Wana Gangilonga mpo?

Hii thread inanikumbusha
mbali sana sana

Tusker Baridii nafikiri tulikuwa wote class moja, mi nilikuwa Class ya 1987, hii thread inanikumbumbusha mbali sana sana, class mate wangu walikuwa ni Kina Joyce Kibasa, Zena Mkwawa, Nyambilia Amuru, Makumulo Waziri, Stewart Mwakabuta, Idi Mtalika, Nasoro Mkwanda, Mercy Sanga, Charles Lusinde, Gloria John (mtoto wa RTO), Moses Mkandawile (RIP). Tulipomaliza seven me nilikukwenda Ifunda Tech Secondary School, lkn Colleagues wangu wengi walikwenda Lugalo Sec.
we uchira1 mbona hilo ndilo lilikuwa chama langu! Kama utakumbuka demu wangu alikuwa Zena na iko siku moja nikakuta wanapeana sound na Godfrey mbwilo pale kwenye mti mkubwa, bahati nzuri shaban wa ndiuka alikuja na yai viza mbili, akapiga walipokaa kisha TUKATELEZA kimyakimya maana tuliogopa jamaa yeye alikuwa darasa la juu yetu na alikuwa superstaa wa Breakdance. unamkumbuka Nassoro eti alikuwa anajidai yeye ni Micheal Jackson
 
Namkumbuka sana Nassoro alivyokuwa anafunga mayenu, na yule jamaa wa stori za cinema za kihindi unamkumbuka?? sikumbuki jina lake. Please ni PM.
 
Naomba tukumbushane enzi za shule.
Mnamkumbuka walimu wa kuu MR Mndeme na kipigo chake na Mr amuri?
Pia muheshimiwa John komba alitufundisha siasa tukiwa darasa la 4 alivyo maliza jkt mafinga alikuwa mwembamba sana (mwalimu wa upe)

Kumbe ni jina la shule mimi nilidhan ni aina ya dawa
 
Namkumbuka sana Nassoro alivyokuwa anafunga mayenu, na yule jamaa wa stori za cinema za kihindi unamkumbuka?? sikumbuki jina lake. Please ni PM.
Jamaa wa story za movie za kihindi nadhani alikuwa anaitwa IBRA, alikuwa mjanjajanja hivi, kwa mwezi anakuja shule siku kumi tu, nakumbuka alitaka kuniingiza mkenge eti nichukue mtungi wa gesi home nimpe akauze.
 
Wana Gangilonga mpo? juzi nilikutana na mwl Hassan dhabiu, bila shaka wewe wa miaka yetu utamkumbuka
alikuwa head teacher miaka yetu na kwa sasa ni mwl mkuu shule ya msingi kihesa ana jiandaa kustaafu
kiukweli alisikitika sana, kuona wanagangilonga tumejisahau hata kuikumbuka shule yetu kwani anataarifa za wadau
wengi wa Gangilonga kuwa wapo juu kimaisha wengi ni wataalamu wa fani tofauti kanipa kazi moja
ya kutafuta no zenu nimtumie aitishe kikao hapa Dar kama wanavyofanya watu a mikoa ya kaskazin.
huu mtandao wetu tuu imarishe ili tuweze anzisha mfuko wa kuisaidia shule yetu.
mimi nilisoma mwaka 1984 to 1990 na no 1 wetu drsn ni Eng Hery sanga , Asimwe bashagi, elton mgongolwa ,andambike mgata ,zena amuri farida kyula, farisa mohamed, selwin john, ipyana mwabwalwa, taba hamis ,ramla kayugwa stan ndali, patrick kihomano, patrick mtenzi, said kitembe korosha mshangila ,niko mwakasege,sifael kulanga
naly mkandawile, sanura nurdin, fatuma nurdin (rip) oscar chongola stela silayo, lukas kambanyuma, kisa mwakalundwa,
husein nose george chagu christian mpalile n.k
 
we uchira1 mbona hilo ndilo lilikuwa chama langu! Kama utakumbuka demu wangu alikuwa Zena na iko siku moja nikakuta wanapeana sound na Godfrey mbwilo pale kwenye mti mkubwa, bahati nzuri shaban wa ndiuka alikuja na yai viza mbili, akapiga walipokaa kisha TUKATELEZA kimyakimya maana tuliogopa jamaa yeye alikuwa darasa la juu yetu na alikuwa superstaa wa Breakdance. unamkumbuka Nassoro eti alikuwa anajidai yeye ni Micheal Jackson

Kumbe ulikuwa unanichukulia demu wangu Zena? Bahati yako sikukujua, ningekuloga!
 
Tusker baridiii! je wewe ninani hasa? nadhani tulisoma wote enzi hizo maana hawa members wote nawajua. Je unamkumbuka ISACK OGUNDESI? Nasoro mara ya mwisho alikuwa moro mhasibu wa manispaa ya wilaya.

Mimi nilihama 1986 tukiwa la sita.
 
Vijana wote ndani ya JF mliopitia Gangillonga "JIWE LINALOSEMA" au ILIGANGA LILONGA (Kwa Kihehe) mmenifurahisha sana kwa jinsi mlivyonikumbusha kuhusu Shule hiyo iliyokuwa imetukuka.Mimi nilitoka pale 1973 wakati Mwalimu Mkuu akiwa Mr.Luhanga,huyo Mwalimu Mndeme (kama ndiye huyo) ndiyo kwanza alikuwa amekuja kuanza kufundisha baaada ya mafunzo yake ya Ualimu. siku kadhaa zilizopita nikiwa kwenye hamsini zangu nilipita hapo Gagilonga ili angalau niione shule iko katika hali gani, kwa kweli inasikitisha utadhani labda ni pango la SIMBLISI.Mandhari nzuri na majengo yaliyokuwa na hadhi, Maabara na Ukumbi mkubwa, maua na Miti mirefu na mizuri yenye maua ya kuvutia vyote hivyo vimetoweka.

Kwa kuwa ninyi vijana mmechangamka kuhusu shule yetu hiyo pendwa na ninaamini mtakuwa katika nafasi nzuri za kuweza kuanzisha wazo la jinsi gani ya kusaidia kuboresha shule hiyo kama moja ya jukumu letu kwa nchi yetu.Leteni wazo hilo hapa JF then tufanye utaratibu wa kuona tutafanya nini kwa ajili ya GANGILONGA yetu pendwa.Serikali yetu ipo usingizi wa PONO sitarajii hata siku moja Manispaa ya Iringa wataweza kuirejesha hali ya Shule angalau kwa 25% only.

Niliandika muda mrefu uliopita,hebu tufanye linalowezekana katika kuisaidia shule yetu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom