masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,408
- 14,113
Ni kweli kabisa na ndio maana kuna watu walidiriki kusema Awamu ya Tano ni ya kidikteta.Mjumbe wa NEC mkoa wa Pwani, Haji Juma anasema machache juu ya madhaifu ya Dkt. Bashiru akiwa Katibu Mkuu CCM.
CCM ilikuwa kama nyumba ya udongo iliyopigwa ripu na rangi kwa nje lakini ndani ilikuwa bado ya udongo.
Alibadilika alipo pata madaraka na kuacha alichokuamini na kulinda maslahi yake binafsi na aliyemchagua.
Dkt. Bashiru alianza kukidhoofisha chama chetu ndani na kujenga makundi yenye hatari ya ukanda.
Katika uongozi wake vikao vya CCM vilitumika kama rubber stamp tu.
Katika uchaguzi uliopita wagombea wengi walioshinda uchaguzi wa ndani ya CCM walikatwa kwa wingi kuliko wakati wowote tangu CCM ianzishwe.
Robo ya wabunge wote waliopo bungeni hawakushinda chaguzi za ndani ya CCM.
Sasa huo utakatifu wa Dkt. Bashiru unatoka wapi?
Nina mengi sana ya kusema juu ya Dkt. Bashiru.View attachment 1771052
Maamuzi yalitolewa bila majadiliano.
Ikafika muda Magufuli mwenyewe slilewa madaraka na kutamka wazi kuwa hawezi kuchukua ushauri wala mawazo ya wengine.
Tukubali, Awamu ya Tano CCM ilikuwa disaster kisiasa.