Wana MMU kwanini mtu akianzisha thread mnamuita mtoto?

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,273
Reaction score
25,303
Habarini wakuu,

Mimi nimekuwa msomaji wa thread zenu mnazokuwa mnazianzisha, pia nimekuwa nikielimishwa na wakati mwingine kuburudishwa.Ila kuna tabia ambayo imeanzishwa kwa baadhi ya member ambayo imekuwa ikinikera, tabia hiyo ni ya kumdharau member anayeanzisha thread na kumuita mtoto mara kasome kwanza, acha utoto na mengineyo.

Hii imekuwa ikiwakatisha tamaa member ambao wamekuwa wakianzisha thread kwa lengo la kupata msaada fulani au ushauri. Ila na nyie member ambao mmekuwa na tabia ya kuanzisha threa zisizo na maana muache ili msiitwe hayo majina. Nawashauri muanzishe hoja zenye nguvu ili mpate ushauri mzuri na sio kejeli kama hizo mnazoitwa na baadhi ya member.

NB: Jamiiforums ni ya watu wote tupendane wakuu

Nawasilisha

By Donatila
 
Donatila

ukikua utajua utoto ukoje, na unavyokera. amini nakuambia, watoto wanaojaribu kujifanya watu wazima na wao wanadhani hawajulikani kama ni watoto wanakera kweli!!! natamani siku moja ianzishwe JF toto point liwe jukwaa maaalum la watoto.
 
Last edited by a moderator:
unajuwa mkuu mtoa mada kinachomfanya mtu aonekane mtoto ni mada ambayo anaiandika. mara nyingi sio rahisi kwa mtu mzima anayejitambua kuandika mada zisizo na mashiko ndiyo hilo huwafanya wajulikane mara moja kuwa watoto
 
Kauliza alafu akajijibu mwenyewe kua hua wanaanzisha mada ambazo hazina maana
 
Mimi sio mtoto mkuu ila msiwe na dharau hivyo Jf ni ya watu wote msijifanye kuwa nyie ndio mnahaki ya kushauri au kutoa hoja peke yenu.
 
unajuwa mkuu mtoa mada kinachomfanya mtu aonekane mtoto ni mada ambayo anaiandika. mara nyingi sio rahisi kwa mtu mzima anayejitambua kuandika mada zisizo na mashiko ndiyo hilo huwafanya wajulikane mara moja kuwa watoto

Asante mkuu kwa kuchangia, hivyo tuwaelimishe namna ya kuanzisha thread tusiwadharau
 
Donatila

ukikua utajua utoto ukoje, na unavyokera. amini nakuambia, watoto wanaojaribu kujifanya watu wazima na wao wanadhani hawajulikani kama ni watoto wanakera kweli!!! natamani siku moja ianzishwe JF toto point liwe jukwaa maaalum la watoto.

Mkuu acha dharau mimi sio mtoto wewe na Jf sio yako peke yako ipo kwa ajili ya watu wote
 
wenye tabia hizo waache mara moja. kuna baadhi yetu ni junior members na pia tunatofautiana kiwango cha elimu. sio vzr kumdharau mtoa mada kwa hoja au elimu yake. wenye tabia hizo za dharau tuache mara 1.
 
Habarini wakuu,

Mimi nimekuwa msomaji wa thread zenu mnazokuwa mnazianzisha, pia nimekuwa nikielimishwa na wakati mwingine kuburudishwa.Ila kuna tabia ambayo imeanzishwa kwa baadhi ya member ambayo imekuwa ikinikera, tabia hiyo ni ya kumdharau member anayeanzisha thread na kumuita mtoto mara kasome kwanza, acha utoto na mengineyo.

Hii imekuwa ikiwakatisha tamaa member ambao wamekuwa wakianzisha thread kwa lengo la kupata msaada fulani au ushauri. Ila na nyie member ambao mmekuwa na tabia ya kuanzisha threa zisizo na maana muache ili msiitwe hayo majina. Nawashauri muanzishe hoja zenye nguvu ili mpate ushauri mzuri na sio kejeli kama hizo mnazoitwa na baadhi ya member.

NB: Jamiiforums ni ya watu wote tupendane wakuu

Nawasilisha

By Donatila

sasa jibu unalo hapo unauliza nini?!! ACHA UTOTO WEWEE
 
Khaa!! Kama unaleta ishu za kitoto utaambiwa mtoto tu hakuna jina jingine zuri
 
Sasa lets say mtu anauliza eti,kuna mkaka amamtaka,afu muda huo huo anasema ni mke wa mtu.kama sio utoto huo ni nini?
 
Hata mtu mzima au aliyekomaa kiakili hawezi kumdharau mtu asiyemjua ukiona mtu ameandika hovyo usikoment ili nawe uonekane umekomaa kiakili. USIJEFIKIRI UNAANDIKA POINT KWA KUMWITA MWENZAKO MTOTO NA UMEISOMA THREAD YAKE.
 
Back
Top Bottom