Tafakuri huru: Choma choma moto ya Ofisi za Vyama vya Siasa, siyo janja janja ya kutafuta kura za Huruma ya Wananchi?

Kejuu

JF-Expert Member
May 20, 2020
645
906
Ndugu zangu watanzania,

Kwakweli Mungu ni mwema kwa ametupa siku ya leo tena.

Ndugu zangu, inapotekea vipindi kama hivi, watu wanatafuta kura, watatumia mbinu mbali mbali, hasa wale ambao wenye sera mfirisi. Nimejiuliza maswali kadhaa hivi:
 1. Je, ni kweli Chama Cha Mapinduzi (CCM), wachome moto ofisi ya chama cha siasa ili wajipatie kura?
 2. Kura zinatokana na kuchoma moto office ya chama cha siasa?
 3. Je, mnazijua vizuri huruka za wabunge wa majimbo ambako office hizo zimechomwa moto? Wengine si wako kwenye idala ya ujasusi wa vyama hivyo?
 4. Je, uwezekano wa kujichomea haupo pale kweli?
 5. Kwani haya matukio hayawezi kuwa na correlation na hili (
 6. Je, huu si mpango wa kuharibu taswira ya uchaguzi, ili matamko kama ya balozi fulani hivi kuwa na nguvu?
 7. Je, inakuaje mgombea fulani hivi anafanya dhiara mpaka usiku (


Ushauri wangu kwa vyama kama hivi, wajikite kwenye sera tu, sisi wananchi tunawasikia, tutawapima, then tutafanya maamuzi October, 28, 2020.

Asante,
Nawasilisha,
Kejuu
 
CCM wacheni utoto wenu, mnachoma moto ofisi za Chadema maeneo ambayo mnajua wazi hamkubaliki ili muwatishe wapiga kura wa maeneo hayo wasijitokeze siku ya kwenda kupiga kura, mnajidanganya, mjue fika KURA ZITAPIGWA NA MSHINDI HALALI ATATANGAZWA.

Hayo maigizo yenu ya kitoto mnayoleta mnapoteza muda tu, liwake jua inyeshe mvua, pakuche pasikuche, lazima wapinzani wa maeneo hayo washinde, wenyewe mmejionea muziki wa Lissu ndio maana mmeanza kutetemeka.
 
CCM ndiyo wanafanya hujuma huzi na wameandaa mavuvuzela yao kudai kuwa ni Chadema ndiyo wanachoma Moto hizo ofisi zao lakini mbona hawaendi polisi kutoa ushahidi huo? CCM mna siasa za kishamba sana,ila mjue safari hii kila pigo litajibiwa kwa pigo lenye ukubwa maradufu
 
 • Nzuri
Reactions: BAK
CCM ndiyo wanafanya hujuma huzi na wameandaa mavuvuzela yao kudai kuwa ni Chadema ndiyo wanachoma Moto hizo ofisi zao lakini mbona hawaendi polisi kutoa ushahidi huo? CCM mna siasa za kishamba sana,ila mjue safari hii kila pigo litajibiwa kwa pigo lenye ukubwa maradufu
Sasa hizo zitakuwa pepo mkuu
 
Endeleeni kujidanganya, safari hii hachezewi mtu, wala hadanganyiki mtu, upinzani watashinda na mtawatangaza washindi, waambie na wenzio.
Jitoeni ufahamu, mtaona kimbuga kitavyowakumba mkuu
 
Hayo maswali vyombo vyetu vya kulinda na uslama vifunue!
 
Yani suala la uchunguzi wa kipolis unaita tafakari!! Sasa unatafakari nini?

Hata waliotia vurugu Hai pia mlisema Chadema wenyewe!
 
 • Nzuri
Reactions: BAK
Ni tafakuri ya kipuuzi hata mtoto wa darasa la pili hawezi kuitoa! CCM mmezowea kufanya siasa za kishetani alafu mnakimbilia kujenga kujenga hoja za kudifend maovu yenu!

Ni kiongozi gani mjinga au mwanachama wa kwenda kuchoma ofisi zao wenyewe? Hivi ni siku gani ulimsikia Lissu au kiongozi yeyote wa CHADEMA akisema anaomba wampe kura za huruma?

Si ndio ninyi kipindi flani hapa baada ya viongozi wa CHADEMA. Freeman Mbowe, Mch. Msigwa , Lazaro Nyalandu na wengine, baada ya hawa viongozi kutia nia ya kugombeda urais, mkazusha eti wameyakimbia majimbo yao kuogopa aibu ya kushindwa katika uchaguzi mkuu ujao, si hao wamerudi majimboni kwao!

Acheni kuwafanya wananchi ni mazuzu, jibuni hoja kwa kutumia hoja na si vingnevyo!
 
 • Nzuri
Reactions: BAK
Ni tafakuri ya kipuuzi hata mtoto wa darasa la pili hawezi kuitoa! CCM mmezowea kufanya siasa za kishetani alafu mnakimbilia kujenga kujenga hoja za kudifend maovu yenu! Ni kiongozi gani mjinga au mwanachama wa kwenda kuchoma ofisi zao wenyewe? Hivi ni siku gani ulimsikia Lissu au kiongozi yeyote wa CHADEMA akisema anaomba wampe kura za huruma??? Si ndio ninyi kipindi flani hapa baada ya viongozi wa CHADEMA. Freeman Mbowe, Mch. Msigwa , Lazaro Nyalandu na wengine, baada ya hawa viongozi kutia nia ya kugombeda urais, mkazusha eti wameyakimbia majimbo yao kuogopa aibu ya kushindwa katika uchaguzi mkuu ujao, si hao wamerudi majimboni kwao! Acheni kuwafanya wananchi ni mazuzu, jibuni hoja kwa kutumia hoja na si vingnevyo!
Umeyasoma maswali hayo vizuri mkuu?
 
Umeyasoma maswali hayo vizuri mkuu?
Mkuu nimeyasoma yote! Nazani sote tulisoma mambo ya Comprehesion kwenye somo la English, Kichwa tu cha habari kimeonyesha mtazamo wako ni kujaribu kushawishi jamii iyaone matukio hayo haramu kama maigizo na mambo ya kutaftia kiki kwa wananchi, kitu ambacho si kweli na hakina kabisa uhalisia wowote na matukio hayo! Nani hazifahamu tabia au nature za DC Sabaya au RC Chalamila?? Mbona hata majuzi tu hapa Mbunge Sugu kakamatwa akichukuwa form ofisi ya NEC? Kwanini Hatjasikia hayo yakitokea kwa mgombea wa CCM Tulia aksoni ambaye kwanza alishaanza kampeni hata kabla ya wakati?
 
 • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom