Wana MMU tushirikiane kuboresha Jukwaa letu

Wana MMU tushirikiane kuboresha Jukwaa letu

Status
Not open for further replies.
Mimi nimeifurahia mada hii kiukweli jukwaa hili limefika pasipo.naamini tunaweza kubadilika
 
Rocky mie nashukuru kwa jitihada zako, na nakubaliana na hoja uliyotoa na zilizotolewa na wengi hapo nyuma.

Kuna tatizo kubwa pia ambalo mie nime observe, naona kama vile tatizo lingine kubwa ni unafiki pia. Kuwa sababu nimezoeana na Rocky (bila kujalisha ni jamvini ama nje ya jamvi) basi siwezi kumkosoa hata kama nimeona kakosea. Hilo kwa kweli nalo ni tatizo…

Kuna wadau wengine hata si waku post sana ila ni wasomaji, na katika usomaji wao hujenga trust katika michango ya baadhi ya members. Hivyo anapo ona huyo mtu ambaye yeye kajenga trust kwake anaunga mkono kitu ambacho kinachukuliwa nje ya maadili basi hata yeye follower inakuwa rahisi kwake kuamini ama kufanya hicho kitu.

Majukwaa ya MMU/CC ndio majukwaa hapa Jf yanayo ongoza kwa members kupendana na kushikamana, inaweza kuwa si wote ila ndio hivyo ikifuatiwa na Jukwaa la Tech and Gadgets and Education. Kupendana kwetu na urafiki wetu usitufanye kufumbia macho ama kuchekea kitu ambavyo kimsingi hata wewe unae unga mkono unaona si sawa, ama waona basi ni kheri usichangie kabisa kuliko kuenda tofauti. Hilo suala halijengi.

Tatizo lingine ambalo nalo halijengi ni tabia ya wadau baadhi ambao wapo karibu (bila kujalisha ni jamvini or not) kuleta habari zao private (Za PM na maisha ya nje ya mtandao) hapa kwa malengo ya kulipuana. Hilo ni suala baya… Ni wengi ambao inaweza tokea kukwazana wa wetu wa karibu but ni kheri mkaongea pembeni na mkamaliza tofauti kuliko kwa njia ya kuanikana. Si nzuri kabisa maana inatokoa tu faida kwa wengine wengi na pia kukusesha raha baadhi kuendelea kushiriki hapa Jamvini na kuwafanya wengine hata kubadili ID. Ubaya wa hili inaongeza hata makundi katika majukwaa... Unakuta huyu is for this member, yule for that member... Na kuweka mazingira hata kama member anakosea sababu tu you consider yupo upande wako basi unashindwa kumkosoa.

Naamini kabisa kama members... Hizo suggestions ulizotoa tukizizingatia na wote tukacheza nafasi zetu Jukwaa litakuwa bora na kuwa vile tutakavyo. Na wengi tutajifunza na kuelimishana pia.

Naona watu wengi wa kuwa CC Umejitahidi kukumbuka. Naomba niongeze hawa ;

BelindaJacob, Zion Daughter, Azimio Jipya, gfsonwin Elia, figganigga, Gaga, Globu, Matola, jouneGwalu, kinyoba, Keren_Happuch, klorokwini, ndyoko, kivuma, lara 1 , Madabwada, MadameX, MAMMAMIA, Mamzalendo, Manyanza, Mbu, Manumbu, Speaker, PetCash, queenkami, Ndahani,

Asante sana mtoa mada na pia Asha Dii kwa mchango wako tutajitahidi kadri tuwezavyo kurudisha hadhi ya hili jukwaa.
 
ushauri 2,nadhan kabla ya kuweka mada husika ni bora kujadili mada nje ya jukwaa,nikimanisha kama kuna watu wanaweza kujadili ktk whatsapp mnaweka kundi la members halafu mnajadilr mkirudi kwny jukwaa mnatabayanisha kile mlicho jadili!naomba mlifikirie hili.
 
Kuna maada zingne hazna maana itabidi mods wetu waangalie hili sasa hvi kuna watoto wameibuka wanapost thread zisizo na maana. Yaan inakuwa ni utoto mtupu inafikia hatua hili jukwaa linaoneakana la watoto
 
Kuna maada zingne hazna maana itabidi mods wetu waangalie hili sasa hvi kuna watoto wameibuka wanapost thread zisizo na maana. Yaan inakuwa ni utoto mtupu inafikia hatua hili jukwaa linaoneakana la watoto

kweli mgirik
 
ni kweli unajuwa watu tunapishana upeo akil hekima na busara wapo wengi kwa kuwa tu wana smart phones wanajuwa kuandika na wanaweza kufunguwa massage wanajb jb tu bila hata kuelewa ndy shida inapoanzia cha msingi hapa yabidi tushirikiane kujenga jamii yetu kwa ustadi mkubwa ni aibu sana kwa watu wazima kuandika ovyo mi nashauri tuwafungie tu maana hawatufai tena
 
ni kweli unajuwa watu tunapishana upeo akil hekima na busara wapo wengi kwa kuwa tu wana smart phones wanajuwa kuandika na wanaweza kufunguwa massage wanajb jb tu bila hata kuelewa ndy shida inapoanzia cha msingi hapa yabidi tushirikiane kujenga jamii yetu kwa ustadi mkubwa ni aibu sana kwa watu wazima kuandika ovyo mi nashauri tuwafungie tu maana hawatufai tena

hovyo...
 
Tngu huu uzi umewekwa hapa naona kama jukwaa linazidi kudorora tu .....!!!!!!!!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom