Wamama naombeni mnijibu hili!

Wamama naombeni mnijibu hili!

Nyalotsi

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2011
Posts
6,989
Reaction score
5,066
Nini huwa kinawajia vichwani mwenu pale mtoto wako wa kiume anapokutambulisha mchumba ambaye wewe hujapendelea? Ni kwanini nyie ndio huwa mnakuwa na vikwazo kuliko kina baba? Akiwa ni binti yako ndio anawekewa vikwazo hivyo wewe utajisikiaje?

Nina mdogo wangu kapendana na Dada mmoja wa Arusha na ana mpango wa kumuoa.

Juzi mwezi uliopita katoa utangulizi kwa mzazi atarajie mgeni atakayekuja kutambulishwa.

Swali la kwanza lilikuwa, kabila gani?

Walipoambiwa anatoka Arusha mama akaanza kufoka na kutoa mifano ya watu waliooa huko na maisha yao yalivyo.

Mimi nilichojiuliza, mbona hata mtu mwenyewe hawamfahamu?

Mbona wameanza kumchukia mtu wasiyemuona?

Hivi ni nini huwa mnahofia?

Kwa kizazi cha sasa kumpata mtu unayehisi ni sahihi wa kabila lako ni suala ambalo limekuwa gumu kidogo, kwa nini bado wamama wanalazimisha?

Dogo aliwahi kupendana na binti wa kabila letu lakini alimtenda vibaya mpaka akapoteza mwelekeo. Naombeni mnifungue akili yangu.
 
Rafiki wazazi wetu walio wengi wana desturi hizo kwasababu hata enzi zao wao wakiolewa kulikuwa na ile hulka kwamba watu wa kabila fulani si zuri kuoa n.k kwahio hio fikra bado wamebaki nayo.. mimi mama yangu mpaka leo hii ana tabia hizo na anataka anichagulie mume,nikimpa green light mbona atapiga vigelegele,wamama wana ile tabia ya kuwa overprotective kwamba wanajua yaliyobora kwa watoto wao aidha awe wa kike au wakiume!Na kama kawaida ya wanawake wote wanapenda kuongea mpaka dini zimesema; kwahio asipopata atakalo lazima atabwabwaja sana tu!
 
Wazazi ni sehem ya maisha yetu.ukiwa mtu mzima mzazi anakuwa na nafasi ya kukushauri tu sio maamuzi...
Angalia nini anashaur maamuz yabaki kwako..ukiyumba kimsimamo sometimes itakukost.
 
Wazazi ni sehem ya maisha yetu.ukiwa mtu mzima mzazi anakuwa na nafasi ya kukushauri tu sio maamuzi...
Angalia nini anashaur maamuz yabaki kwako..ukiyumba kimsimamo sometimes itakukost.

Kuna mambo ambayo wakishauri inabidi uyafuate kama walivyoshauri. Lakini, kwa nini uanze kujenga chuki na mtu ambaye hata hujamuona? Huwa naamini kwamba mama ana uwezo wa kumsoma mtu na kutambua kwamba anafaa au hafai. Inakuwaje anakuwa defensive? Ni nini anachopigania?
 
Rafiki wazazi wetu walio wengi wana desturi hizo kwasababu hata enzi zao wao wakiolewa kulikuwa na ile hulka kwamba watu wa kabila fulani si zuri kuoa n.k kwahio hio fikra bado wamebaki nayo.. mimi mama yangu mpaka leo hii ana tabia hizo na anataka anichagulie mume,nikimpa green light mbona atapiga vigelegele,wamama wana ile tabia ya kuwa overprotective kwamba wanajua yaliyobora kwa watoto wao aidha awe wa kike au wakiume!Na kama kawaida ya wanawake wote wanapenda kuongea mpaka dini zimesema; kwahio asipopata atakalo lazima atabwabwaja sana tu!

Unajua nilimsikiliza mama mpaka nikapata hasira kama mie ndio ninayezuiwa. Wanafaa kuwa washauri na sio waamuzi wakuu. wao wenyewe sasa hivi ukiwaambia wakutafutie mchumba hawawapati ila tuu wanalazimisha mtu wa kabila lao. Mbona kina baba huwa hawaulizii mambo kama haya?
 
Wanaume kiasilia sio watu wakujali sana haswa vitu vidogo vidogo hivo kama wanawake!Wanawake ndio tulivyoumbwa vitu vidogo tunavikuza na kuvifanya big deal…Na unayoyasema ni kweli wazazi wanatakiwa wawe washauri na si waaumzi kwasababu sio wao wataoishi na huyo mtu!Naweza kuongezea kitu pia lakini naomba usiwe offended:USHIRIKINA pia nadhani unahusika,na wamama wengi wanapenda ushirikina,akienda kwa kalumanzila akipigwa ramli anaambiwa huyo mwanamke hafai blah blah blah basi nae na imani yake potofu mtu anaamini;na kuwa na msimamo hasi kwamba hataki binti huyo awe memba wa familia!
 
Hii imenikuta na mimi yaani alivyonipelekwa tu kwa mama yake na kunitambukisha yule mama alicheka kicheko flani hivi,toka hapo mpendwa wangu akanibadilikia kabisa,huwa sipati jibu alimweleza nini mwanae juu yangu.ila sijawahi kuona mtoto wa kiume kuwa karibu na mama yake kiasi kile na mwanaume mwenyewe kutwa kumsifia mama yake tu.
 
mama yangu ananiambiaga neno moja MWANANGU MUNGU AKUSAIDIE

Kweli kabisa. mi natamani kina mama wote tuwaombee watoto wetu awe wa kiume au wakike....wapate wenza watakao weza kuishi kwa amani ..upendo na masikilizano. Tuache tabia za kutoa hukumu kwa kigezo cha ukabila. Na kwa hali ilivyo sasa watoto wanakutana na wenza wao huko vyuoni kama si mashuleni. Tuwaombee na ni vizuri tuwashauri sio kuwaamulia au kuwapangia
 
Back
Top Bottom