Wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii. CHADEMA wana macho? Je, wawasamehe Wabunge 19 wabarikiwe, au wakomae nao walaaniwe?


Bonafide Genuine. Umenikumbusha enzi za kesi ya Rwakatale na ile video yake.
 

Hakuna sarakasi. Ni kiburi Cha spika wa bunge kuanzia ndugau na huyu kilaza wa Sasa hivi.
 
Kaka pascal,tunajuheshimu Sana Tena Sana.
Ila kwa Sasa hoja zako zina walakini.
Tayari wewe rangi yako inajulikana,Mara mia ungeendelea kujifanya uko neutral.
Mda mwingine usomi wenu inafikia kuonekana hopless kwa wengi waliokuwa na matumaini nanyi.
Kinachowaharibia kaka,ni uchawa,kujipendekeza,kuhitaji huruma kutoka kwa mwenyekiti WA CCM,Njaa,undumilakuwili,hamsimamii misimamo ya HakiπŸ€”.
Ila kikubwa mnaangalia maslahi yenu Kwanza na sio maslahi ya Taifa.
Mpaka mda huu wewe,usiwe unatuletea mabandiko yahusuyo siasa kana kwamba wewe upo pembeni.

We jikite katika kujenga Chama chako na mabandiko yahusu chama chako kikongwe.
Mbona hujawahi tuletea bandiko lonalohusu Utawala WA CCM tangu uhuru mpaka Leo hii matatizo lukuki mpaka Nchi inakuwa maskini irihali Ina raslimali kedekede.
Kazi jusifiana kwa kutegemew teuzi.

Labda Kama kaka nimesahau,shusha Bandiko ulilowahi leta humu la kusisitiza Katiba mpya ipatikane iwe isiwe ikiwa na maana kuwa mwenendo WA kuongoza Nchi ya Sasa yenye wakazi millions 59+

Au ndo ile NYANI haoni kundule😳😳.
Tafadhaki kaka,watanzania WA Leo sio wale wa mwaka 1950.

Mnatukosea Sana wasomi WA Nchi hii mlio katika CCM.
Huu ndo ukweli,
Magufuri mlimsifu Sana,lakini mkasahau kuwa ni zao la Ccm.Tatizo la Nchi hii ni Katiba iliyopo haiendani na Ulimwengu wa Sasa.

CCM inaharibu Nchi hii kwa kukumbatia mfumo mbovu,wenye harufu ya kurithishana.
Usijaribu kushauri vyama vya siasa vikubwa Kama Chadema,ACT Wazalendo.kavishauri vile vya CCM B.

Uchaguzi WA 2020 Kuna chochote ulichokisema kweli,au ndo mabandiko ya kusifu na kuabudu😭.
Kaka X mas njema tu.
 
Mayalla huyu ninayemfahamu mimi, mimi siku zote humtofautisha Paskali na Chadema na analijua hilo kupitia Posti zangu, bahati nzuru leo ndiyo mara yako ya kwanza kuniona.
 
Paskali, nyie ni watu wawili na Chadema ni zaidi ya nyie watu wawili ni taasisi hivyo sijui mtatumia miujiza gani kuiangisha! Pamoja na kazi na jasho hulipa lakini kwa hili nasema hapana, angalia Post zako tangu 2013 labda na nyuma umekuwa ukisema Chadema imekufa in wishes lakini machoni Chadema ipo na ni ileile, ila najiuliza mathlani leo ikifa furaha yenu ni kuona wafuasi wake wamekosa haki yao ya kupenda wakipendacho? Ni wachawi tu watafurahia hilo.
 
nashauri wakomae nao walaniewe
 
Ukisoma comments za wadau utaona kwamba zaidi ya asilimia 90 wanapinga ulichokiandika. Maana yake ni kwamba hoja zako hazina relevance yoyote, hivyo unatakiwa kubadilika. Watu si wajinga tena wa kulishwa propaganda zako.
 
Elimu maana yake ni nini? Serikali ilisema haina haja(nia) yakuendelea na kesi. wote tulifuatilia ushahidi wa ugaidi ambao ni kukata miti,kuweka magogo,kutuma pesa kwenye simu na mashahidi ambao hata shule waliyosoma hawamjui mwalimu mkuu au hata calassmate mmoja. unaposema Mbowe kasamehewa unajisikiliza? Bibilia uliyoinukuu inasema aombaye atapewa,atafutaye atapata na abishaye hodi atafunguliwa. waache kina mdee waone haja ya kuomba msamaha kama wanakubali wamekosea. so andiko linge kaa hivi Halima ombeni msamaha.
 
Ni kweli maana naona kama anawabeba mgongoni kiaina na hataki kuona walichokifanya, bali anaona tu Chadema wanachotakiwa kufanya kuhusiana na hao 19.
Mkuu Telesphore Magobe T, mimi niko very honest, najihesabu ni mtetezi huru wa haki, na hata kama ni wakosefu wanaostahili kuhukumiwa kufukuzwa, basi wahukumiwe kwa haki, kama ni kufukuzwa wafukuzwe kwa haki.

Sii wengi humu wanaijua na wameisoma w
katiba ya Chadema, mimi naijua katiba ya Chadema nimeisoma kinyume nyume!.

Nimeamua kujitokeza wazi sio ili kuingilia mambo ya ndani ya Chadema bali kujiridhisha kuwa katika fukuza fukuza hii ya hawa 19, jee haki imetendeka?, wanachama wale wamehukumiwa na haki kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni za Katiba ya CHADEMA?.

Mamlaka binafsi ya kuingilia mambo ya ndani ya CHADEMA, ni kwa mujibu wa katiba nchi, kipengele cha uhuru wa kutoa maoni na haki ya kiraia kwa "public bodies" ambapo japo CHADEMA ni taasisi huru yenye mamlaka kamili ya kujifanyia mambo yake yenyewe, CHADEMA pia ni taasisi ya umma, public party, inayo gharimiwa na fedha za umma, public money, ambazo ni kodi yetu hivyo "the public has the right to know its public as well as its private conduct!".

Swali la kwanza la kujiuliza ni
  1. Kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, ili kumvua mtu uanachama kuna mlolongo wa kanuni na taratibu za kufuatwa na miongoni mwake ni hizi nitakazo ziorodhesha hapa chini, jee zilifuatwa?.
  2. Kuandaa Hati ya Mashtaka kwa maandishi yenye tuhuma zote ambazo mtuhumiwa anakabiliwa nazo. Jee hati hizi za mashitaka kimaandishi ziliandaliwa?.
  3. Hati hiyo ya mashitaki kimaandishi inatakiwa ikabidhiwa kwa mtuhumiwa kwa "despatch" ili kuthibitisha imemfikia, jee hili lilifanyika?, nimesikia kuna watu waliitwa kwa simu, kuna watu waliitwa kwa WhatsApp na barua zimetumwa kwa WhatsApp jee huu ndio utaratibu kwa jambo zito kama hili?.
  4. Mtuhumiwa atatakiwa kuzijibu tuhuma za mashitaka hayo ndani ya kipindi cha siku 14 tangu tarehe aliyopokea barua ile ili apate muda wa kutosha kutafakari, jee hili lilifanyika?.
  5. Baada ya majibu ya hati ile ya mashitaka kurejeshwa, ndipo mamlaka ya nidhamu ingepaswa kuitisha kikao rasmi kwa mujibu wa katiba na kumwalika mtuhumiwa kwa barua ili kumpa nafasi ya kujieleza na kumsikiliza kabla ya kufikia maamuzi!. Jee kwenye huo uamuzi uliotangazwa jana na Bavicha, Jee sheria, taratibu na kanuni zilifuatwa?!.
  6. Kanuni ya kwanza ya haki ni "no body is condemned unheard!". Yaani hakuna yoyote atakayehukumiwa bila kusikilizwa!. Wameitwa kienyeji enyeji, wakagoma wamehukumiwa in "absentia" bila kusikikizwa, hii ni haki?.
  7. Nawasisitiza Chadema kutenda haki ili pia kuepuka hukumu ya kitu kinachoitwa karma isije kuwakumba kwa siku za usoni. Ukiwatendea watu uovu au ubaya kwa kuwaonea, bakora za karma ya uovu ule zitakuja kuitandika Chadema siku zijazo.
Wito faraja kwa wadhulumiwa wote wanaonyanyaswa na kudharauliwa kwa ajili ya kupigania haki yao ndani ya Chadema hadi kufukuzwa kama mbwa!. Kama nyinyi ni watu wa haki, msihofu na kutimuliwa Chadema, Mungu yupo na ni mkubwa zaidi ya Chadema. Mungu atawasinamia na kokote muendako atawainua na kuwalipia, itakuwa ni story ya ," jiwe walilolikataa waashi litafanywa kuwa jiwe Kuu la pembeni", mnaweza kuinuliwa hadi Chadema kuja kuwapigia magoti huko mbele ya safari.

Ushauri huu lengo lake ni kutuaminisha sisi Watanzania wengine tusio wanachama wa CHADEMA, kuwa Chadema ni chama cha haki na kinafanya maamuzi yake kwa haki kufuata misingi ya sheria, taratibu na kanuni za haki, hivyo kutupa matumaini kuwa CHADEMA inaweza kuaminiwa na kukabidhiwa nchi mwaka 2025!, vinginevyo kwa mambo haya kama yalivyo sasa, na kama CHADEMA haitabadilika, then kwa 2025 CHADEMA itakuwa bado haijakomaa kiasi cha kutosha kuaminika na kukabidhiwa nchi!, hivyo 2025 ni CCM tena.!.
P
 
Ukisoma comments za wadau utaona kwamba zaidi ya asilimia 90 wanapinga ulichokiandika. Maana yake ni kwamba hoja zako hazina relevance yoyote, hivyo unatakiwa kubadilika. Watu si wajinga tena wa kulishwa propaganda zako.
Mkuu malantu , umeisha wahi kukisikia kitabu kinaitwa "An Enemy of the People " kilichoandikwa na Hendrix Ibsen?
P
 
Umemaliza yote mkuu.
 
Tujaribu kutafiti chuki za Paskali dhidi ya Chadema zilianza nini na nini ilikuwa chanzo na hasa dhidi ya Mbowe jambo ambalo yeye halifichi, binafsi ninaamini Mbowe akitoka Chadema Paskali atazaliwa upya, roho yake itakuwa huru.
Mkuu Hismastersvoice , I don't know how old you are, ila uliwahi kusikia kipindi kinaitwa Kiti Moto?, na kilikuwa kinaendeshewa wapi?.
Kwa kukusaidia wewe na wengine, kipindi cha Kiti Moto, kilikuwa kinaendeshewa Kilimanjaro hotel na Club Billicanas, mimi wakati naoa vikao vyangu, harusi yangu tumeendeshea Club Billicanas na ukumbi ni Freeman Mbowe ametupa bure!.

Hivyo Mbowe ni rafiki yangu mkubwa na tumetoka nae mbali toka enzi za Mbowe Hotels hivyo sina chuki yoyote na Mbowe, kosa langu kubwa ni kupenda haki, kosa kubwa la Chadema ni kutotenda haki.

Unaweza kuniangalia nilizungumza na Mbowe usikilize kwa makini nimesema nini kuhusu mimi na Freeman
View: https://youtu.be/fxDX_gkCE1E?si=kXh5FLNJxYynqi_gPasco
 
CHADEMA WANAFANYA MAMBO YA KITOTO SANA....

WENZAO WANAGROUM CHIPUKIZI WAO WAMEKAZANA NA AKINA BIBI MDEE

SHENZIIIIIIII KABISA
Shenzi mwenyewe. Hao wanagroum chipukizi wanavunja sheria unataka Chadema nao waingie kwenye huo ushenzi wa kutokuheshimu sheria za nchi. Hao akina Halima walishavuliwa uanachama kitambo hao ni wanaccm. S
 
Maneno kuntu kabisa haya kwa Pascal.
 
Kupenda HAKI......ni kichaa pekee atakuelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…