Wana CCM tuchutame, Hatujachelewa kutubu. Ona Ole Sabaya alishupaza shingo

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Kuomba msamaha sio ushamba hata kidogo, Ole Sabaya angeenda Clouds FM kuomba msamaha na kutubu angesamehewa na wananchi kwa uchafu na ujinga alioufanya huku akilindwa na mfalme niliyempigania Katika kitengo cha Propaganda ndani ya chama kwa lazima na sio kwamba nilipenda ilikuwa lazima. Sabaya angeikimbia laana ya wananchi, Angebakiwa na hukumu ya Dunia ambayo kwa sala na maombi ya wananchi waliomsamehe angeishi huko mahabusu kwa neema na mguso wa maombi.

Sabaya kwa kutembea na kivuli cha Marehamu akaenda clouds FM kujinasibu kwa maovu, kuwa ili uchafu na utekaji uendelee basi lazima CCM ishinde Hai, alijisahau kuwa yeye hana hata Biashara ya Bigijii lakini kaharibu biashara za watu za mabilioni ya shilingi.

Katika mfululizo wa watu waliofanya ubaya na uchafuzi wapo wengi sana sana, Sisi wengine tuliomba msamaha hapa na kwa wale wana JF tunaofahamiana na kukutana nina amani tele.

Wafuatao waombe msamaha kuna uchafu mwingi na upuuzi mwingi mmefanya.

Harrison Mwakyembe wakati wa sakata la Roma mkatoliki ulitumika kufanya Roma aogope kuongea yaliyomkuta.

Humprey na Bashiru, Mmeligawa Taifa pande mbili kwa kutumika wakati wa uchaguzi wa mwaka 2020 na ule wa serikali za mitaa. Lengo lenu lilikuwa watanzania wavunje msingi wa Baba wa Taifa waanze kuchukiana na kupigana mitaani, Mlichochea sana ccm wawachukie Wengine, Kama sio Utanzania wetu mambo yangekuwa yameharibika kabisa, Kuna wakati hata wana ccm kama mimi tulihisi wewe Bashiru na Mfalme sio Raia wa Tanzania mnatoka Burundi huko.

Paul Makonda na Mwigulu Nchemba. Mliyoyafanya ni makubwa zaidi, Bora Mwigulu ulikuwa huna la kufanya ukatimuliwa maana kuna maagizo yalizidi uwezo wako na Imani yako ukatimuliwa.

Nashauri iteni Press ongeeni kuwa mnaomba msamaha kwa mabaya mliofanya wakati wa uongozi wenu kwa kujua au kutokujua huo ndio ustaarabu, Karma is a Bitch.

Haya kuna siku watu watawashtaki tu, Hakuna atakayekubali damu za Akwilina, Ben Saanane, Risasi za Lissu na Azory yapite Bure.

Ole Sabaya alijisahau alihisi mfalme bado yupo, Mfalme hayupo. Tuliosoma nyakati tuliomba msamaha hapa kwa kutetea Uchumi unakua na Ajira kedekede huku tukisifia miradi ni pesa za ndani wakati tunajua nchi ipo chali na taabani lakini hatukuwa na jinsi ilitupasa hayo yafanyike.

Kwa sasa tunashindwa hata kutoa analysis za Uchumi kwani sisi wenyewe tulishabikia sheria mbovu za kuficha takwimu na kubana uhuru wa vyombo vya habari.

Labda Mama Samia akirekebisha sheria Itakuwa rahisi kufanya uchambuzi hapa, Sheria bado ni zile zile za Mfalme ambazo tulizifanyia Propaganda kuwa nzuri, Sheria zilibana takwimu na access ya taarifa za Serikali.

Mama Samia ahimize mawaziri kupeleka miswada ya mabadiliko ya sheria Bungeni za Mfalme.

Time will tell
 
Mtajitokeza mmoja mmoja huko mapangoni hadi muishe!

Ukombozi wa taifa ulianza tarehe 9/3 ukahitimishwa tarehe 17!

Vipi buku 7 zitaanza kutoka lini ili muanze kumuita Samia Chuma?
 
Wameshazoea kushupaza shingo dawa yenu kuwafanya kama Diamond kule twitter.
 
Mtajitokeza mmoja mmoja hadi huko mapangoni hadi muishe!

Ukombozi wa taifa ulianza tarehe 9/3 ukahitimishwa tarahe 17!

Vipi buku 7 zitaanza kutoka lini ili muanze kumuita Samia Chuma?
Ni uhalisia mambo yalikuwa hovyo hapo kati

Hata sisi tuna ndugu maelfu huko ambao ni wa mbali lakini mfumo uliharibu maisha yao

Tusiangalie sana matumbo yetu kuna kesho ya Wengine pia
 
Ni uhalisia mambo yalikuwa hovyo hapo kati

Hata sisi tuna ndugu maelfu huko ambao ni wa mbali lakini mfumo uliharibu maisha yao

Tusiangalie sana matumbo yetu kuna kesho ya Wengine pia
Magu alikuwa kiongozi muovu na dhalimu, tuombe taifa hili lisiangukie tena mikononi mwa kiongozi muovu wa aina yake. Yaani mlikuwa mnatumika kwenye siasa chafu mpaka ilikuwa aibu. Kibaya zaidi watu waelewa ndio walikuwa wa kwanza kumsifia yule dhalimu.
 
Magu alikuwa kiongozi muovu na dhalimu, tuombe taifa hili lisiangukie tena mikononi mwa kiongozi muovu wa aina yake. Yaani mlikuwa mnatumika kwenye siasa chafu mpaka ilikuwa aibu. Kibaya zaidi watu waelewa ndio walikuwa wa kwanza kumsifia yule dhalimu.
Alikuwa muovu kwa wizi, mafisadi na wauza madawa ya kulevya mkuu ila moto waliupata na watamkumbuka mpaka kufa kwao au na wewe ni mmoja wao mkuu!!?
 
kwa Samia yeye wakati huo yanafanywa hasa hayo ya siasa za kina pole pole na bashiru hakunufaika au hakuwa mwana ccm?
 
Alikuwa muovu kwa wizi, mafisadi na wauza madawa ya kulevya mkuu ila moto waliupata na watamkumbuka mpaka kufa kwao au na wewe ni mmoja wao mkuu!!?

Narudia tena, alikuwa mtu muovu na dhalimu mkubwa. Toka lini jizi la kura likapambana na wizi? Nitajie fisadi yoyote aliyefungwa maana alisema mahakama ya mifisadi ilikosa wateja.
 
Dah, Taifa lilipitia bonde la uvuli wa mauti.
Nadhani ilikuwa ni lzm tupite huko Ili tuje tukae SAwa.

Prophet Bushiri prophecies on Tanzania 2015 google hii kitu alitabiri kwamba

1.John ndie mshindi wa uraisi.

2.Tanzania itakumbwa na tetemeko.

3.Hali ya uchumi wa Tanzania itakuwa mbaya mbaya KILA mwaka.

4.Anaona anga la Tanzania limejaa damu KILA mtu ni shahidi mauaji ya kihistoria watu wameuliwa, wasiojulikana,mauaji kibiti,mapanga kwenye chaguzi,watu kuuliwa na police yaani ya umwagaji damu iliingizwa kutoka kwa PAKA pale uswahiba ulipopamba moto.

Tabiri hizi zilileta hali ya kurushiana maneno Kati ya Gwajima na Bushiri kabla ya uchaguzi October 2015.
 
Back
Top Bottom