Wamiliki wa Mitandao ya Kijamii huwa wanajiingizia kipato katika namna tatu na kila namna inategemea Ukubwa(idadi ya watumiaji) wa Mtandao husika
1.Kwa Mitandao ya Kijamii michanga Kama Jamiiforums huwa inajiingizia pesa kwa njia ya AdSense (Mara nyingi Google AdSense)
Mmiliki wa Mtandao anapokea Codes maalumu kutoka Google ambazo zitaonyesha matangazo (Personalized ads) katika Website yake,na atalipwa pindi watumiaji wa Mtandao wake watakapo click hizo ads(Pay per click)...
Ukiacha Third party ads Kama za Google,njia nyingine ndogo ndogo ni Donation kutoka kwa Members wenyewe,Mara nyingi hii huwa ni katika forums au organization yoyote itakayo fadhili huo Mtandao
Nafikiri kwa Jamiiforums,inatumia hizo njia mbili za mwisho
2.Njia ya pili niku promotes Ads
Hii haina tofauti na njia ya kwanza ila hufanywa katika namna tofauti
Watumiaji wa Mtandao wako wanakuwa na uwezo wa kufungua Account na kupost matangazo Yao katika Mtandao huo huo,na mmiliki wa Mtandao atachukua commission kwa kila Ads itakayo kuwa clicked
Njia hii hutumiwa na Social network yenye watumiaji wengi Kama Facebook, YouTube na Instagram
3.Njia ya mwisho ni Big Data
Na hapa ndio utajiri wa mtu kama Mark Zuckerberg unapokuja
Chochote unacho post Jamiiforums,iwe Email yako, comment,picha,au post ni data
Data Kama data yaani Email yako au post yako haina maana yoyote
Ila Data hizi zinapounganishwa kwa pamoja tunapata Information kuhusu wewe
Data +Data +Data +.......Data = Information
Mfano
😀ata ya kwanza ni Email yako, Email inaweza kuwa synced na device yako (Simu au PC)
So Email yako inaweza kutupa data ya pili ambayo ni Ip address ya Simu au PC yako
Then kwa kutumia Ip address yako tunaweza kukusanya list ya website unazopenda kuperuzi na content za site hizo
Then kwa kutumia mlolongo wa hizo data pamoja na data nyingine nyingi ndogo ndogo
Tunaweza kupata information kamili kuhusu wewe na vitu unavyopenda kuviona Mtandao
Hii itatusaidia kujua ni Aina gani ya ads zitakazo onyeshwa kwenye Device yako
Kama unapenda kuperuzi website zenye content za afya Basi Kuna uwezekano mkubwa uka click matangazo yanayohusu Afya
Na hapa ndio utagundua kwanini ni rahisi Sana kukutana na Tangazo Facebook, Instagram au YouTube linaloendana na kile unachotaka au kutamani (Japo sio Mara zote)
Sasa kwa Social network kubwa Kama Facebook yenye watumiaji zaidi ya Billion 2
Ndio wapotumia Advantage hii kuuza Information zako kwa Online marketers au Kutengeneza personalized Ads
Kuhusu Mitandao ya Kijamii kulipwa kulingana na Mb unazotumia ni jibu la Kijinga kuwahi kulisikia
Sent using
Jamii Forums mobile app