Mkuu mimi pia ni mzaliwa wa kanda hiyo. Our challenges are almost similar. Lets take it as a challenge. Nimeishi Kibondo, Kasulu, Ujiji nk. Kigoma bado iko nyuma hilo halipingiki. Tena nyuma sana! You can only understand kama umeshaliishi lile vumbi la Kibondo! Kikubwa tuzichukulie hizi kama Changamoto za mda. Sometimes nakuwa disappointed kwa sababu katika mikoa yetu ya kanda ya ziwa ni wahaya ambao waliweka utaratibu wa kujenga makwao toka zamani. Leo ukienda Kigoma kuna watu nawafahamu ni engineers, lawyers nk..tunakunywa nao bia mjini Lakini ukienda makwao huko ni fedheha! Siyo Kigoma tuu..njoo Ngara, bihalamlo, Chato nk. Wote tuna Changamoto zile zile. Bado ambao wamesonga mbele hawarudi nyuma kuwakwamua wa kwao!
Kipi kifanyike? Kwanza wananchi wa haya maeneo tuamke. Tutambue kwamba kuendeleza haya maeneo ni jukumu letu. Pili, Serikali iendeleze juhudi za miundombinu. Kama ile barabara ya Nyakanazi kwenda Kigoma ikikamilika nina hakika kabisa itabadilisha Kigoma. Na ile barabara ya Tabora-Kigoma ikiwekwa lami tutaongea mengine.
Ingawa miundombinu ni hafifu Lakini bado hata wana-Kigoma wenyewe hawajakamata fursa zilizopo kisawasawa. Mfano last time nilitoka Kabanga-Ngara nikaenda Bujumbura nikatokea Kigoma. Ule ukanda una fursa nyingi sana. Lakini ndo hivyo bado tunalia njaa na umasikini.
In all, lazima tukubali kwamba baadhi ya maeneo yetu yako nyuma na ni jukumu letu sisi wananchi kupambana na kuhakikisha tunajikwamua. Maana na hiyo serikali yenyewe tunayoitegemea inaongozwa na watu ambao nao wana vipaumbele na njaa zao.
Lakini as a matter of fact, kama mtu ambaye nimeishi na kufanya kazi Kigoma, Kiukweli wana-Kigoma can and should do better! Tunaweza kuweka visingizio maelfu mwisho wa siku ukweli unabaki pale pale. Tunahitaji kuamka.
Hata Kahama, Katoro, Lunzewe nk..miji inayochipukia....ni juhudi za watu. Juzi kati vilikuwa ni vijiji...leo tunaongea mengine.