Wana JF, Kuna nini Apollo Hospital? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wana JF, Kuna nini Apollo Hospital?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by majany, Nov 1, 2011.

 1. majany

  majany JF-Expert Member

  #1
  Nov 1, 2011
  Joined: Sep 30, 2008
  Messages: 1,199
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Jamani hivi hakuna mkono wa mtu yeyote ambaye anapata manufaa kwa wagonjwa kupelekwa kwenye hospitali hii??au nani anawaelewa wamiliki wa hospitali hii??
   
 2. P

  Percival JF-Expert Member

  #2
  Nov 1, 2011
  Joined: Mar 23, 2010
  Messages: 2,567
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Hii ni hospital maarufu na ya hali ya juu na bei yake ni nafuu ukiringanisha na hospitali za nchi za magharibi. Watu wengi wa nje wanatumia hii hospitali.

  Kitu ambacho unatakiwa kujiuliza sii hawa wabunge wanakwenda hospitali gani , swali ni kuwa ikiwa wao wanapata hizi huduma watakuwa na motisha gani kuweka juhudi kuwa hospitali za hapa nchini zitowe huduma nzuri .
   
 3. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #3
  Nov 1, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  apollo wanatarajia kujenga hospitali tanzania.
   
 4. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #4
  Feb 1, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Je wajua: Kwenda kutibiwa India inawezeka ni "biashara" ya watu fulani?

  31/01/2012  Ni ujumbe kutoka kwa mdau wa afya, unajieleza! Tafadhali tuachane na kuuliza "nani mjumbe" tukazie "nini ujumbe"!

  [HR][/HR]

  It is very possible that, private practice in India is driven by pay back system, you refer a patient to Apollo you get paid.

  I just don't have evidence but I am sure move za hospitali kukusanya wagonjwa na kuwapeleka India zitakuwa driven by this payment system, I bet our officials may also be involved.

  And these people are serious about that business, Apollo wanaanza kuwapa huduma wagonjwa Dubai, so from the airport you start getting services.

  And the practice is made in such a way unafanyiwa vipimo vingi kadiri inavyowezekana, including those you don't need, the aim being to maximize the cost.

  I am posted at Christian Medical College Hospital in India, this is a hospital which is not business oriented, but it is the best cardiology centre in India, it is one of the best nephrology centre in India also, iko Tamil Nadu km 120 kutoka Chennai.

  The cost of services here is 1/3 ya gharama za Apollo and the like, the cost is even cheaper as compared to cost of some services in Nairobi (kuna mgonjwa alikuwa na leukemia Nairobi, gharama ya matibabu Nairobi ilitosha kulipia usafiri, matibabu gharama za kuishi hapa Vellore na akabaki na change), but guess what, no one is referring patient to CMC even in India itself because this hospital does not entertain the system of pay back!!!!!

  It is very sad in deed!
  Source: wavuti.com* - Blogu
  Under Creative Commons License: Attribution Share Alike
   
 5. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #5
  Feb 1, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,663
  Likes Received: 3,317
  Trophy Points: 280
  Alaaa kuuumbeeeeee
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Feb 1, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,532
  Trophy Points: 280
  Eng. Mtolera,
  Hapa umesema kweli, kuna tip nono madakitari wetu wanapata ku recomend watu waende Apolo!

  Nilipata Brachial Plexsus nikaenda Muhimbili hawatibu wakaniuliza kama nitaaford niende South au India. Nikachagua South, wakafanya initial oparation. Nikarudi ila kwa vile cost za South ni kubwa, nika opt kwenda India, Apollo!.

  Hapo nilikuta ni biashara zaidi kuliko matibabu!. Unafanyiwa kila kipimo unanunuliwa kila kifaa na madawa kibao hata ambayo huyahitaji!.

  Walifanya walichoweza in bussiness wise na kurejea nyumbani!. Baada ya muda kupita nafuu kidogo ndipo nikaseek second opinion toka kwa daktari bingwa toka Ujerumani ndipo akafanya vipimo upya na kuniambia India did nothing! kwa kwa assesment yake they can do nothing!. Lakini kila madaktari wa India wakija huniona na kunisisitizia "You just come to Apollo there is something we can still do!".

  Hebu toa hizo data za hiyo Hospital pale Wizarani kama mijitu haijakutolea mimacho!. Wahindi ni wafanya biashara wazuri ila hii biashara ya matibabu kwa watu wa nchi masikini kama Tanzania huku madaktari bingwa wetu wakivuna chochote!, huu ni unyonyaji mbaya kuliko ukoloni!. No wonder kwa nini madaktari bingwa hawagomi!.
   
 7. k

  kajunju JF-Expert Member

  #7
  Feb 1, 2012
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Hii inajulikana kuwa ni biashara. muhindi hana urafiki na mtu mweusi, urafiki na pale tu unapomtumia ili apate.serikali hii inafanya biashara si vingine
   
 8. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #8
  Feb 1, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Kama unataka kusema jambo sema ukiwa na ushahidi, kama ni hisia zako tu kuwa makini kusema. nitafurahi mkithibitisha hili maana litawafungua watu macho na sio kuwaongezea manunguniko juu ya gharama za matibabu.
   
 9. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #9
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  kuna ukweli hapa hata mm nlishasikia na kushuhudia. india sio mchezo
   
 10. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #10
  Feb 1, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  eheeeeeeee :nerd:
   
 11. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #11
  Feb 1, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Naona Pasco huko busy na madaktari baada ya sarakasi zako za jana kugonga mwamba

  Shame on you:A S embarassed:
   
 12. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #12
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Pasco
  tunategemea msaada kutoka kwenu,kuweka wazi haya mambo,nyie karamu zenu zinafika mbari sana
   
 13. B

  Bijou JF-Expert Member

  #13
  Feb 3, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145

  mkuu naomba address ya hiyo hospitali ya Christian Medical College Hospital, huwezi juwa inaweza hitajika, seriously plessssssssssssssssssssz naoma
   
 14. C

  Cape city Member

  #14
  Feb 3, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Duuuuh.....
   
 15. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #15
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  subirini niwaletee daktari mmoja wa india alivyojaribu kuadvertise hospitali yake ili tuwapeleke wagonjwa huko india.
   
 16. Allyeee

  Allyeee Member

  #16
  Feb 5, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 75
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wadau wa jf nashindwa pata jibu hv ni kwanini kila kiongozi mgonjwa anaenda kutibiwa India tena hospital ya Appolo inamaana Hamna hospitali nyingine?
   
 17. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #17
  Feb 5, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  wana mkatabata na hiyo sipitali
  afu kuna punguzo la bei.
   
 18. B

  Baba Jotham Member

  #18
  Mar 18, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 84
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Ni muda kidogo nimejaribu kujiuliza na kutafakari zaidi juu ya mahusiano yetu kama taifa na Hospital ya Apolo iliyopo nchini India.Nimejaribu kutafakar ubora wake,huduma zake,gharama zake na mengine mengi hadi kutushawishi kama taifa kuwapeleka viongozi wetu wakubwa kwa matibabu(Mwandosya na Mwakyusa).Siyo hao tu,hata yule aliyemwagiwa tindikali igunga alipelekwa huko.Pia msanii wa original comedy naye amepelekwa huko kwa ufadhili wa raisi wa jamhur ya muungano.
  Napenda kujua kulikoni Appolo? je kuna ajenda ya kisiasa katikati? na kama ni ubora wa kuzidi nchi zote duniani,sisi kama taifa tunajifunza nini?
   
 19. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #19
  Mar 18, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  ni swala la ubora na unafuu wa gharama za tiba.

   
 20. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #20
  Mar 18, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Hapo kuna 10% ya Blandina kwa kila mgonjwa anaingia ile hospitali. Kwa hiyo hata kama Pinda kamuweka bench BNyoni lakini bado anavuta mkwanja wake toka kwa wahindi.
   
Loading...