwa raia waishio maeneo ya vijiji hivyo vinavyo zunguka Utegi, ombi letu kama raia wanaoteseka turuhusiwe kurudi utegi farm kuendelea na shughuli zetu za kilimo na kuishi.

Leo hii, wanatishia raia, wanaweka bicon zao ndani ya vijiji hivyo na wameingia ndani ya miji ya watu, yaani ni usumbufu kwakweli, wana utegi tunaomba JWTZ itoke Utegi Farm na kama wanakuwepo basi raia wasisumbuliwe waachwe wafanye shughuli zao za kilimo ndani ya Utegi Farm.

Tunawaomba Baraza la Madiwani ndani ya Wilaya ya Rorya, Mbunge wetu wa Rorya, Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Waziri anayehusika na Rais wa JMT Mama yetu mpendwa Samia Suluhu Hassan msikilize kilio chetu sisi wana Utegi, tumechoka kuangaishwa na jeshi.

Tunamuomba Rais wetu mpendwa Samia atutazame kwa jina la kipekee sisi wapiga kura wake wana Utegi, Lakairo, namba tatu na wengine jamani mko kimya sisi wanyonge wa Utegi tutasaidiwa na nani?

Hatupingi uwepo wa JWTZ Utegi bali tunapinga usumbufu, bikon tunazowekewa hadi majumbani kwetu, yanamanisha nini? Mbunge yuko kimya kama vile hajui, Madiwani kimya kama vile hawajui, wana utegi tutaenda kulima wapi?

Tunahitaji Utegi Farm irudishwe kwenye mikono ya raia, ili tuendelee na shughuli zetu za kilimo pamoja na watu kurudi kuishi kwenye maeneo yao, toka watu walipo hamishwa kwa nguvu kutoka utegi farm hatujawai nufaika na chochote kile.

Tunaomba Utegi Farm irudi kwetu, tumekuwa wengi tumezaliana maeneo yaliyopimwa enzi hizo za 70 kwa 70 haitoshi kuishi sisi, watoto wetu na wajukuu zetu, mtuachie Utegi Farm!
 
Rais Magufuli alikuwa dikteta aliyefanikiwa kuumiza roho za raia wengi sana na hata kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi wa kawaida, huku akijidai kuwatetea wanyonge na kumtangulza Mungu. Mnafiq mkubwa! Mungu anamuona huko aliko.
 
Ila na nyie wajaruo wa rorya mmezidi kuwa wavivu na walalamishi sana hapo utegi Farm hata mkiachiwa lile shamba liwe lenu hamtaweza kuliendeleza na badala yake mtaingia kwenye migogoro mikubwa na familia ya mzee Igogo ni bora libaki kwa gavament na Jwtz
 
Back
Top Bottom