Wana JF

Maelezo uliyonipa hayatoshi kumtambulisha huyo mtu.........Hivi unadhani kuna CUF wangap ambao wanaweza kuwa wanafanya kazi CCM. Mimi sio mwanasiasa siwezi jua. Ila hapo bado hujanisaidia kumjua MS.
ni mwandishi wa habari....!
 
I thought the motto was "Where we dare to talk openly" !!!!!!!!!!!!!
:shocked: :shocked: :shocked: :shocked: :shocked: :shocked: :shocked:
kweli wewe unafaa JF kweli wewe, ngoja tuanzishe thread ya ligi tukuchosheeeee, mwenyewe utatulia, maana weye si mgeni ati'
 
Salama humu?!
Rafiki yangu karibu sana...

Usione watu wana wasiwasi, kuna n'tu mmoja katuletea malokasa hapa kwa miezi kadhaa tumekaa kimya, sasa vijana wamemuamkia kwelikweli kaanza ku-multiply, so we are very cautious

Karibu pita mpaka ndani mazee
 

Wa chombo kipi cha habari?
Alichosema Ismail Jussa


Wale wanaokwepa hoja, ngoja niwawekee tena hapa post yangu ya kabla wajielimishe zaidi. Na nanukuu "Nachelea kujibu suala lako kwa sababu ni attempt ya kutuondoa kwenye mjadala niliouanzisha. Hii ni tactic nzuri ya kukwepa kujibu hoja katik...a mjadala. Wewe umemwambia Omar kuwa is attempting to divert from your point but it is you who is trying to divert the whole focus of the debate. Lakini bila ya kukuruhusu kutuondoa kwenye mjadala, nadhani ukiweka ushabiki wako pembeni, na ukawa objective kidogo tu, utaona kuwa kama kuna haja ya kuungana mkono basi Slaa na Chadema ndiyo waliopaswa kumuunga mkono Prof. Lipumba na CUF. Hoja zangu ni hizi (1) Kwanza Prof. Lipumba is more competent and more exposed in both local and international affairs and leadership than Slaa whose experience is merely of a whistleblower; (2) CUF ni chama cha kitaifa wakati Chadema iko Tanganyika tu; (3) Kwa performance ya kisayansi na si ya kukusanya watu kwa helikopta, CUF ina nguvu zaidi Bara na Zanzibar, kigezo ni kila uchaguzi CUF imekuwa mara zote inashika nafasi ya chama cha pili na hivyo kukipa sifa ya kuwa chama mbadala - angalia matokeo hata ya uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji ambapo pamoja na magazeti kuibeba sana Chadema, bado CUF imeshika nafasi ya pili (kumbuka huu uchaguzi ulikuwa Bara peke yake); (4) CUF imejijenga kitaasisi na kuweza kuwa stable party na kufanya maamuzi kwa utaratibu unaoleweka na ndiyo maana kina-manage migogoro ya ndani kwa njia za kikatiba na zinazoeleweka wakati Chadema kinaendeshwa na familia moja na zaidi Mtei/Mbowe. mfano mzuri wa kukosekana institutional framework na operationalisation ya Chadema ni ukweli kwamba kila kikifanya chaguzi za bawacha, bavicha etc zinavurugika kwa kukosa mwelekeo na mwongozo na kutawaliwa na matakwa binafsi ya baadhi ya viongozi; (5) Chadema kimeshindwa kujivua gamba la ukabila na udini na sasa ndiyo kinazidi kutopea huko wakati CUF imetanda kila pembe ya Tanzania; (6) CUF kina mtandao wa chama wenye muundo uliokamilika wa uongozi uliojipanga kitaasisi wakati Chadema hakina muundo na huishia kuokota wajumbe wa vikao mitaani kupata uhalali wa vikao; (7) CUF kimeonyesha umakini mkubwa katika uongozi na hata katika Kambi ya Upinzani Bungeni kimeonyesha ukomavu tofauti na Chadema ambao hata wale wabunge wake 11 tu wanashindwa kuelewana; (8) CUF kina misingi ya kidemokrasia na ndiyo maana hata Prof. Safari aliachiwa kushindana kwa uwazi na Prof. Lipumba kwenye nafasi ya Uenyekiti wakati Chadema kina uongozi wa kiimla wa muasisi wa Chama mwenye uwezo wa kumuengua mgombea Uenyekiti ili mkwewe apite bila ya kupingwa; (9) CUF kinaeleweka kiitikadi na kisera kuwa chama cha kiliberali na kimebakia hivyo katika historia yake yote ya miaka 18 wakati Chadema hakijitambui - kilianza kuwa mwanachama wa uliberali (Liberal International) na kuishia kujiunga na mtandao wa vyama vya kihafidhina ulimwenguni (International Democrats Union). Hata viongozi wake wako wanojiita capitalists, wengine wanasema ni liberals na wengine wanajiita social democrats. Kikishinda uchaguzi kitaongoza kwa itikadi na sera ipi? Hata chenyewe hakijitambui - kimejiunga na mtandao wa vyama vya mrengo wa kulia (Uhafidhina waliko Republicans, Conservatives, Christian Democrats, Likud etc) lakini Katiba yake inadai ni chama cha mrengo wa kati ambao ungepaswa kuwa ni Centrist - Liberal). Na kutokana na sababu hizo zote nimalizie kwa kuweka hitimisho ambalo ni nukta ya (10) Tiketi ya Lipumba/Juma Duni ni tiketi imara na yenye nguvu kiuongozi na kiuwezo ukilinganisha na ile ya Slaa/Said Mzee. Kwa hoja hizi chache tu kutokana na ufinyu wa nafasi na muda, nadhani utakubaliana na mimi kuwa ni Chadema iliyopaswa kuiunga mkono CUF mpaka hapo Chadema itapoweza kukua na kuwa na hadhi ya chama cha siasa badala ya kuwa kampuni ya Mtei and family" mwisho wa kunukuu. Nadhani tujielekeze kwenye hoja hizo na tusiishie kwa kutoa lugha za matusi ambazo ni dalili ya kuishiwa hoja na nguvu.
hapo vipi braniac?
 
Rafiki yangu karibu sana...

Usione watu wana wasiwasi, kuna n'tu mmoja katuletea malokasa hapa kwa miezi kadhaa tumekaa kimya, sasa vijana wamemuamkia kwelikweli kaanza ku-multiply, so we are very cautious

Karibu pita mpaka ndani mazee
Nashukuru ila angalieni msije kimbiza wageni wema.
:smile-big: :smile-big: :smile-big: :smile-big: :smile-big:
 
Nashukuru ila angalieni msije kimbiza wageni wema.
:smile-big: :smile-big: :smile-big: :smile-big: :smile-big:
ohoooo... na maonyo tena??? kwanza signature yako inaonekana mtu anajilipua, pili avatar yako ni ya heshima, tatu maneno yako si ya mgeni NA HIZO EMOTICONS ZAKO NDIO KABISAA... TAHADHARI, CHUKUA HATUA:deadhorse:
 
Braniac!

Kina kitu kina nisumbua waweza elezea kidogo hii " Honour Killings" kwa misingi ya imani yako....

Asante

 
ohoooo... na maonyo tena???
Ni angalizo tu,....no disrespect whatsoever intended.
:peace: :peace: :peace:
kwanza signature yako inaonekana mtu anajilipua,
Hiyo ni ecomotion tu kwangu hakuna zaidi ya hapo. Na ninachoomanisha ni kuwa nalipua bomu kuanika ukweli uliopo katika signature yangu lakini naona inawezekana watu wameitafsiri tofauti. Nashukuru kwa kuligusia hilo, nitabadili hiyo ecomotion muda si mrefu.
pili avatar yako ni ya heshima,
Nashukuru kwa kuliona hilo
tatu maneno yako si ya mgeni
Sijui unamaanisha kitu gani...japokuwa ni kweli mimi si mgeni kwenye forums lakini si hii ya JF.
NA HIZO EMOTICONS ZAKO NDIO KABISAA...
I am totally lost...............
TAHADHARI, CHUKUA HATUA:deadhorse:
Kinga ni bora kuliko tiba.....ni vizuri sana.:peace:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom