Wana Kigoma embu jengeni kwenu

Wana Kigoma embu jengeni kwenu

kagera wanaishi maisha ya kizamani sana..hakuna mgeni anaweza kwenda akafungua hata biashara ya maana...utabaki na duka lako nobody bother to come n buy anything!wazawa tu ndio wanaweza
Wabinafsi mno, huo ukurutu sijui utawatoka lini? wakifika miji ya watu wanaendeleza Ubinafsi, ni hatari sana.
 
Kigoma ni sehemu nzuri kwa kuishi na kuwekeza,lakini serkali imetelekeza mkoa ule kwa muda mrefu,kwahiyo wananchi wote wenye uwezo na fikra chanya za maendeleo waliamua kuhama na kwenda kuishi sehemu zenye huduma zote za msingi..

Mfanyabiashara makini hawezi kukaa sehemu haina barabara,haina umeme,haina ndege,.

Watu wa kigoma ni wachapa kazi haswaa ila kazi zao haziwafikishi popote sababu serikali haijawekeza vizuri kwenye miundombinu hasa barabara za kuingia na kutoka kigoma.


Kigoma inahitaji vitu vifuatavyo ili iende mbele

1.meli angalau mbili za mizigo na abilia kwa ajili ya DRC na Burundi.

2.Barabara ya lami Kigoma-mpanda.

3.barabara ya lami kigoma-tabora

4.barabara ya lami kigoma-shinyanga
5.barabara ya lami kigoma-kagera

6.barabara ya lami kigoma-burundi

7.usafiri wa ndege wa uhakika

8.umeme wa uhakika.

Hiyo miundo mbinu itasaidia sana.
 
Wabinafsi mno, huo ukurutu sijui utawatoka lini? wakifika miji ya watu wanaendeleza Ubinafsi, ni hatari sana.
Hatuna ubinafsi!smtyms wa mikoa mimgin wanajifeel inferior na kujitenga!hilo nimeliona many of the times
Na smtms cc tunapendana sana htbkm mtu hmjui vzr,hch kinawakera wngn wntk tuchukiane km wngn
 
Hatuna ubinafsi!smtyms wa mikoa mimgin wanajifeel inferior na kujitenga!hilo nimeliona many of the times
Na smtms cc tunapendana sana htbkm mtu hmjui vzr,hch kinawakera wngn wntk tuchukiane km wngn
Umeandika vitu gani?maandishi yako hayahitaji uchawi kujua umri wako
 
Ukifika Kigoma ni mji uliokauka sana kimaendeleo japo imepakana na nchi zaidi ya mbili. Mbaya zaidi harufu ya kule ni harufu ya kichawichawi. Wenyeji wa huko wamelogezewa ubishi wa kijingajinga tu.

Jamani wanakigoma jengini kwenu, embu igeni mfano wa watu wa Kaskazini kama wa Kilimanjaro, Arusha na atlist Tanga.

Yani hadi wapemba na waunguja wamewazidi kimaendeleo na huku wako visiwani. Acheni hizo bana jengeni kwenu.

Futeni hiyo sifa ya kijinga mnayojisifia ya uchawi. Mkiendekeza mtaendelea kuwa masikini hadi sana.

Tanga watoe, kama kuna mabadiliko labda yameanza jan

 
ila kigoma ni pabaya jamani hata mi nikishaenda kikazi...hamna maendeleo kabisaa.
ukienda wajua tu wewe ni mgeni sio wakule na wanashangaa kabisa.
Yan mi hapo ndio huwa nnawaona wale watu ni wa ajabu yani ni kawaida yao c unajua mchawi akiona mgeni lazma anajihami akuwangie kwanza ili ajue una kinga gani ili usije ukawa unamzidi nguvu madawa yake yasije yakamrudi akafa yeye mwenyewe yaani mwambao wote wa ziwa tanganyika maisha yao ni ndagu tu
 
Mkuu niliwahi fika mwanza mbona hawako vibaya Sana nilikaa siku 8 tuu nikageuza au Uko ndani ndani ndo balaa nini?
Nadhani alimaanisha kipato cha jumla kimkoa ugawanye kwa mamilioni ya wanamwanza
 
Kigoma palinipatia way forward ya maisha. Asante wakimbizi.

Kwa wageni ni kuchuma na kuondoka si pa kukaa kabisa.
 
Hatuna ubinafsi!smtyms wa mikoa mimgin wanajifeel inferior na kujitenga!hilo nimeliona many of the times
Na smtms cc tunapendana sana htbkm mtu hmjui vzr,hch kinawakera wngn wntk tuchukiane km wngn
Wacha kuleta maandishi ya kigoma huku au unataka uanze kubishana kama kawaida yenu
 
Ni ukweli uliobayana kwamba mkoa wa Kigoma uko nyuma kimaendeleo ukilinganisha na baadhi ya mikoa ya Jamhuri hii. Maendeleo ya eneo lolote lile hutegemea juhudi binafsi za wazawa ambao wanaamua kwa dhati kufanya mabadiliko ya kifikra kuendana na wakati. Serikali ambayo ndio mdau mkuu wa maendeleo, mchango wake huonekana pale ambapo watu wenye mkoa wao wameanza kuwa na mwelekeo wa kuyasaka maendeleo.

Tangu uhuru Waha ambao ndio wenyeji wa mkoa wa Kigoma wamekuwa wakiuhama mkoa huo na kukimbilia mikoa ya Morogoro na Tanga ambayo kwa kiasi kikubwa ina ardhi inayofanana na mkoa wa Kigoma, aidha wengine wamehamia kufanya biashara katika mikoa ya Tabora, Geita(hasa Chato) Mwanza(Sengerema) na Shinyanga hasa maeneo ya Katoro,Runzewe na Bukombe. Mikoa mingine pia ina waha wengi tu ambao wana maendeleo mazuri tu, kama wangeamua kuwekeza Kigoma ni wazi kungekuwa na mabadiliko.

Kama kasi ya wenyeji wa mkoa wa Kigoma itaendelea kuwa kubwa kama ilivyokuwa mwanzo na hivi ilivyo sasa, basi hakuna namna ya mkoa ule kuwa na maendeleo kwa mwenyeji, zaidi sana maendeleo yataonekana kwa watu waliohamia kufuata fursa ambazo ni nyingi sana hasa upande wa ardhi yenye rutuba.

Mikoa yote yenye maendeleo duni hugeuka kuwa mtaji kwa wanasiasa na viongozi waandamizi kwa sababu bajeti za mikoa husika hutolewa kila mwaka hata kama hakuna maendeleo. Tujiulize wakuu wa mikoa,wilaya na wabunge wao wanalipwa kwa kazi gani waliyoifanya wakati mikoa wanayoisimamia inaakisi umasikini uliokithiri?
Kituko na labda mshangao ninaoupata ni pale ninapoona awamu hii ya tano ikiwa imesheheni viongozi wakuu serikalini(Waha 3) tena kwenye nafasi nyeti na bado hakuna jitihada za kuuendeleza mkoa ule, naona na kusikia mbunge maarufu wa upinzani mkoani Kigoma akiwapiga vijembe na kuwaponda viongozi wenye asili ya Kigoma badala ya kuunganisha nguvu ile kubadilisha hali ya mkoa wa Kigoma.
 
Mtoa maada hafikirii kwa kina juu ya maendeleo yanayoletwa na watu weyewe wa eneo husika na yale yanayoletwa na Serikali! Hatahivyo, sioni kama kuna Mkoa usiyo na wachawi na washirikina. Ni fikra duni kusema, hauwezi kurudi nyumbani/Mkoani kwenu eti kwa sababu ya wachawi/washirikina wkt kila mahali wametapakaa hapa Africa na pengine Ulimwenguni kote. Jadilini kwa kina aina ya umasikini wa mkoa unaosababishwa na watu wenyewe na kwa hali halisi na ule umasikini unaosababishwa na uongozi mbovu wa Serikali husika
Nilipata kusoma sehemu kuwa South Africa wanataka kuanzisha chuo cha mambo ya Uchawi kwa hiyo watakuwa maskini?
 
Mleta mada lazima uwekwe kwenye chupa. Ndo utaacha umbeya wa kusema sema mikoa ya watu.
Tusipo waambia ukweli watazidi kuuua mkoa wa kigoma kwa ujinga wao. Tuwaambie wakajenge na kwao.
 
Back
Top Bottom