Wamasai na ngoma ya "esotho????"!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wamasai na ngoma ya "esotho????"!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Dark City, Sep 12, 2011.

 1. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ghafla bila kutarajia, nimejikuta naangalia kipindi cha Shajara kupitia TBC1, kilichokuwa kinaongelea ngoma ya kabila la Wamasaia inayoitwa esotho (samahani kama nimekosea neno hilo). Sikuwahi kuisikia hii ngoma na kama nimewaelewa vizuri, ngoma hii inahusisha yafuatayo.
  -Ngoma hii wanacheza watoto na vijana kuanzia miaka 8 na kuendelea, na huchezwa kipindi ambacho wanyama wana malisho ya kutosha.
  -Lengo lake (sina hakika kama ni rasmi) ni kuwapa nafasi ya kujifunza kufanya ngono!!
  -Morani mmoja anaweza kupendwa na wasichana hadi kumi....na wote atafanya nao ngono peke yake...Na kumetolewa ushahidi kwamba kama Morani huyo kapata lishe ya kutosha (maziwa na nyama) anaweza kufanya ngono na wasicha hadi 5 kwa usiku mmoja. Wanajikusanya kwenye boma moja na hawaoneani wivu!
  -Msichana alihakikisha anaenda kwenye kundi ambapo mchumba wake hayupo
  -Madhara yake kwa ni pamoja na msichana kupata mimba ila kwa siku za karibuni, ngoma hii inaongeza uwezekano wa kuambukizana ukimwi. Inasemekana hakuna matumizi ya kondomu katika ngoma hii!

  Inawezekana yapo mengine mengi ila hii ni uthibitisho mwingine kwamba nchi yetu ina utajiri wa tamaduni ambazo tunaweza kuzifanyia mabadiliko chanya na kuzitumie kiuchumi. Bahati mbaya watu wanaangalia baadhi ya tamaduni ambazo zilikuwa na nia nzuri kwa mtazamo hasi!
   
 2. m

  masssaiboi JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2011
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 637
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 33
  hii mpya, kijiji gani hicho niende kavekesheni kidogo, nimpe mama hausi break.
   
 3. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Nimeona kwenye TBC1 na kwa kweli sikujua ni wapi yalikofanyika mahojiano yaliyokuwa yanarushwa. Mtangazaji alikuwa Amina Molel na amehoji watu wa rika tofauti.

  Ngoja tusubiri wadau wenye taarifa watueleze...Hata hivyo nakushauri usiione hii kama fursa ya ngono rahisi bali kitu kinachoweza kutumiwa positively. Kama ni ngono za fasta fasta kwa nini usiende kwa machangu??
   
 4. m

  masssaiboi JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2011
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 637
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 33
  Nope, Nataka nikajifunze utamaduni mpya na ngoma za kijadi ambazo sikuzipitia huku A-town
   
 5. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Hiyo kabla ndiyo yenye mambo ya asili mpaka hivi sasa Africa nzima na bila kukosea maana cjapata hata kuona hicho kipindi kwa sababu ya NGELEJA kutopatika huku kwe2 kwa muda husika lakini matukio kama hayo sanasana yapo kanda ya Kaskazini. Na ngoja wadau waje humu.
   
 6. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #6
  Sep 12, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  <br />
  <br />
  Hata mimi nimeicheki TBC one.
   
 7. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #7
  Sep 12, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hata mimi nasubiri wadau wenye kujua vizuri watupe uhondo zaidi,

  Otherwise itabidi tuombe msaada kwa washirika kutoka A-town...Naamini akina Preta, PJ, Wiselady hawatakuwa wachoyo wa elimu...!!
   
 8. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Nimependa avatar yako....I wish ingekuwa kweli.....ukizingatia matikiti maji yanarudisha heshima ya usiku!!
   
 9. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #9
  Sep 12, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Wamasai wana the most elaborate dancings' kuliko kabaila lolote lile ambalo nimefuataila kwa karibu.... Bahati nzuri i am into culture and its music (thou kwa kubabaisha hivo hivo...) nimewahi sikia hii dance ulotaja hapa... thou sina hakika saana na jina ulotaja for ninajua kua kuna dance yao ina process ndefu kweli (nimesahau jina ila nikilisoma nakumbuka) inayo husisha baadhi ya mambo ulotaja hapo juu.... Hio dance huenda sambamba (baada hasa ya kutoka jandoni wakirudi tu) saana na moja ya dance maarufu kwa jina la "Adumu" - ambayo hulenga kutengeneza Man out of boys... yaani sio tu awe mtoto wa kiume, bali awe na sifa ya uanaume... Hio ulotaja ni moja ya dance hufuata badae....
   
 10. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #10
  Sep 12, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mbona umeishia katika kati kati ADii,

  Nilikuwa naanza kuvuta kasi kupata uhondo wa hiyo Adumu dance kabla ya Esotho......

  Nashukuru kwa kutuongenzea dimension katika kudadavua hii mada tamu....

  Napenda sana ngoma zetu na nitafurahi wenye uelewa mpana wakiacha kutubania wakatupa shule...!!
   
 11. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #11
  Sep 12, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Ukifuatilia dance zao wamasaaii kila moja ina maana yake... nisiku nyingi saana nilisoma hizo vitu but viko soo interesting, alafu majina ya dances zao kazi kweli kukumbuka for wana dances za kila stage.... iwe kwa wanawake ama kwa waume... Hivo DC hapo nashindwa la kuongezea zaidi, ila tu kuwapongeza kua pamoja na mabadiliko yoote haya bado wamejitahidi saana ku maintain culture yao....
   
 12. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #12
  Sep 12, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ahsante sana Rafiki....,

  Ngoja tusubiri wadau wa mambo hayo watupatie uhondo zaidi!

  Ubarikiwe sana.

  Babu DC
   
 13. Monasha

  Monasha JF-Expert Member

  #13
  Sep 13, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 509
  Likes Received: 297
  Trophy Points: 80
  Hapa mmenigusa kwa kweli..
  Kabla sijasema chochote, Mimi ni mmasai tena yule wa asili kabisa. Kwetu Ngorongoro.
  Kwanza nashukuru kwa mtoa mada na nakupongeza vilevile kwa kuwa karibu na masuala ya utamaduni wa nchi yetu.
  Naomba nikusahihishe kidogo.
  Siyo Esotho ni Esoto. Esoto siyo Ngoma bali ni utamaduni tu. Esoto maana yake ni Makutano ya morani na intoyie(wasichana) bila kujali umri wa msichana. Nini maana ya msichana kwa kimasai?? ...Ni wale wote ambao hawajaingia jandoni, kama ambavyo mnajua kwamba wamasai mpaka watoto wa kike wanafanyiwa tohara. Lakini msichana akishaingia tu jandoni basi anatengwa kwenye kundi hili la kwenda kujumuika huko Esoto.
  Kwa hiyo esoto inahusisha vijana kwa kiume yaani morani kama ulivyosema na hawa mandito yaani wasichana. Huko wanaenda kucheza ngoma mbalimbali. Pia siyo siri Ngono ipo kwa wingi. Hapa ndipo wasichana wengi wa kimasai wanapopoteza usichana wao.
  Lakini kiasili Esoto haikuwa ni chanzo cha watoto wa kike kupata mimba ingali bado wadogo. Msichana kwa mila ya kimasai kupata mimba wakati bado hajafanyiwa tohara, ni jambo la aibu sana kwake na familia yake pia. Zamani msichana akishafanya kosa kama hili, anaweza hata kutengwa na jamii kabisa. Walichokuwa wanafanya kuonyesha ukali juu ya hili suala la mtoto kupata mimba ni kwamba mtoto yule(msichana) anapelekwa porini pamoja na ndama jike halafu wanafungwa kwenye mti. Wanaachwa kwa usiku mmoja halafu kama msichana ndo kachukuliwa na wanyama wakali basi inakula kwake na ndama anarudishwa home. Vilevile kama ni ndama ndo kaliwa basi mtoto atapona na kurudishwa nyumbani. Hiyo ilikuwa zamani sana. Kwa sasa kitu kama hicho hakuna wakuu.
  Esoto baada ya milipuko ya magonjwa nayo imeanza kufifia sana japo bado ipo katika baadhi ya maeneo. Na kama mkuu ulivyosema ni kweli esoto huwa inafanyika nyakati za usiku hasa wakati wa masika ambapo kuna watu wana shibe kwao na kwa mifugo vilevile. Huwa ni kama vile mkulima anapotoka shambani na kwenda pengine baa kujiburudisha baada ya kazi nzito japo si nzuri sana. Hapa (esoto) ndo mahali ambapo vijana wa rika moja yaani morani hukutana na kuenjoy na wasichana wao. Wanaenjoy ngoma na ngono pia.
  Hayo ni kwa uchache mkuu. Ukitaka nirudi nitarudi kadiri ya maswali yenu..

  Yapo mengi ya kueleza kama nitapata nafasi.
   
 14. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #14
  Sep 13, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  wamasai nowdays washakua wahuni, wakifika town wanazitupa mila zao kabisa, hawa watu wa ajabu sana!
   
 15. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #15
  Sep 13, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ahsante sana Mkuu Zakayo,

  Kuna kitu bado sijaele na naomba unisaidie zaidi. Kwa maelezo yako esoto inahusisha morani na intoyie (wasichana wadogo kabla ya kwenda jandoni).

  Kama naelewa vizuri...morani anakuwa keshaenda jando...sasa inakuwaje morani anayekuwa keshaenda jando aambatane na wasichana wadogo?

  Halafu unasema haikuwa chanzo cha mimba...hapo una maana kwa sababu wasichana walikuwa wadogo sana au kulikuwa na mbinu za kuzuia mimba. Tafadhali usituchoke!
   
 16. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #16
  Sep 13, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Suala la uhuni wa mjini siyo la wamasai peke yao...Hata watu wa makabila mengine wakifika town wanabadilika. Kwa hiyo wamasai hawawezi kuishi kama wako kijijini wakati wako town!
   
 17. Monasha

  Monasha JF-Expert Member

  #17
  Sep 20, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 509
  Likes Received: 297
  Trophy Points: 80
  Kwanza samahani kwa kuchelewa kukujibu ndugu.

  Ni jadi yetu Morani kucheza na kutumia muda mwingi na wasichana. Hata kama akiwa ameoa. Kwa hiyo si jambo la kushangaa kwa hao walioingia jandoni kuendelea kuspend na wasichana.
  Simaanishi kwamba wasichana hapa wanakuwa wadogo sana. Ni kwamba wanatumia mbinu za asili kuzuia mimba. Mbinu hizo ni pamoja na kufuata kalenda....nadhani unanielewa kaka. Mama pia huwa karibu na mwanaye ili kuepuka janga hili la kupata mimba mapema ingali mwanaye ni msichana bado.
   
 18. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #18
  Sep 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Mkuu zakayo mie naishi kiteto. Kuna siku tulienda kwenye ngoma kama hiyo ilikuwa inachezwa kwenye mji wa mzee mmoja alikuwa ana usinga kuonyesha kuwa yeye ndiye mwenye mji. Pale tulikuta morani wengi wanaimba na kucheza huku wameongozana wa wasichana. kila baada ya mmorani katikati kulikuwa na vibinti viwili au vitatu. Kuna mtu alituambia kuwa kuna wakati, msichana mmoja na morani mmoja huwa wanafanya mapenzi huku wasichan wengine wakiwaangali hadi jamaa anapokojoa then wanatawanyika. Je ni kweli hili la mvulana na msichana kufanya ngono huku wengine wakiangalia live?
   
 19. c

  charndams JF-Expert Member

  #19
  Sep 20, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 437
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  Jamani napita. nitarudi baadae
   
Loading...