Alichosema mtatiro kuhusu vurugu za zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Alichosema mtatiro kuhusu vurugu za zanzibar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ALEX PETER, May 29, 2012.

 1. ALEX PETER

  ALEX PETER Senior Member

  #1
  May 29, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mtatiro-julius.jpg
  [h=6]HILI LA ZANZIBAR HALIUNGWI MKONO “LABDA NA MWENDA WAZIMU TU”

  Habari za uchomaji wa makanisa Zanzibar katika vurugu za hivi karibuni haziungwi mkono kwa namna yoyote ile. Yeyote anayefanya vitendo hivi ni gaidi kwa sababu anafanya vitendo vya kigaidi. Serikali ya zanzibar ichukue hatua kali sana za kisheria kwa yeyote aliyehusika na vitendo hivi bila kujali yeye ni nani.

  Kuchoma makanisa ni jambo la hatari sana, sielewi anayefanya hivi yeye ni dini gani, sijui ni dini ipi inayoruhusu uchomaji wa nyumba za ibada za dini nyingine, ni dini ya shetani peke yake inaweza kufanya hivyo.

  Kuna watu wanasema ati ni “waislamu” ndiyo wanafanya vitendo hivyo, mie nakataa, nasema wanaofanya hivyo siyo waislamu. Waislamu walioko Zanzibar naowajua mimi ni wakarimu, ni watulivu na wasikivu na wanapenda amani. Hata mapambano ya wafuasi wa CUF na CCM yaliisha kwa wao wenyewe kuridhiana.

  Wazanzibari siyo wakatili kiasi hiki. Kuchoma makanisa hakuwezi kufananishwa na kuchoma Mahakama, ikulu,polisi n.k. Uchomaji wa makanisa au misikiti ni uchonganishi mkubwa unaoibua vita mahali pengi duniani. Anayefanya hivyo ana malengo mabaya sana siyo kwa wananchi wa Zanzibar tu bali kwa wananchi wa wa Tanzania kwa ujumla.

  Hii ni kwa sababu makanisa yakishachomwa tetesi zinasema wamechoma waislamu(jambo ambalo siliamini), tetesi hizi zikizidi na pakatokea athari kubwa kwa makanisa na labda watu(wakristo) wakachomwa na kufariki ndani ya makanisa hayo, ina maana wakristo watapoteza ndugu zao.

  Kama Zanzibar pana wakristo wachache ambao hawawezi kulipiza kisasi cha adui wasiyemjua, lazima ndugu zao wakristo walioko bara watataka kulipiza kisasi kwa wazanzibari(waislamu) walioko Tanganyika ambao wamejenga na kuoa na kufanya biashara Bara na ambao hata ZAN ID(Vitambulisho vya ukaazi vya Zanzibar hawana) – kwamba kwa sheria za uraia za Zanzibar hata wakirudi kesho hawatambuliki kama wazanzibari.

  Nakadiria kuwa kuna wazanzibari takribani laki tatu au laki nne walioko Tanganyika. Wengi wao wana maduka na biashara nyingi, wamenunua mashamba yao huku Tanganyika na kwa kweli maisha yao na vifo vyao na maziko yao viko huku Tanganyika kila inapotokea.

  Sasa fikiria hawa “magaidi” wanaojivalisha na kusingizia waislamu watakapoendelea kutuchonganisha na tukajikuta hasira zimepanda kila upande. Utastukia mali za wakristo na makanisa yanachomwa na hata wahusika kuuawa huko Zanzibar na utastukia pia wazanzibari walioko Tanganyika nao wanaanza kuhujumiwa mali zao na kuuawa na “magaidi” wa bara watakaojivisha joho la “ukristo” au “joho la kuwapigania ndugu zao waliouawa Zanzibar” kwa maslahi yao.

  Mchezo huu utaendelea mbele, kwa sababu wazanzibari wengi watakaouawa na kuhujumiwa huku Tanganyika ni waislamu(hii ni kwa sababu asilimia 99 ya wazanzibari ni waislamu) itapelekea waislamu wenzao ambao ni mamilioni walioko Tanganyika kutaka kuwatetea waislamu wenzao wenye asili ya Zanzibar. Hapo ndipo itaibuka vita kamili ya dini ya kikristo na kiislamu(Naomba haya yatokee wakati sipo duniani, naomba nisishuhudie ukatili wa Rwanda ndani ya nchi ninayoipenda kama Tanzania).

  Vita ya kidini, lol! Mamilioni watateketea, malaki watachinjwa, akina mama watabakwa, watoto watanajisiwa…..what a hell? Wendazimu wachache waliochekewa watavaa majoho ya dini…..CNN watatangaza vita ya kidini Tanzania, Mashirika ya kimataifa yataingiza misaada na geresha huku nchi inahujumiwa. Vikundi vya waasi kina Kony na mwenzie nao wataingia kutuunga mkono, hatimaye Tanzania itageuka kuwa jehanamu ya duniani. Nyerere na wenzie watakuwa wanalia na kupiga vifua vyao kwa huzuni kuu. Kisiwa cha amani kimegeuka kuwa Dimbwi la maafa na laana ya damu za mauaji.

  Mambo haya huanza kama mchezo tu. Na yameanza, hakuna mtu mwenye haki ya kudai haki yake na kuhujumu mali za watu wengine na kuchoma makanisa ya watu wengine. Wanaofanya vitendo hivi ni wahuni wakuu na serikali ya Zanzibar ichukue hatua kali sana.

  Uhuni wa namna hii ulitokea pale Tandahimba mwezi uliopita ambapo “polisi” walihusika “live” katika oparesheni ya kikatili ya kuchoma “waziwazi” maduka zaidi ya 55 ya wafanyabiashara na gari moja na pikipiki moja. Kabla hawajaanza oparesheni “ushenzi” hiyo “polisi” walitengeneza tukio kwa “kuichoma” ofisi ya OCD ili wapate nafasi ya kulipiza kisasi kwa wananchi wasio na hatia(kisasi cha kutengeneza) – Ujinga ulioje, aibu iliyoje?

  Pana makundi yanadai Zanzibari huru, yaachiwe uhuru wao, yasikilizwe. Wajanja wasijitokeze wakatumia upenyo huo ili kuyavunja makundi hayo kwa kuyabambikizia uchomaji makanisa ili kuyahusisha na hila za dini moja kuhujumu dini nyingine, tuache michezo hii ya kipuuzi. Siamini kama uamsho na wanaharakati wale ndio wanachoma makanisa, naamini kuna janja nyuma ya suala hili. Labda pana wajanja wanataka kuua “move” ya mjadala wa kudai Zanzibari huru.

  Majuzi wazanzibari waliamua kuwa na serikali ya umoja wa kitaifa, wakapiga kura wakaamua sawia na serikali yao ikawa, hawakutushirikisha kwa sababu peke yao wanaweza kusimamia na kuendesha mambo yao na tumeona wanaweza. Mie nasema wazanzibari wakidai Zanzibar huru yao tusiwapige na kuwakamata na kuwanyanyasa, tukae nao mezani tusikilize hoja zao. Na kama wengi wao wakitaka Zanzibar huru yao tuwape.

  Baba yangu mzee aliyeko kijijini hatapungukiwa na lolote iwapo Zanzibar itaendeleza muungano na Tanzania au itajitoa. Zanzibar ikijitoa katika muungano haitaongeza wala kupunguza kilo ya sukari au kilo ya mchele. Watanzania wana matatizo makubwa yanayotishia uhai wao kila kukicha kuliko muungano huku Tanganyika . Muungano ni jambo la kisiasa tu na kama “mkuu wa kaya anasema usijadiliwe” lazima utavunjika tu, hana namna ya kuuokoa maana kushindana na umma wa upande mmoja ni kazi bure.

  Mie nawashauri sana pia wana vikundi vya uamsho na na watu wote wanaodai Zanzibari yao kuwa watumie busara na njia za kawaida sana kudai haki yao wanayoiamini. Kwa sababu tume ya jaji warioba inakwenda kukusanya maoni ya katiba waisubiri, ikifika waioneshe na waieleze kuwa hawautaki muungano.

  ”Majority of zanzibaris” wakiwa na msimamo huo maana yake ni kuwa katiba ya Tanzania “itafeli” kwa sababu lazima ipitishwe na pande zote za muungano kwa uwiano sawa. Hii ni njia nyepesi sana kuliko njia zingine, wanaweza kuendelea kutoa elimu juu ya kuupinga muungano kwa njia ya makongamano na mikutano tu. Hii itawasaidia kutengeneza mtizamo mzuri na kuondoa uwezekano wa watu wowote wenye nia mbaya kutumia shughuli zao na kujenga taswira mbaya sana zinazoweza kuweka amani, usalama na mshikamano wa wananchi hatarini.

  Mwisho ni kwa serikali zote mbili, hii ya Jakaya na ile ya Shein na Maalim Seif. “Movement” hii ya uamusho na makundi mengine ya kijamii, kiharakati na kidini upande wa Zanzibar ya kudai kuvunja muungano siyo jambo la kubeza na kuchezea. Ukiwatizama wale uamsho utaona umati wa watu wanaokusanya ni mkubwa kuliko mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa. Hii ina maana kuwa panahitajika busara na nia thabiti katika kumalizana na wananchi hawa.

  Serikali zote mbili zikae nao chini na kutatua suala hili. Ni bora kuuvunja muungano kwa heri(kwa utaratibu), kuliko kuuvunja kwa nguvu. Muungano ukivunjika kwa nguvu na ghafla patatokea mpasuko mkubwa sana. Pana ma-laki ya wazanzibari wako Tanganyika, pana mahusiano makubwa yameshajengwa. Tunahitaji “mechanism”na akili nyingi kulishughulikia.

  “Nguvu na mabavu havitasaidia kuzima mawazo thabiti ambayo wananchi wanayaamini, nguvu na majeshi vinaweza kuua mwili tu lakini haviui dhamira” Hata kama wananchi hawa watapigwa na kukamatwa na kuwekwa gerezani moto huu hautazimika. Muungano utizamwe upya, tusikilize matakwa ya wananchi wengi, ikiwa wengi watasema uvunjwe basi na tuuvunje kwa amani.

  (Haya ni maoni yangu binafsi, kwa namna yoyote ile yasihusishwe na chama changu wala uongozi wangu ndani ya chama).

  Julius Mtatiro +255 717/787/ 536759,
  Dar es salaam,
  29 Mei 2012.[/h]
   
 2. B

  Babuu Rogger JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 80
  Kaaazi kwelikweli.
   
 3. franktemu123

  franktemu123 JF-Expert Member

  #3
  May 29, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 775
  Likes Received: 299
  Trophy Points: 80
  Pumba tupu Mtatiro! siasa haikufai kaka rudi kwenye taaluma uliyosomea. Hapo CUF wanakutumia tu kama Muhuri lakini hawakupendi CUF japo mwanzilishi wake alikuwa Mkristu (James Mapalala) wahuni kina Maalim Seif/Lipumba wakampoka chama hata hii ndoa ya CCM na CUF imefanikiwa kwa kuwa Ba Riz(CCM) na Uongozi wa juu wa CUF dini moja wanajadili mambo yao msikitini ambako wewe Mtatiro huwezi kuingia. SHTUKA MTATIRO UNATUMIWA na wewe kwa sababu una njaa unakubali bila kujijua.
   
 4. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #4
  May 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,255
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  kwa hiyo naona Mtatiro anaweka assumption kwenye vitu vilivyo wazi kabisa! Kuna siku naona atakuja na tamko mambo yanayotokea, yanatokea yenyewe hayasababishwi kutokea. Kwa hiyo anajaribu kutuambia wamechoma waumini wa hilo kanisa wenyewe au anataka kutuambia yanajichoma moto yenyewe hakuna mtu anaeyachoma! Unajua kutetea upumbavu ujasiri fulani unahitajika kidogo!
   
 5. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #5
  May 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Kwanza Kiongozi wa aliyeidhinisha kuchomwa hayo Makanisa Jina lake lipelekwe kwenye Majina ya Materorist Duniani; na pia wachunguze hicho chama chake wapi wanapata pesa ili huyo mtoa pesa ashitakiwe sababu wanatumia hizo pesa kubagua wananchi wenye asili ya kikristo.

  Yaani hii Iwe CIA na British Intelligence Issue; Angalia watalii wameogopa kwenda Zanzibar; HUYU MTU NI GAIDI
   
 6. K

  Kimbito nyama Senior Member

  #6
  May 29, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 157
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimejaribu kumwelewa Mtatiro kuwa waliochoma makanisa si Waislamu wote bali ni wachace tu wenye ni zao mbaya!
   
 7. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #7
  May 29, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na Mtatiro 100%

  Serikali yenyewe kwa kushirikiana na hao viongozi wa makanisa au bila kushirikiana nao, ndio waliochoma hayo makanisa.

  ilikuwa vigumu, kwa serikali kuwasimamisha wale jamaa na ndio maana wakatumia trick hii waliyoitumia sasa.

  Mwenye akili na afikili, kulikuwa kuna uhusiano gani kwa waziri wa mambo ya ndani kuongozana na balozi wa US,UK,CANADA na wengineo kuzungumza na UAMSHO ?

  This was planned na i swear HAWATAFANIKIWA.

  MAKANISA YAMECHOMWA NA USALAMA WA TAIFA KUSHIRIKIANA AU BILA KUSHIRIIANA NA VIONGOZI WA DINI.
   
 8. a

  abu alfauzaan Member

  #8
  May 29, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  umenena ndugu,
  wambie na ao wehu wakibara,
  waache ku2ngangania,
  2ko tayar 2kose sote,unles mu2achie nchi ye2,
  wezi,wahuni,wanyama nyinyi,2peni nchi ye2 mijizi mikubwa
   
 9. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #9
  May 29, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  kwahiyo mtatiro anataka kusema aliyechoma makanisa anatoka huku bara au nje ya nchi?
   
 10. S

  Swalihina New Member

  #10
  May 29, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unajuwa waswahili nadhani uwa wanatizama picha za njee wanao fanya madamano na wao hujaribu ili wapate kuonekana ktk Tv na kusikilikana ktk Radio lakini wajuwe amani ni kitu muhimu sana kama walijaribu wamepata wasifanye tena

  hebu tutizame mtume wetu SWA alifanyaje alipo igombowa Meeka panapo muhimu kupigana tupigane laa pana umuhimu kuzungumza na hili linawezekana
   
 11. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #11
  May 29, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mtatiro,sijakuelewa,kwa hiyo makanisa yamejichoma,na hata kama ni kikundi cha wahuni unavyosema hawana dini,je hii mihadhara ulikuwa huioni.Kumbuka wenye akili walipata kutahadharisha,mficha malazi kifo humuumbua.Msalimie mtume wa mnyaaaaazi mungu a.k.a maalim seif
   
 12. Mangaline

  Mangaline JF-Expert Member

  #12
  May 29, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 1,052
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mkuu, Alex Peter, Aksante sana kwa kuleta uzi huu. Mawazo ya Mkuu Mtatiro ni mawazo ya busara sana, na Tuombe Mungu amfunulie mafunuo haya Mkuu wa kaya, asiwe na roho kama ya mtangulizi wake, yasijetokea kama yale ya zanzibari ya 20.., ambapo walikimbilia shimoni, na kugeuza kisiwa cha amani kikawa ziwa la damu. Tuombe busara za bunge, kikao cha kwanza cha bunge cha mwezi june, kiondoe sheria inayo kandamiza uhuru wa watu kutoa maoni yao juu ya muungano.
  Kwa upande wa pili, tusilaumu tulipoanguka, bali tuangalie tulipojikwaa. Ndugu zetu wa zanzibari wamekuwa na mengi juu ya muungano, na kila njia ya amani waliyotumia, ilikutana na mkono wa chuma, uliogandamiza maoni yao kwa mabavu. Kumbuka, yuko wapi Aboud Jumbe!, Kutokana na matumizi ya mabavu ya muda mrefu, busara haiwezi kutumika, ila kila njia, bila kujali kama inajenga au inabomoa, itatumika. Hivyo yaliyotokea, ni matunda ya serikali kutumia mabavu katika kulazimisha mawazo yake.
  TUOMBE AMANI, HAKUNA ATAKAYENUFAIKA NA MACHAFUKO. WANANCHI TUTAUMIA, VILEVILE WATAWALA WATAUMIA. HAKUNA FAIDA YA MACHAFUKO.
  MUNGU IBARIKI TANGANYIKA, MUNGU IBARIKI ZANZIBARI, TANZANIA R.I.P.
   
 13. S

  Swalihina New Member

  #13
  May 29, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tuweche kijichokowa jicho kwani halina utani ukikosea maoteo yake ni kupofuka na kupata ulemavu wa kudumu mwisho wake utaitwa chongo lakini kama unge tulia ukamwambia mtu akutizame jicho lako kuna nini aidha kwa haraka haraka ungepulizwa au ungepata dawa jicho likawa powa ni bora kutumia busara zaidi kuliko hasira tunachoma mipira tena njiani barabara zinaunguwa jee hasara ya nani hebu tukae tuone hawatosikia kilio cha watu au wabishi nasema tena jicho tusilitofuwe nanyi bara msitupe maneno yalio mabaya nyie mnatakiwa mseme pole tu na si vienginevo tumieni busara zaidi kuliko mambo mengine.
   
 14. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #14
  May 29, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,499
  Likes Received: 19,914
  Trophy Points: 280
  astagafulilah
   
 15. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #15
  May 29, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  namshangaa anasema waliochoma makanisa si waislamu-naona anataka kujidanganya mwenyewe-kwani aliyechoma hayo makanisa ni nani kama si waislamu?naona anataka kuwatetea ndugu zake-in either way-hawawez kujisafisha juu ya hili
   
 16. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #16
  May 29, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,072
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  kweli aisee!. wewe ndo umedhihilisha yaliyomo moyoni mwenu. hayo unayo sema ndo kauli za wapemba. hata walioko bara. mimi nmekaa tayari tayari. Mumeanzisha si tutamaliza.
  Kudadadadadadadadadadekiiiiii
   
 17. Tanzania Mpya

  Tanzania Mpya JF-Expert Member

  #17
  May 29, 2012
  Joined: Apr 11, 2012
  Messages: 248
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 45
  Nami nakubaliana na hayo hapo juu. Muungano huu unaonekana kuwa mali ya viongozi wa ccm tu, ndiyo maana hawataki ujadiliwe. Kwani umekuwa Mungu huu kwamba waumini wakihoji watakufuru au watalaaniwa? Kama muungano upo kwa ajili ya mwananchi naye anaulalamikia kwa nini kuendelea kumlazimisha aabudu? Huku nako ni kukiuka haki za binadamu ambako serikali imelalamikiwa jana tu na tume ya haki za binadamu. Wananchi tuulizwe, tuseme bila woga nini tunataka. Mungu ibariki Tz.
   
 18. k

  karafuu Member

  #18
  May 29, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hivi vurugu za arusha cdm walikiteka kituo cha polisi wakavunja miundombinu?
   
 19. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #19
  May 29, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  masikiiiini kijana mdogo lakini bado hajitambui.
   
 20. M

  Mwakyonde JF-Expert Member

  #20
  May 29, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  na wewe ni moja ya haya retards, zanzibar hamlimi hata nyanya, siku mkijitenga na njaa itakua imeingia kwenu
   
Loading...