Wamiliki magari wa Zamani vs wa Sasa

KndNo1

JF-Expert Member
Oct 26, 2021
627
2,023
Kuishi kwingi ni kuona mengi.. Nimeona mengi yakibadilika kwenye ununuzi wa magari..

1. Enzi hizo watu waliokuwa kwenye circle yangu hakuna aliyenunua gari kwa mkopo.. Gari tulidunduliza hela mpaka tukavuta..

2. Magari yetu ya kwanza almost 85% yalikuwa ni pick ups.. Hakukuwa na mnunuzi wa Crown..!
Pick-up inakuwa na bomba nyuma.. Unaenda gerezani kushona turubai..!

3. Wengi wetu tulinunua gari la kwanza tukiwa na miaka 30+..
Leo hii vijana wadogo 25 wanapush vyuma vya moto..!

4. Gari zetu zilikuwa mpya aisee.. Mimi 1994 nikipata Nissan Pickup model ya 1991..yaani gari ya miaka 3 nyuma.. Leo hii sidhani kama ninahiyo hela ya kununua pickup ya 2019.. Tofauti na leo magari mapya machache..!
 
Sure aisee.. Ndio maana hata gari zilikuwa zinadumu.. Kukuta gari imegongwa upande sio rahisi.. Nidhamu na kufuata sheria barabarani.. Siku hizi wachomekeaji wengi..
Suzuki Samurai SJ410..!
 
nyie mnaongelea mbali, 2010 tu hapa arusha sikuwahi kuona foleni ya magari ila siku hizi mpaka arusha kuna foleni, maboda boda ya kutosha.

yaani saivi mda wowote unasikia pu side mirror haipo alafu bodaboda anaamsha
 
Back
Top Bottom