Wana CCM Wenzangu hiki tunachokifanya hakina Baraka za Mungu

Toka hela tuzochanga kuwahami ndugu zetu wa kagera zilipogeuzwa rungu la kisiasa, mimi sichangi tena!!!!!

Hata msiba wa arusha sikuchanga.
Kama ni kosa kutokuchanga/ kutoa rambirambi naomba mnisamehe.

Hela zangu haziwezi kupangiwa matumizi na wajinga wajinga mithili ya Gambo.
 
Huyu Bollen Ngetti namfahamu sana. Ni kada mtiifu sana wa chama chakavu lakini kwenye ukweli jamaa hapepesagi macho. Naona tutasikia "si mwenzetu" au kuvuliwa uanachama. Wazalendo hawatakiwi CCM.
 
Kusema ukweli kitendo cha CCM kula pesa za wafiwa ni laana kubwa
 
Hivi wakiambiwa ndio wamewaua wale watoto ili eapate pesa watamlaumu mtu
 
WANA CCM wenzangu, hiki tunachokifanya hakina baraka za Allah/Mungu/Yehova/ Nyasaye kabisa. Hebu tulitafakari maana sidhani kama ni ubinadamu. Huu ni utapeli ndugu zangu tusiunge mkono hata kama nia ni njema kiasi gani.

Nazungumzia huu utamaduni mpya wa kukusanya pesa za rambi-rambi na kuyapangia matumizi mengine. Hii ni dhahiri Serikali yetu inafurahia majanga na mabalaa kutokea ili kupata pesa. Kwamba majanga ni dili (biashara). Hii ni aibu kubwa. Tunaona wivu wa mini na hela za rambi-rambi? Huu si utu!

Nimekutana na mzazi aliyepoteza mwanaye Arusha anaumia sana kusikia eti kifo cha mwanaye imekuwa ni chanzo cha mapato ya Serikali kukarabati Hospitali ya Mount Meru. Amelia sana mbele yangu kwenye simu.

Nashauri ingependeza basi baada ya kukusanya rambi-rambi yote hata kama ni Mabilioni Ndg Mrisho Gambo angewaita wafiwa wote pamoja na kuuza wazo hilo kwao then kuwasikiliza maoni yao. Pengine wangesema kiasi Fulani mtupe na salio ikaboreshe hospitali au kununua vitabu kwa shule zote za Arusha. Wafiwa si wajinga wangetoa mawazo mazuri. Huo ndio uongozi shirikishi na si kuwapangia matumizi pesa zao. Ndio maana nimetoa wito kwa wanasheria kuwasaidia wafiwa hawa kudai pesa hizi ni zao. Mkoa haukufiwa, Gambo hakufiwa. Wapo wazazi in person waliofiwa ndio wanaochangiwa. Daini hela hizi ili iwe fundisho kwa majanga yajayo (hatuombei).

Tukiruhusu utamaduni huu mpya wa kutumia rambi-rambi siku atatokea Mkurugenzi mwendawazimu akishatafuna hela za umma na hana namna ya kulipa ni kuhujumu njia ya reli iache njia watu wafee kadhaa au achome shule maana rambi-rambi itakusanywa naye kuzipangia matumizi alikoiba. Tusishabikie hili la rafiki yangu Gambo. Si Jema!

NASISITIZA: Wanasheria wasaidieni wafiwa kudai hela hizi maana ni zao. Ni kwa ajili ya watoto wao. Watatumia kupalilia makaburi ya wanao. Niko tayari kulipia gharama za mawakili ili tabia hii ikome Tanzania. Misiba ya watu isiwe harusi ya Serikali.
[HASHTAG]#UzalendoKwanza[/HASHTAG]. Bollen Ngeti. UVCCM Taifa
Kwa hiyo serikali ya awamu hii imegeuza majnga na misiba kuwa revenue source, hiyo kali, kwa hiyo huko tunako elekea ukifiwa rambi rambi zote mali ya serikali sijui kama tutafika.
 
Inasikitisha Zaidi ya Kawaida kama Msiba huo usigetokea inamaanisha ukarabati ulikuwa hakuna ?Nami Naunga hoja Tumuogope Mungu Matukio ya Majanga na Misiba kisigeuzwe kuwa chanzo cha kupata fedha za Rambirambi kwa Wahanga na kuzibadrishia Matumizi Tumuogope Mungu Tuwajali Wajane,Yatima na Wagane tuiepuke gadhabu ya Mungu
 
WANA CCM wenzangu, hiki tunachokifanya hakina baraka za Allah/Mungu/Yehova/ Nyasaye kabisa. Hebu tulitafakari maana sidhani kama ni ubinadamu. Huu ni utapeli ndugu zangu tusiunge mkono hata kama nia ni njema kiasi gani.

Nazungumzia huu utamaduni mpya wa kukusanya pesa za rambi-rambi na kuyapangia matumizi mengine. Hii ni dhahiri Serikali yetu inafurahia majanga na mabalaa kutokea ili kupata pesa. Kwamba majanga ni dili (biashara). Hii ni aibu kubwa. Tunaona wivu wa mini na hela za rambi-rambi? Huu si utu!

Nimekutana na mzazi aliyepoteza mwanaye Arusha anaumia sana kusikia eti kifo cha mwanaye imekuwa ni chanzo cha mapato ya Serikali kukarabati Hospitali ya Mount Meru. Amelia sana mbele yangu kwenye simu.

Nashauri ingependeza basi baada ya kukusanya rambi-rambi yote hata kama ni Mabilioni Ndg Mrisho Gambo angewaita wafiwa wote pamoja na kuuza wazo hilo kwao then kuwasikiliza maoni yao. Pengine wangesema kiasi Fulani mtupe na salio ikaboreshe hospitali au kununua vitabu kwa shule zote za Arusha. Wafiwa si wajinga wangetoa mawazo mazuri. Huo ndio uongozi shirikishi na si kuwapangia matumizi pesa zao. Ndio maana nimetoa wito kwa wanasheria kuwasaidia wafiwa hawa kudai pesa hizi ni zao. Mkoa haukufiwa, Gambo hakufiwa. Wapo wazazi in person waliofiwa ndio wanaochangiwa. Daini hela hizi ili iwe fundisho kwa majanga yajayo (hatuombei).

Tukiruhusu utamaduni huu mpya wa kutumia rambi-rambi siku atatokea Mkurugenzi mwendawazimu akishatafuna hela za umma na hana namna ya kulipa ni kuhujumu njia ya reli iache njia watu wafee kadhaa au achome shule maana rambi-rambi itakusanywa naye kuzipangia matumizi alikoiba. Tusishabikie hili la rafiki yangu Gambo. Si Jema!

NASISITIZA: Wanasheria wasaidieni wafiwa kudai hela hizi maana ni zao. Ni kwa ajili ya watoto wao. Watatumia kupalilia makaburi ya wanao. Niko tayari kulipia gharama za mawakili ili tabia hii ikome Tanzania. Misiba ya watu isiwe harusi ya Serikali.
[HASHTAG]#UzalendoKwanza[/HASHTAG]. Bollen Ngeti. UVCCM Taifa
michango ya taasisi ingejikita kwenye mazishi kwa hadhi na uwezo wake... na pesa zilizotolewa na watu na mashirika ya dini na binafsi zingelenga wafiwa period.... Mengine yaliyoyafanya ni aibu.
Wajifunze kwa next time.. dunia ya sasa kosa kidogo unazua makelele
 
..kifo cha mwanaye imekuwa ni chanzo cha mapato ya Serikali kukarabati Hospitali ya Mount Meru.

No wonder Mrisho Gambo na boss wake Magufuli hawataki katakata pesa ipite sehemu nyingine zaidi yao. This is madness. Michango ya rambirambi kusaidia wafiwa inakuwaje inapigwa panga ili ukakarabati Hospitali? Why?
 
Kuna kitu sijakielewa hapo Arusha kwa huyo bwana Mkoa.
Hivi wazo la kutapeli fedha za rambirambi limekuja baada ya kutuhumiwa kuwa kuna fedha hazionekani au lilikua limeshapangwa tangu mwanzo?
Nauliza tu, je, Makamu wa Rais alisomewa risala ya maamuzi ya mkoa kuchota fedha za rambi rambi zilizochangwa kwa ajili ya kuwafariji wazazi waliopatwa na msiba au ni ujanja wa bwana mkoa ameamua kutumia baada ya kuingia kwenye kashfa nzito ya kuficha kiasi cha fedha za rambirambi ili kumdanganya mkuu wa ardhi ya Tanganyika?

Kama hilo wazo lilikuwepo tangu mwanzo basi namsamehe bwana mkoa mana itakuwa ni makubaliano ya kamati ya maafa ya mkoa.
Lakini la kama ni wazo lake la kijanja baada ya kutuhumiwa na kubaini kuwa endapo mkuu wa ardhi ya Tanganyika akifuatilia na kugundua kuwa hawa kuna fedha zimepotea basi hali yake ya kimadaraka ingekuwa mashakani .Yani ametafuta kiki ya kumfurahisha bwana mkuu wa ardhi ya Tanganyika basi siwezi kumuunga mkono huyo bwana mkoa kwa hilo.
Rambi rambi ile bado ilitolewa kwa sababu ya ule msiba kuwagusa sana watanzania na sio kwa ajili ya kutekeleza miradi ya serikali.

Wazazi wa wale watoto ndio walioathirika kwa kusomesha watoto wao kwa gharama kubwa kwa miaka saba halafua wakawapoteza watoto wao ambao walikua wanakaribia kuhitimu masomo yao. Pia ndoto za wazazi siku zote ni kuwa ipo siku watoto wao wangefikia malengo yao ya kielimu na kuwasaidi katika uzee wao.Kwa hiyo wale wazazi walikua na kila sababu ya kupewa rambirambi zile zote.

Tujiulize tu kwa nini Wamarekani wameamua kuwapeleka wale watoto wakatibiwe Marekani kwa gharama ambayo ni kubwa sana kuliko hata rambirambi yote iliyotolewa?
Jibu ni rahisi wenzetu wanajali utu wa mtu mmoja mmoja. Wangeweza wakakimbilia kwanza kutoa misaada ya kununua Ambulance kwa ajili ya kuwahisha majeruhi hospitalini. Na tena watanzania na serikali tungewapigia na makofi. Lakini wenzetu wanaujua wazi kuwa suala la uhai na maisha ya mtu aliyeko kwenye matatizo ni muhimu na pia ni njia nzuri ya kuonyesha upendo kwa binadamu wenzetu. Hospitali au hata ambulance zinaweza zikajengwa kwa fedha za mikopo ya serikali. Na pia sio jukumu la mkuu wa mkoa kukarabati hospitali kwa kuwa hospitali zina mafungu yake ya ukarabati. Na serikali imekua ikisema kuwa ina fedha za kutosha kwenye shughuli za kimaendeleo na kijamii ikiwa ni pamoja na kutoa elimu bure.

Naunga mkono wazo la kurejesha fedha za rambi kurejeshwa kwa wafiwa.
bwana mkoa huo atafute michango mingine kwa ushawishi wake na sio kupitia mgongo wa msiba tena kwa kupiga panga bila makubaliano na wachangaji wala wale waliochangiwa wala marehemu. Hii ni dhulma kubwa kwa familia za marehemu.

.
 
yana roho mbaya aisee lakini zile rambirambi za police waliouwawa hawakuzipangia matumizi mengine.
 
Rambirambi za maafa ya Bukoba zilikarabati miundo mbinu za kijamii kama shule, zahanati , hospitali n.k ndio Sera za CCM kwa sasa
 
Rambirambi ndio kiki inayo trend bavicha.mnawazidishia uchungu tu wafiwa
Chadema waliahidi milioni 50.pelekeni basi
Tatizo la nyinyi ccm mnataka mfanye ninyi wenye kazi za kijamii kwani kuwaona wafiwa ni kosa hata nikiwa na waandishi wakutoka marekani ni kweli ccm msiifanye nchi hii kuwa ya kwenu pekee yenu
 
Hivi huyu Gambo hana hofu ya Mungu, unatoa wapi ujasili wa kugawa rambi rambi za wafiwa. Huu upinzani sasa unatupeleka bapaya
 
Back
Top Bottom