Companero
Platinum Member
- Jul 12, 2008
- 5,604
- 1,704
Mngetekeleza walau asilimia 50 tu ya mapendekezo ya hizo PhD na Ripoti za Utafiti yakinifu wale kusingekuwa na matatizo mnayoyaongolea kana kwamba chanzo chake ni mfugaji - ninyi mnaona sawa viongozi kujigawia ekari mpaka 1,000 huko Kilosa na Mvomero ila mnaona shida wafugaji kujifugia mifugo yao kwa amani bila kubugudhiwa na dola na wanamaendeleo uchwara wenye nadharia walizoazima kutoka kwenye jamii ambazo hata hawazijui? Suluhisho ni kuwaachia wafugaji maeneo wafuge kwa amani kwa kutumia mifumo yao ya transihumansi ambayo imetunza mazingira kwa karne na karne kabla hamjawavuruga na elimu yenu ya kimagharibi inayojiona inajua kila kitu na kutuvurugia ardhi ya nchi yetu na misaada yenu isiyo endelevu kwa kuwa haijali hali halisi ya mazingira yetu!