Wamiliki huharibiwa biashara zao na wafanyakazi wao

Black listed

Senior Member
Apr 6, 2023
182
252
Mara nyingi wamiliki wa biashara (kampuni) wengi huwaamini wafanyakazi wao kuendesha biashara zao katika idara tofauti za kampuni husika.

Wafanyakazi hawa huharibu biashara za mabosi wao either kwa bahati mbaya (makosa ya kibinadamu) au kwa kukusudia. Makosa ya kukusudia huwa wanafanya kwa interest zao bila kujali kama wanamuumiza mwajiri wao au la.

Unamtendea ndivyo sivyo mteja asiye na tatizo lolote huku humwambii kosa lake, je, huu ni uungwana? Mteja anaishia kunung'unika tu na hawezi kupata msaada wa utatuzi wa tatizo alilosababishiwa maana bosi yuko mbali, hawezi kumfikia!

Sasa mteja akiondoka, ataendelea kunung'unika, na safari hii manung'uniko yake atayaongea kwa watu wengine. Hii itapelekea watu wengi kuanza kuwa na wasiwasi juu ya huduma zitolewazo na kampuni husika!

Hapa utakuta watu (wateja) huanza kufikiria kwenda kupata huduma mahala pengine (competitors) na wewe kubakiwa na wateja wachache sana, maana wateja hufuata huduma bora.

Nyie wafanyakazi, msimuharibie bosi wenu biashara yake, kwani ametumia gharama kubwa " ku-establish brand yake", halafu ninyi kutokana na interest zenu tu eti huyu simpendi namfukuza, mnamharibia biashara bosi wenu!

Wakurugenzi, kuweni makini na baadhi ya wafanyakazi wenu. Baadhi wapo hapo wanacheka na wewe kinafiki tu lakini akilini mwao wapo tofauti na unavyowaona usoni!

Biashara ni wateja (wengine wanasema mteja ni mfalme), bila kuwa na wateja kampuni itakufa. Unaweza kusema "nina wateja wengi, hata akiondoka huyu nitabaki na wengi", huyu anayeondoka anaweza kuondoka na wengi!
 
Back
Top Bottom