Viper
JF-Expert Member
- Dec 21, 2007
- 3,667
- 1,401
Mapokezi ya kale ya hayo makabila tajwa hapo juu yaliweza kuchukua sehemu moja ya Fasihi simulizi ambayo ilitumbuiza, nasihi, taanasi, sherehesha, kutoa taazia na kwa malengo mengineyo. Maarufu zaidi katika mapokezi hayo ni matumbuizo ya watoto wakati wa faragha (mapumziko) na wanapojianda kwenda kulala Wazee wa kale wa Kiswahili walikuwa na namna nyingi za kuwatumbuiza watoto wao. Kati ya namna hizo ni kuwaimbia vipokeo, kuwatolea hadithi, mashairi na nyimbo mbali mbali nyakati za jioni Wakati mwengine watoto na vijana wa marika mamoja wanapopata nyakati za faragha hujitumbuiza kwa vipokeo na michezo kadha wa kadha ...
Kwa hizi jamii za washwali halisi pia huwa nafurahishwa sana na kiswahili chao ni kitamu mnoo ...
UKALE WA MAPOKEZI
Bado hakujajulikana ukale hasa wa mapokezi haya. Kulinganana baadhi ya mapokezi yanatufanya tutoe makisio fulani juu ya tarehe ya mapokezi hayo. Kwa mfano
Mapokezi haya yanakisika kuwepo tokea karne ya kumi na tano ambapo wareno na wazungu wengineo walikuwa wameshawasili sehemu za Mvita. Halikadhalika, kutajwa kwa neno "shilingi" inatueleza kuwepo kwa matumizi ya sarafu katika kame kumi na nane au pengine kabla yake. Mfano wa mapokezi yenye kutumia neno hilo Ia sarafu tulilo nukuu hapo juu ni huu ufwatao:Peepepepeta
Wazungu wawili wapita
Wan kovu za kitwa
Wakitoneshana wateta
Sara ntokapi na ulingo
toka n'komani Baulingo..."
"Shilingi yangara yaua (kipokezi hurudiwa mara mbili),
sijauona mpili pili na maua yake mchikichoo...."
Yaamkinika pia ,baadhi ya mapokezi haya ni ya jadi najadi Katika baaadhi ya sababu zinazotufanya tudhanie hivyo ni kule kuwepo kwa istilahi za kale na/au zilizo sahaulika3.
[h=1] MAUDHUI NA MALENGO YA MAPOKEZI
[/h]
Mapokezi ya watu wa kale yalikuwa na malengo na maudhui mbalimbali. Yapo yaliyodhamiriwa kutumbuiza, kufunza vijana, kuwashajiisha,na kuwaongoza wawe ni watoto wema wenye nidhamu. Mapokezi haya yalitumika nyakati za kupasha jando, harusi, mavuno na wakati wa huzuni na misukosuko. Kisiwa cha Mvita sasa chafahamika zaidi kwa jina Ia Mombasa Hapa ndipo mahali mwandishi alipozaliwa na alipokulia. Maandishi mengi ya kale yametumia neno Mvita kuliko jina lenginelo. Hii ni moja ya sababa muandishi amependelea kutumia jina hilo katika makala haya. Natoashukurani nyingi kwa dadaangu Bi. Leyla Ali Abdalla (b. 1962) wa Magongo, Mombasa, ambaye alitumia wakati wake mrefu kunisimuliya na kunitolea kimahadhi baadbi ya mapokezi haya, 10 Desemba, 1998.. 3 Mahojiano yangu na mzee wangu Shelkh Ahmad Nabahany, mtafiti mashuhuri wa lugha ya Kiswahili, Mombasa, Swahili Cultural Centre 21 May,1998.
MAPOKEZI YA WATOTO NA MICHEZO YAO
Watoto na vijana hujumuika pamoja kwa matumbuizo na taanasi mbali mbali hususan nyakati za jioni Mara nyengine katika sherehe rasmi, wakunga na wavyele hukusanyika kuwaongoza vijana hasa wanaobaleghe na wanaokaribia kufunga ndoa Michezo marufu ya watoto wa Kiswahili tangu zama hizo ni pamoja na kucheza kibe ndolee, ulimbo, tega n'kutege, blada, nusu mkalili, kuruka kamba, Kurusha tiara,mieleka, kirumbizi, kupiga goma (ya ropa), na michezo mengineyo. Nyakati nyigine wavyele wanapopata faragha huwatumbuiza watoto wao kwa qasida, mashairi, haditbi, vitendawili na mapokezi mbali mbali. Yafuatayo m baadhi ya mapokezi hayo:
Bibi songa nyele
Bibi songa nyele shanuo la nini?
Kitwa chaniuma dawa yake nini?
Ponda tangawizi upake nyusini,
Mahaba sindano ya choma maini
Aliyomi
Al yomi aliyomi alimsabaha ilyomi,
Kuna mnazi mmoja wapanda watu watatu
Akianguka mmoja, Hamadi mwana wa watu.
Ndege ruka ndege ruka na barua mdomoni
Ukufika ukafika mbwagie mapajani.
Usinione nimekonda ukadhani kwetu sili
Nala mtele kibaba na nyama nusu ratili
Kitoria baa kitoria baa
Kahela kahela kajumbaka.
Pepeta
Peepepepeta
Wazungu wawili wapita
Wan kovu za kitwa
Wakitoneshana wateta
Sara n n'tokapi na ulingo
Natoka mkomani kunwa tembo
Kesho n'tashuka Marekebu
Na zinga lamoto Ia dhahabu.
Sukuma kidau tunende
Kwa Bwana Hamadi Madende
Tukampokonye maembe
Na wali mtamu kwa tende
Mariamu na mpishi wake (Kipokezi hiki hurudiwa mara mbili).
Ukuti wa mnazi
Ukuti ukuti
Wa mnazi wa mnazi
Ukingia upepo
Wan tetema Wan tetema
pia hizo kabila tajwa hapo juu ni watani mfano angalia hili pokezi hapo chini
Msegeju
Msegeju ana ngombe
Nami n no ngombe zangu
Namwambia tutanganye
Hataki
Kwa heri nenda zangu.
Mapokezi ya Harusini
Bibi harusi ndoo kaole
Kaole mgeni kangia
Mgeni kongo
Aya eei Mgeni kangia.
Hongera mwanangu ee
Hongera nami nihongere mwana eei
Mama uchungu mwana uchungu Eei
Nyamala mwonangu siliye oyee
Tumbo la uvyere linaumo mno eei
Linauma mno hoyee!
Sema yuwapi mamake harusi aje hapa
Tuhangaike naye (kipokezi)
Na ndugu yake harusi aje hapa
Tuhangaike naye
Na rafiki yake harusi aje hapa
tuhangaike naye...
Aje amfunze mwari
Asije kufedheheka
Amwitikie mumewe kwa kila anachotaka.. 4
[h=3] Mapokezi yanayotolewa na tanaasi
[/h]Yapo mapokezi ambayo watoto wa mvita, wadigo & wasegeju huyatowa huka wakitaanasi u kucheza michezo mbali mbali. Baadhi ya taanasi hizo m michezo mbaiimbaii nayo huchezwa hivi: 4 Rajiisha maelezo ya nambari 2 (mbili) hapo juu.
Ulimbo
Katika ulimbo wasichana hufanya mviringo wakishikana mikono. Binti yeyote hutajwa na kuingia kati kati ya boma akicheza kwa maringo huku akiimbiwa
Ulimbo bayoyo baa
Binti fulani piga goti tukuone
Bingili bingili mpaka pwani
Barua kwa baba
Kijana hushika barua au mfano wake na kuzunguka nje ya boma Ia waliokaa chini huku akiimba Napeleka barua kwa baba. Kijana huyo atazunguka huku akilenga mtu wake kimoyomoyo. Anapomkaribia atamgusa na huku akitimka mbio. Aliyeguswa naye atamfurusha huyo mwenye barua hadi amshike. Akishindwa kumshika mwenye barua basi alochukua yeye barua na kufanya kama mwenye barua wa kwanza alivyofanya. Mwenye barua huimba mapokezi yake hivi:
Napeleka barua kwa baba, ikanipotea ndiani(Hurudiwa mara mbili) Si wewe, na si wewe, ni wewe... (mwenye barua akifanya uchaguzi wake).
Kipara ngoto
Anaye nyoa nyele (kipara) hugolewa na wenzake na kuimbiwa:
Kipara ngoto, maji yamoto Ukimpata mtie ngoto.
[h=3]Kidengele
[/h] Anaye onaekana na kitu chepesi kama vile sufi au unyoa utosini mwake pasi na yeye mwenyewe kujitambua, hugolewa na wenzake na kuuimbiwa:
Mtu wangu an kidengele Kesho tam nyoa nyele.
Matezo ya simba
Katika mchezo huu mmoja wa wanadi katika vijana atajifinya ni baba anaye nadi kuwatahadharisha watoto wake juu ya udhalimu na uvamizi wa simba. Mnadi huyo kumbe nimvamizi pia. Hivyo basi atanadi na wenziwe kumuitikia mnadi anapofika pale kwenye msemo usemao nashuka chini mnadi ataruka na kuwatimua mbio vijana wenziwe hadi amshike mmoja wao. Mapokezi ya matezo ya simba ni haya yafuatayo:
Mnadi: Watoto wangu eeh!
Wapokezi: Eeeh!
Mnadi: Mimi baba yenu
Wapokezi: Eeeh!
Mnadi:Sina nguvu tena eee ya kuua simba.
Wapokezi: Eeeh!
Mnadi:Simba m mkali eeh!
Wapokezi: Eeeh!
Mnadi:Aliua mama eels!, akaua nyanya eels!, akaua ndugu eels! akaua...
Wapokezi: Eeeh!
Mnadi: Nani kamata?
WapokeziMimi kamata, kama mume kweli kama mke kweli sishuka chini
Mnadi: Haya nashuka chini(Mnadi ataruka na kuanza kuwatimuwa mbio wenzake hadi amshike mmoja wao).
Kizuizui
Mchezaji hufungwa macho (kizui zui) zw) kwa lengo Ia kushika mtu katika kundi la wachezaji wenziwe. Anaye shikwa naye atafunga kizuizui
Mpunga na nyama na uliwe
Mpunga na nyama na uliwe ni mchezo ambao vijana hukusanya mlima wa mchanga na kijiti Kikawe kwa juu yake. Wachezaji huwa wawili au watatu. Kila mmoja huvuta mchanga polepole upande wake kwa vidole vya mikono miwili hadi kijiti kianguke upande wa mshindi
Hali ya totore
Wale wanaoshindwa katika michezo mwisho huimbiwa Waliyataka wenyewe, haliya totore. ilobaki n shauri yao
[h=3] Ngoma
[/h]Zifuatazo ni baadhi ya ama ya ngoma zao maarufu zilizokuwa zikipigwa kisiwani Mvita (mombasa kwa sasa) pwani ya Tanga "wadigo & wasegeju" & waunguja hadi kufikia wakati wa uhuru Ngoma hizo za kale zilizosifika ni Kirumbizi, Twari la Ndia, Vugo Lele mama, Chakacha Mdodoki, sengenya Kimanyema Mabumbumbu, Namba, Gwaride, Twarabu, Sumsumiya, Mwaribe, Sindimba, na Mwanzele. Ngoma chache mno bado zingaliko katika maeneo ya pwani katika jamii hizi za waswahili ..pindi makala haya yalipotayarishwa na mwandishi. Baadhi ya ngoma tulizonukuu hapo juu zimekufa baada kukemewa na kupingwa na mashekhe na wanazuoni Afrika Mshariki
Makala haya yamejaribu kwa kiasi fulani kutoa maelezo juu ya mapokezi na taanasi mbali mbali za hayo makabila . Mapokezi haya ambayo yanakaribia kutoweka na mengine kusahaulika kabisa yaliweza kutumbuiza, kuongoza, kufunza, kushajiisba, kufurahisha na kuhuzunisha hadhirina mbalimbali. Mapokezi haya yaliweza pia kujenga maadili, dasturi na adabu za watoto wa Kiswahili. Fasihi simulizi kama hii iliongeza ladha utamu wa lugha na kukipamba Kiswahili Hapo ndipo tukasema kila msimu ukija huja na yake