Wamachinga ni kwanini Wanachoma MOTO pia OFISI za CCM??

Wamachinga ni kwanini Wanachoma MOTO pia OFISI za CCM??

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803

KWA NINI WANACHOMA MOTO OSFISI ZA CCM..?



1045097_331270930337757_264328690_n.jpg
​


Wale mashabiki wataendelea kunipinga, kwa sababu wako kama maroboti, yanafanya kazi kulingana na jinsi yalivyoelekezwa, na hapa wapo waliolekezwa kubishabisha tu kila kitu. Na hapa endeleeni kubisha kasha mpinge. Mmesetiwa hivyo.

Leo kumeibuka vurugu kati ya Wamachinga na Polisi. Kwetu haishangazi, mapambano haya hayajaanza leo, na sioni kama yataisha kesho. Yalitokea Mwanza, Mbeya, Iringa na Dar es Salaam.

Bila haya kuna watu wakaanza kuyahusisha na vyama Fulani vya kisiasa huku ukweli wakiuficha kwenye makoti ya suti zao. Unamtoa Mmachinga Manzese, unampeleka wapi? Umemwandalia wapi pa kufanyia biashara? Je, pana kidhi mahitaji ya mwanadamu, yaani choo nk? Kama hayatazingatiwa haya, sioni mapambano haya yakifika mwisho.

Hayo ni kidogo, lakini kuna taarifa kwamba iko ofisi ya CCM imechomwa moto. Kama ni kweli, kwa mtu mwenye upeo anaweza akajiuliza swali, je, Kwa nini wachome ofisi za CCM moto?


*** LOWASSA alionana na Wamachinga wa MWANZA!!!!
 
Safi sana, choma maCCM choma choma kabisa.good job! :target:
 
wameshamwelewa adui yao mkubwa ni yupi ...hongereni sana chings
 
Unafikiri kwa sababu ni wamachinga hawawezi kuona chanzo cha matatizo yao?! Hawa jamaa wanajua kwamba ofisi za kijani ndiyo chanzo cha matatizo yao.
 
Wanaochoma ni wafuasi wa Chadema wala siyo machinga.
 
Na bado afadhali watu wameamka
Nchi hii imewekwa rehani
hela zimefichwa nje
hakuna hospitals, elimu ndo kwa heri
wanawake wanajifungulia sakafuni na kulala na vichanga vyao sakafuni
maccm wanatuletea blaa hadi kieleweke
 
Wanaochoma ni wafuasi wa Chadema wala siyo machinga.

endeleeni kuwaza hivyo hivyo badala ya kuangalia tatizo ni nini nyie mnarukia kwenye hukumu moja kwa moja,wanochoma ofisi za ccm;
1.kwa sababu ndio chama kilichoshikilia dol.a

2.ndio chama kinachopitisha na kutetea sheria kandamizi kwa mwananchi mnyonge
 
Bado ikulu

Sent from BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Chilisosi; Mleta mada amesema wanaohusisha jambo hili na vyama fulani wanatumiwa, je wewe si mmojawao? Mleta mada anataka kujua, wanapohamishwa machinga bila kuandaa mazingira bora na miundombinu ya afya kama maji,choo na umeme...hizi ni sera za gani?
 
Last edited by a moderator:
Kwa nn wasichome kituo cha polis? Au waagizaji wako ccm nn
 
Wanaochoma ni wafuasi wa Chadema wala siyo machinga.

matak..(some text missing) yako,unadhani chadema wana akili za ki-maku kama za ccm na faller wenu nchemba,ndio wajue sasa watu wameshalijua tatzo.U-MAKU-MAKU wenu huko huko na cuf wenu.
 
Wamechoma ofisi za ccm sababu sisiemu dio chanzo cha matatizo yao toka tumepata uhuru.
 
Wanaochoma ni wafuasi wa Chadema wala siyo machinga.


BINGO.... Nilitegemea JIBU HILO - Sababu Tumeshakuwa Wavivu wa KIMAENDELEO; tunajazana OFISINI kufisadi; kuongelea UDINI; kubaguana

Nyerere is GONE is time to DESTROY DAMN NATION... Hakuna tena anayefikiria anything wrong in this nation run by CCM is CHADEMA... Waache Wazungu waje wachote waondoke sisi tunabaki ni sababu ya CHADEMA...
 
Nakumbuka nilipokuwa boarding school, vurumai zikitokea (labda chakula kibaya au whatever) hasila zetu tulizipeleka katika nyumba za walimu. Tulidhani walimu ndio chanzo cha matatizo yetu, wanaiba pesa zetu, hawatupendi, and you name it. Leo hii naomba kwa M/Mungu atusamehe madhambi yetu. Tuliwaonea na kuwadhulumu walimu wetu, wao pia walikuwa na matatizo makubwa, lakini wakiingia darasani, matatizo yao yote waliyaacha mlangoni. Nadhani wengu mtakubaliana na mimi ya kuwa, tatizo ni serikali. Sawa na wamachinga kuchoma moto office za CCM, hawalijui walitendalo. watendaji wa CCM kata au wilaya/mkoa, hawana uhusiano wowote na mipango miji. Hao wananchama wanajichangisha, kuuza vyao na kuomba omba kujenga sehemu ambayo watakutana na kuongelea maendeleo yao. Tatizo ni serikali, aliyetoa order ni Mmachinga mwenzao Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam (shoka halikati mti, mpaka liwe na kipande cha mti), watekelezaji tunaishi nao mitaani, office zao tunazijua, je nini kinachowashinda nyie wamachinga?
 
Hao tunawajua tayari ni watu wa aina gani

BAVICHA NI JANGA LA TAIFA


Mmewashika hao Wahalifu au MNAJISEMEA tu? Juzi LOWASSA alikuwa na Mmachinga wa MWANZA amewanunulia JEZi na kuwapa checki ya Sh. Million 20 -- Hivi LOWASSA anatoa wapi hayo MAPESSA?

Na alifukuzwa kazi ya UWAZIRI MKUU??? Kwanini Mapokezi yake ni ya AINA HII??? Anajua kujipendekeza na hizo senti zake

1.+LOWASSA+3.jpg



1.+LOWASSA+11.jpg


c.c Ritz
 
Wamechoma ofisi za ccm sababu sisiemu dio chanzo cha matatizo yao toka tumepata uhuru.

Uhuru upi?kama wa tanganyika basi haipo nchi hiyo,kama ni tanzania basi haijawahi kupata uhuru nchi hiyo,watanganyika bado watumwa na mtaendelea kuwa hivyo mpaka mkiweza kuuondosha ukoloni mweusi.
 
Wamechoka serikali isiyo sikivu.
 
Back
Top Bottom