Ernest Sungura: Nilipata kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa hadi Mwaka jana 2022

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Ndugu zangu nadhani wengi mtakuwa mmepumzika. Lakini kwa kuwa nimewekwa katika kundi hili maalum baada ya kutokea mjadala kunihusu, naomba nianzie kujibu kilichoandikwa JF na mengine yatafuata taratibu

Ndugu zangu wana Tasnia ya Habari, kipekee sana ninawashukuru kwa maswali na mjadala humu kuhusu kauli ya kuchaguliwa kwangu nafasi ya Katibu Mtendaji wa MCT. Ninamshukuru sana Mwenyezi Mungu, Bodi ya Wakurugenzi ya MCT, Wajumbe na Wana TASNIA wote mlionistahilisha.

Nitakuwa na wasaa wa kufafanua mengi wakati ukifika, nitakapokuwa, rasmi, Mtendaji Mkuu wa Taasisi yetu ya MCT. Kwa sasa ninaomba niseme kwa kifupi sana:-

1. Mimi si Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa. Ni kweli nilipata kuwa Mjumbe. Ujumbe wangu ulikoma tangu mwaka jana. Baada ya hapo, kama walivyokuwa wanatasnia wengine waliowahi kurudi kuitumikia Tasnia, nami nilirejea rasmi kuitumikia tasnia yangu ya habari kwa nafasi ya Lead Mentor katika taasisi niliyowahi kuiongoza zamani ya TMF.

2. Kuhusu nafasi ya MCT kumekuwa na mchakato huru wa zaidi ya mwaka mmoja wa nafasi ya mrithi wa Katibu Mtendaji aliyepo sasa. Ni imani yangu kuwa jopo la Wabobezi husika limejiridhisha kwa vigezo na masharti yote kabla ya kuutangazia umma kustahili kwangu. Ninamshukuru Mungu na wote waliohusika katika mchakato huo.

3. Naomba niwashukuru sana wote waliochangia katika mada hii. Nimeona kuwa wapo wengine waliofafanua au kutoa majibu ya hoja kadhaa. Ninawashukuru sana.

4. Kwa sasa Katibu Mtendaji bado ni ndugu yetu na mwanatasnia mwenzetu Kajubi Mukajanga. Wakati ukifika na ikimpendeza Mwenyezi Mungu kuvaa viatu vyake rasmi, nitatoa ufafanuzi zaidi ikibidi kwa hoja zitakazojitokeza huku nikiomba ushirikiano wenu mliowahi kunipa enzi nikiongoza TMF iwe hivyo pia kwa taasisi yetu ya MCT.

ASANTENI SANA!

Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM ateuliwa kuongoza Baraza la Habari Tanzania (MCT)
 
Back
Top Bottom