Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
WANA CCM wenzangu, hiki tunachokifanya hakina baraka za Allah/Mungu/Yehova/ Nyasaye kabisa. Hebu tulitafakari maana sidhani kama ni ubinadamu. Huu ni utapeli ndugu zangu tusiunge mkono hata kama nia ni njema kiasi gani.
Nazungumzia huu utamaduni mpya wa kukusanya pesa za rambi-rambi na kuyapangia matumizi mengine. Hii ni dhahiri Serikali yetu inafurahia majanga na mabalaa kutokea ili kupata pesa. Kwamba majanga ni dili (biashara). Hii ni aibu kubwa. Tunaona wivu wa mini na hela za rambi-rambi? Huu si utu!
Nimekutana na mzazi aliyepoteza mwanaye Arusha anaumia sana kusikia eti kifo cha mwanaye imekuwa ni chanzo cha mapato ya Serikali kukarabati Hospitali ya Mount Meru. Amelia sana mbele yangu kwenye simu.
Nashauri ingependeza basi baada ya kukusanya rambi-rambi yote hata kama ni Mabilioni Ndg Mrisho Gambo angewaita wafiwa wote pamoja na kuuza wazo hilo kwao then kuwasikiliza maoni yao. Pengine wangesema kiasi Fulani mtupe na salio ikaboreshe hospitali au kununua vitabu kwa shule zote za Arusha. Wafiwa si wajinga wangetoa mawazo mazuri. Huo ndio uongozi shirikishi na si kuwapangia matumizi pesa zao. Ndio maana nimetoa wito kwa wanasheria kuwasaidia wafiwa hawa kudai pesa hizi ni zao. Mkoa haukufiwa, Gambo hakufiwa. Wapo wazazi in person waliofiwa ndio wanaochangiwa. Daini hela hizi ili iwe fundisho kwa majanga yajayo (hatuombei).
Tukiruhusu utamaduni huu mpya wa kutumia rambi-rambi siku atatokea Mkurugenzi mwendawazimu akishatafuna hela za umma na hana namna ya kulipa ni kuhujumu njia ya reli iache njia watu wafee kadhaa au achome shule maana rambi-rambi itakusanywa naye kuzipangia matumizi alikoiba. Tusishabikie hili la rafiki yangu Gambo. Si Jema!
NASISITIZA: Wanasheria wasaidieni wafiwa kudai hela hizi maana ni zao. Ni kwa ajili ya watoto wao. Watatumia kupalilia makaburi ya wanao. Niko tayari kulipia gharama za mawakili ili tabia hii ikome Tanzania. Misiba ya watu isiwe harusi ya Serikali.
[HASHTAG]#UzalendoKwanza[/HASHTAG]. Bollen Ngeti. UVCCM Taifa