Wana jf niungeni mkono namshtaki lusinde.

Dec 11, 2010
3,321
6,328
Wakuu.
Mtakumbuka kuwa mbunge wa Mtera Mheshimiwa alie kubuhu kwa Matusi Livingstone Lusinde muda mwingi wa kampeni za Arumeru alikuwa akiporomosha mipasho ya matusi badala ya kunadi sera za chama chake dhidi ya viongozi waandamizi wa chadema.

Nimeona nijitoe na kuchukua jukumu la kumshtaki kwa matusi yake aliyo kuwa anatoa, hivyo basi, kwa kutambua kuwa yeye ni mwanasiasa asiye kuwa na staha wala kidhibiti maneno kwenye mdomo wake nimeamua kumfungulia mashtaka kwenye mahakama ya wananchi, mahakama kubwa yenye madhara ya sasa na baadae kwa wanasiasa, mahakama hiyo ni wananchi hasa wa jimbo lake walio mchagua.

Nimeamua kuchoma [ku-burn] cd za matusi yake na kuanzia jumamosi na jumapili ya juma hili [siku za mapumziko baada ya kulitumikia taifa] nitakuwa stendi ya mabasi ya Dodoma nagawa bure cd hizo kwa abiria wanao kwenda Dodoma nikiamini kuwa zita wafikia wale ambao hawana fursa ya ufahamu wa kushusha [kudownload] matusi hayo kutoka kwenye youtube.

Shime wapenda mabadiliko na wote mlio chukizwa na matusi hayo niungeni mkono. Kama una laptop au kompyuta ya kawaida download matusi ya Lusinde, nunua ki kasha cha Cd ambacho ni kiasi cha shilingi elfu 10 au nunua cd za rejareja kwa shilingi 300, zi-burn kisha piga moyo konde nenda pale stendi ya ubungo mwisho wa juma tafuta gari za Dodoma wape bure abiria kiasi unacho weza.

Kwa wale wana JF walioko Dodoma, wafanye hivyo kwa kugawa kwa abiria wanao kwenda moja kwa moja Mtera. Naamini kama wengi wetu hatukupenda matusi yale wapo walio mchagua pia hawata yapenda, watajua namna ya kumuadhibu au kumsamehe.

Naomba kuwasilisha nikiamini kuwa tunaweza kama tukiamua kukomesha viongozi wazalilishaji. Popote ulipo saidia kwenye hili kwa njia yoyote.
 
Upo Dar maeneo gani? Nipo Dar ila naondoka Kesho kutwa napenda tuonane nifanikoshe Kidogo hili hata kwa empty CD za kutosha.
 
Kwakweli hilo jambo ni la busara na nakuunga mkono muheshimiwa ila usisaha na zile za dr. Slaa pale mwembe yang alipomtukana jakaya kikwete na mama yake kipindi cha kampeni burn kwa pamoja....tukipata wazalendo 100 tu kama wewe tutafika mbali.
 
wakazi wa mtera wengi wanatumia zile kanda za zamani...
 
Umenena kweli Mtoi na hakika wazo lako ni zuri sana. Nimewatumia pesa na ujumbe huu wa kukuunga mkono wadogo wangu wawili ili wafanikishe zoezi, mmoja yuko Udom na mwingine chuo cha mipango. Kwa wanachuo wote walioko Dodoma walioko humu jf watusaidie kufikisha kesi hii mahakama ya wananchi na wengine wenye ndugu/jamaa Dodoma wawezesheni kumshtaki Lusinde kwa wanajimbo wake.
 
Umenena kweli Mtoi na hakika wazo lako ni zuri sana. Nimewatumia pesa na ujumbe huu wa kukuunga mkono wadogo wangu wawili ili wafanikishe zoezi, mmoja yuko Udom na mwingine chuo cha mipango. Kwa wanachuo wote walioko Dodoma walioko humu jf watusaidie kufikisha kesi hii mahakama ya wananchi na wengine wenye ndugu/jamaa Dodoma wawezesheni kumshtaki Lusinde kwa wanajimbo wake.
dah we unataka umfukuzishe chuo mdogo wako
 
Nimelipenda hili wazo. Acha sasa tumrudishe akafanye kazi yake ya U-DJ. Hatuwezi kuwa na kiongozi anaenuka mdomo. mitusi-mitusi tu, tena mbele ya watoto. Hakuna haja ya kumwonea huruma. kama kuna mtu mwingi mwenye wazo mbadala nae aungalishe. we need to have intergrative aproach kummaliza
 
Mi nadhani zoezi hili lisiishie Dodoma tu, Lusinde alisimama pale jukwaani kuwakilisha Chama chake (CCM).
Hivyo basi tuna jukumu la kukishtaki Chama chake kwa Watanzania wote tukianzia Mtera anakotoka yule ki.la.za.
 
Ile Audience hadhara aliyokuwa akiihutubia ilikuwa ya namna gani? mbona haikuonyeshwa vema? Mimi nimeona ni watoto na wanawake wachache. iko kama vile ilikuwa ya kimagumashi!

Hakika hata nafsi yake inansuta!
Tumshitaki kwa umma wa watanzania wote! Naunga umko hoja
 
Wakuu.
Kuunga mkono hoja kuendane na matendo. Nunua cd's burn zitume Dodoma au gawa kwa watu unao ishi nao karibu, kama sivyo hamishia kwenye simu wahamishie watu kwa bluetooth.
 
Back
Top Bottom