Wana DarWing tukamuone mwenzetu Inkoskaz

Wana DarWing tukamuone mwenzetu Inkoskaz

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,758
Reaction score
9,592
Habarini marafiki


Leo hii nimesoma thread ya
Inkoskaz imenihuzunisha na kunifanya nione huruma juu yake. Thread hii ina kichwa cha habari kisemacho "Tafuteni nanyi mtaona, bisheni mtafunguliwa, na ombeni nanyi mtapewa". Ipo kule kwenye Gazeti letu la JF, Habari na hoja mchanganyiko.

Kwanini nimewaomba wana DarWing tukamuone mwenzetu huyu rafiki mwenzetu hapa alipatwa na ajali mbaya sana ambayo imepelekea baadhi ya viungo vyake kuvunjika kwa ajali hiyo.

Nilivyosoma hii post machozi yalinitoka kwa ghafla nikashindwa kuendelea kusoma kwani yalikuwa yanandoka kwenye keyboard, na nikaingiwa na huruma ambayo nashindwa kuielezea hapa kwani muda si mrefu nimetoka kuisoma na nimemuomba mawasiliano ili niweze kuwaorganize wenzangu twende tukamwone
mwenzetu pale MOI kitengo cha mifupa, alilazwa tangia July alipopata ajali mbaya pale maeneo ya TABATA 15/AUGUST alipoandika hiyo hiyo thread.

Jamani marafiki zangu wote tujipange twende Muhimbili tukamwone mwenzetu. Leo ni kwake hujui kesho ni kwa nani tuwe pamoja katika majanga haya.

Sitaki kuwahimiza au kuwafanya mjisikie kama nilivyojisikia mie bali nawasihi tu kwa huruma zake Mungu tujipange wapendwa twende tukamwone kwa yule aliye nafasi au kitu chochote tupange siku twende pale Muhimbili tukamwone rafiki yetu.

N:B. Samahani kwa wale ambao ni wepesi wasiangalie picha hizi

TUMUOMBE KWA MUNGU AMPONYE NA AMPE AFYA NJEMA

Hapa ndivyo alivyo:
View attachment 114544View attachment 114544


copy: Bujibuji, cacico, Mtambuzi, gfsonwin, Smile, Kipaji Halisi, Jiwe Linaloishi, Paloma, Mamndenyi, Madame B, Kijino, Asprin, Mentor, Lady doctor, watu8, figganigga, mathematics, Mwita Maranya, Mokoyo, swagga, stevoh, monaco, @Mgeda, sweetlady, Bishanga Maxence Melo na marafiki wengine ambao sijawamention hapa pls tupange ni lini tukamwone mwenzetu

Nc: kwani hujafa hujaumbika wapenzi
kibao ha
 
Last edited by a moderator:
Ni faraja iliyoje kukuta uzi huu wa ladyfurahia na wadau waliochangia kwa kuguswa.inanikumbusha maana halisi ya kujiunga jf ni kujifunza.kuhabarishana..kujenga mahusiano.kusaidiana..kufanikisha biadhara ns malengo..kupeana ushauri.. nasaha..faraja na masuluhisho kwa ushirikiano
mbarikiwe nyote kwa mashirikiano haya
 
Last edited by a moderator:
Ni faraja iliyoje kukuta uzi huu wa ladyfurahia na wadau waliochangia kwa kuguswa.inanikumbusha maana halisi ya kujiunga jf ni kujifunza.kuhabarishana..kujenga mahusiano.kusaidiana..kufanikisha biadhara ns malengo..kupeana ushauri.. nasaha..faraja na masuluhisho kwa ushirikiano
mbarikiwe nyote kwa mashirikiano haya

Kaka pole sana.. Unaendeleaje sasa..?

Ahsante sana ladyfurahia kwa taarifa..
 
Last edited by a moderator:
Kaka pole sana.. Unaendeleaje sasa..?

Ahsante sana ladyfurahia kwa taarifa..

Mkuu asante..naendekea vema.madaktari na wauguzi kwa uwezo wake mola wamefanya kazi yao kwa ufanisi na hivyo kunipa nafuu
Ni janga linalochukua muda mrefu kutengemaa.uvumilivu na imani ni silaha kuu
 
Last edited by a moderator:
pole sana sana sana Mkuu,tuko pamoja,bado upo pale MOI? Unaweza kutoa Mwongozo kidogo?
Mimi nina Imani utapona,Kwa Imani utapona.
Shukuru Mungu kwa Kuwa ni Mwema.
Pole sana.
 
Mkuu asante..naendekea vema.madaktari na wauguzi kwa uwezo wake mola wamefanya kazi yao kwa ufanisi na hivyo kunipa nafuu
Ni janga linalochukua muda mrefu kutengemaa.uvumilivu na imani ni silaha kuu

Hakika Mungu ataweka mikono yake juu ya madaktari wako uweze pata tiba na uponaji wa haraka na urejee kama awali!
 
Pole sana mwana jf mwenzetu. ladyfurahia tujuze namna ya kumpata hapo naweza pitia pale Ili nikamwone.
unifikishie na salamu zangu rafiki....
Mungu akipenda nitakapoibukia Dar nitamtafuta.
Pole sana Inkoskaz kwa kuugua, Tunamshukuru Mungu kukuona unachangia tena uzi. Mungu ni mwema atakupitisha salama
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom